Miss World: Sheria zinawazuia akinamama kushiriki ni za 'kibaguzi '

Veronika Didusenko ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano Haki miliki ya picha BRIGHTON PICTURES
Image caption Veronika Didusenko ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano

''Masharti ya kuingia katika mashindano ya Mrembo wa Dunia yana ubaguzi …hakuna nafasi yake katika karne hii ya 21''

Mrembo Veronika Didusenko mwenye umri wa miaka 24, alishinda taji la mrembo wa Ukraine (Miss Ukraine) mwaka 2018 lakini alinyang'anywa taji hilo pale waandaaji walipogundua kuwa ni mama.

Sheria za shindano zinapiga marufuku mrembo yoyote kushiriki katika mashindano yatakayoruhusu kushiriki katika mashindano ya mrembo wa dunia kama wakiwa na watoto.

Na sasa Veronika, ambaye ana mtoto mwenye umri wa miaka 5, ameamua kuchukua hatua za kisheria kwa waandaji wa mashindano hayo kuhusu sheria zao.

''Nataka niwabadilishe, na kuwapa changamoto. Nataka nihakikishe sheria za kushiriki mashindano ya urembo wa dunia zibadilike na zilingane sawa sawa na wakati huu.'' Aliiambia Radio 1 Newsbeat.

''Nataka niwaweke sawa kutokana kwa maisha ya sasa na kuangalia maisha halisi ya wanake kwa nyanza hizi, na kutambua kuwa wanaweza kufanya kazi na vile vile mambo mengine nje ya kazi.''

Veronika anadai aliamua kushiriki Taji la ''Miss Ukraine'' kukuza kituo chake cha kusaidia watu na alishangaa alipopewa ushindi wa shindano hilo.

Angeenda kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya urembo wa dunia lakini siku nne baadae alinyang'anywa taji hilo.

'' Ilikuwa ni jambo la aibu na la kufedhehesha kwangu,'' alisema.

''Nilijisikia vibaya kwasababu sio mimi peke yangu ninayofanyiwa haya, ni kitu ambacho wanawake wengi duniani wanakabaliana nacho, ambao labda wanataka kushiriki lakini hawaruhusiwi kushiriki kwasababu tu wana watoto.''

Veronika amekubali kuiona shetia hiyo kwenye fomu ya kuomba kushiriki, lakini alishauriwa kushiriki na waandaji hao.

''Kwanini mwanamke akataliwe kushiriki kwasababu tu ni mama? Haitii maanani kabisa''

''Kuwa mama haileti madhara yanayomzuia mshiriki kufanya kazi au kuwa mwanamitindo au kufanya kazi zangu.''

''Kwahiyo sheria hizo hazikuleta maana yoyote kwangu.''

Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wa shirika la ''Miss World'' Julia Morley, aliulizwa kuhusu sheria hiyo katika mahojiano mwaka jana.

''Unapojaribu shirika la kimataifa likubaliane na wewe, inabidi uangalie kila mtu na wanapiga kura kulinagana na yale yaliyoruhusiwa.'' Aliiambia Good Morning Britain.

''Chochote ninacho hisi mimi au unachohisihisi umoja wa ulaya ni kitu kingine kabisa kulingana na kile sehemu zingine za dunia wanazo kubaliana nayo, inabidi waangalie sheria zao za kidini na mambo mengine kadhaa.''

''Kama unanielewa vizuri hatuna hisia zetu pekee, inabidi tuzingatie na hisisa za wengine. Kwahiyo tunalolifanya sisi ni kutafuta usawa kwa pande zote mbili.''

Ndani ya mwaka 2014, kiongozi wa shindano la urembo nchini Uingereza lijulikanalo kama 'Miss England competition' Angie Beasley, alisema itakuwa ngumu sana kwa washindi kugawanya muda wao kwa kazii hii ya urembo na kuwa mama.

Akizungumza na kituo cha habari cha ITV Bi Angie alisema ''Kitendo cha mama kusafiri sehemu mbali mbali duniani akisaidia vituo vya kutoa misaada kwa watoto kwa mwaka mmoja, ni jambo halimtendei haki mtoto pamoja na familia nzima.''

''Inaleta matatizo pale linapokuja swala la nani atamlea mtoto au watoto wa mama yule aliyeshinda.''

Lakini Veronika anasema mtoto wake yupo vizuri kwasababu smekuwa akisafiri nae kwaajili ya kazi zake.

''Ameona nchi nyingi sana kwa umri wake. Kwa mwangalio wangu naona ni mtoto ambaye anauwezo wa kufikiri mkubwa kuliko watoto wengine.''

''Kwahiyo 'Miss World' kusema wanahofia kuhusu mtoto...Ni jambo la kipuuzi sana kwangu''

Veronika anasema anatumaini kuwa kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kisheria kutawafanya 'Miss World' kubadilisha sheria hiyo. Shindano hilo linaanza mwaka huu mjini London tarehe 14 Disemba.

Anawakilishwa na mwanasheria wa kutetea haki za kibinadamu Ravi Naik ambaye anadai chini ya sheria ya haki swa ya mwaka 2010, sheria hiyo ya kuingilia shindano hilo ni ya ubaguzi.

''Nataka 'Miss World' ibadilishe sheria zake kufanya mashindano haya kuwa wazi kwa watu wote'' amesema Veronika.

''Kwasababu mashindano yanayoruhusu mtu yoyote kushiriki yanaweza kusaidia ubaguzi wa kijinsia, na kutengeneza nafasi za kazi kwa washiriki na kuweza kuwainua wanawake.

''Kwa mfano, nyumba za mitindo nyingi huruhusu wanawake wajawazito, wanawake wenye umbo kubwa na warembo wa umri wowote, kwa ajili ya hafla zao za mitindo.

''Kwahiyo mashindano ya warembo yanahitaji kufuata uongozi wao na kuwasherekea wanawake wote kwa usawa.''

Shindano la mlimbwende wa Dunia lina sheria na kanuni zake

Image caption Baadhi ya Walimbwende wa Tanzania

Mashindano ya ulimbwende nchini Tanzania mwaka 2014 yaliingia dosari la namna hiyohiyo kwa madai ya udanganyifu wa kuwa na mtoto na hivyo kuvuliwa taji la Tanzania kwa mwaka huo.

Bi Basila Mwanukuzi ambaye aliwahi kuwa Mlimbwende wa Tanzania 1998 na sasa ni muandaaji wa mashindano hayo hakutaka kuzungumzia suala hilo la kuwa kile kilichotokea Ukraine kiliwahi kutokea nchini mwake, "sikuwa kiongozi wakati huo hivyo sijui chochote, "

Aliongeza kusema kuwa ,

''Tunafahamu kwamba kila mashindano yanakuwa na sheria na kanuni na taratibu zake ambazo kila mshiriki anatakiwa kuzifuata na katika dunia hii vitu vinasheria zake.''

''Inafahamika wazi kuwa hata sisi hapa Tanzania tunafuata vigezo vya mashindani ya Miss World, kwa sababu Miss Tanzania iwapo hatatimiza vigezo basi akifika mbele ataondolewa, kisheria inatakiwa usidanganye kwa sababu mwisho wa siku ukweli utajulikana.''

Hata hivyo bi Basila ameona kuwa madai kuwa kumuondoa mama katika mashindano ya Mlimbwende wa Dunia kwa kigezo kuwa ana mtoto ni uonevu na ubaguzi ni jambo sahihi.

''Mimi kama mama na nina watoto, ukishakua mama unafanya majukumu ya mama... Miss anakua na majukumu mengi, anazunguka duniani. Ni vigumu sana kupata muda wa kumlea mtoto.

Vigezo vikiwekwa vinakua na sababu zake na ni lazima vifuatwe", Basila anasema.

Newsbeat imewasiliana na shirika la miss world, kuona kama wanalolote la kuzungumza kuhusu swala hili.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii