Rwanda yasaini makubaliano na timu ya Paris Saint-Germain kuimarisha sekta ya utalii

Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,tauzwa katika uwanja wa michezo viwa Paris. Haki miliki ya picha RDB
Image caption Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,tauzwa katika uwanja wa michezo viwa Paris.

Serikali ya Rwanda na mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa wametangaza kufikia makubaliano ya kibiashara kuendeleza sekta ya utalii nchini Rwanda katika kampeni ya kuhamasisha watu kutembelea Rwanda.

Kulingana na Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda (ADB) Bi Clare Akamanzi mapatano yaliyosainiwa kati ya serikali ya Rwanda na club ya Ufaransa ya Paris Saint Germain ni mapana yakihusu sekta mbali mbali :

''Ni katika kuendeleza kampeni yetu ya 'Visit Rwanda' ama tembelea Rwanda. Siyo hayo tu kwani tutatumia pia mitandao ya timu ya PSG nchini Ufaransa na kwengineko . Unajua hii ni timu ambayo ina washirika wengi katika sekta mbali mbali kama viwanda vya nguo na mitindo. Hii itatusaidia kufahamisha dunia yale ambayo na sisi tunayafanya katika sekta yetu ya utalii na mambo mengine yanayotengenezwa hapa Rwanda'', alisema Bi Kamanzi.

Unaweza pia kusoma:

Kwa mujibu wa mapatano hayo ya miaka 3 kwanzia mwaka ujao wa michezo mabango ya Visit Rwanda yataanza kuonekana kwenye uwanja wa timu hiyo wa Parc des Prince na kwenye fulana za timu ya wanawake.

'' Zaidi ya hayo sisi pekee ndio tunaruhusiwa kuuza chai ya Rwanda na kahawa ndani ya uwanja wa PSG wakati wa mechi. Na kila mwaka tutakuwa na kampeni ya wiki nzima inayofahamika kama Rwanda week mjini Paris ni kama wiki ya maonyesho ya bidhaa na utamaduni wa Rwanda mjini Paris'' alisema Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Rwanda.

Leo, ligi ya mabingwa wa Ufaransa imetuma ujumbe wa video kupitia mtandao wa Twitter, unaoonesha wachezaji kama Neymar, Kylian Mbappé, Marco Veratti na wengineo wakisifu maeneo ya kitalii ya Rwanda:

Bodi ya mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, imetangaza kwamba chini ya makubaliano hayo, majani chai na kahawa kutoka Rwanda,vitauzwa katika uwanja wa michezo viwa Paris.

"Bango lenye maneno 'Tembelea Rwanda' litaonyeshwa katika uwanja wa Parc des Princes, kwenye fulana za timu ya wanawake ya Paris Saint-Germain pamoja na nyuma ya nguo zao za mazoezi", tangazo hilo limesema.

Hata hivyo, Rwanda na timu ya PSG hazijasema lolote kuhusu kitita cha pesa walichokubaliana katika kipindi hicho cha miaka mitatu.

Baadhi ya wachezaji nyota wa PSG na baadhi ya nyota wake wa zamani watatembelea maeneo tofauti ya kitalii nchini Rwanda kama njia ya kuuvutia watu wengine duniani kuzulu pia maeneo hayo.

Timu hiyo maarufu ya Ufaransa itachangia pia katika mpango wa kuinua soka ya vijana nchini Rwanda.

Inasemekana kwamba mwaka 2018, Rwanda ilipata mapato ya dola milioni 380 huku mwaka huu ikipania kupata dola milioni 405.

Mei mwaka jana, Rwanda ilitangaza mpango wa ushirikiano na timu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya England.

Inasemekana makubaliano hayo yaliigarimu serikali ya Rwanda dola milioni 30. Pande zote hazijatoa maelezo yoyote juu ya gharama hiyo zote hazijazungumzia.

Unaweza pia kutazama :

Huwezi kusikiliza tena
David Luiz wa Arsenal azuru Rwanda

Ushirikiano huo wa miaka 3 ulilenga kuimarisha sekta ya utalii nchini Rwanda, uwekezaji na maendeleo ya mchezo wa soka.

Makubaliano kati ya Arsenal na Rwanda,yalihusu timu ya kwanza, timu ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 na timu za wanawake.

Pia ilitangazwa kwamba maneno 'Tembelea Rwanda' yatakuwa yakionekana kwenye mabango maalum ya kibiasara ndani ya uwanja wa Emerates wakati wa mechi za Arsenal.

Wakosoaji nchini Rwanda huistumu serikali kwa mapatano hayo wakihoji ikiwa ndiyo kipaumbele cha matatizo yanayowasumbua wananchi.

Akiwajibu wakosoaji wa mpango wa kunadi utalii kwa njia ya timu kubwa, rais wa Rwanda Paul Kagame alisema wakosoaji wanapaswa kuwa na hoja za msingi wanapokosoa jambo, akisisitiza kuwa ni heri kufanya mambo ya maana kwa nchi yake kuliko kuacha kulifanya kwa kuhofia ukosoaji ambao ni lazima utakuwepo.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Sherehe za kuwapatia majina sokwe zafanyika nchini Rwanda

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii