Utaratibu wa kulala na maiti kueneza maambukizi ya ebola DRC

Ebola

Mila na desturi zinatajwa kuwa miongoni mwa changamoto katika shughuli za kupambana na ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Utamaduni ambao wananchi wameuzoea umekuwa ukirudisha nyuma jitihada mbalimbali za kujikinga na maambukizi.

Jinsi shughuli za mazishi zinavyofanyika DRC, kulala na maiti, kumuogesha na kumvika nguo marehemu, ni baadhi ya mila zinazo sababisha kuenea kwa ugonjwa huo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ambapo zaidi ya watu 2300 wamefariki dunia.

Ebola umekuwa ugonjwa sugu na hatari katika eneo lote la mashariki mwa Kongo. Licha ya chanjo pamoja na tiba zinazotolewa kutoka kwa madaktari, lakini jitihada za kuutokomeza kabisa ugonjwa hazijakuwa rahisi.

Maswali kadhaa yameulizwa kuhusu hilo, ni kipi kinachoweza kuwa chanzo na sababu kubwa za kutofanikiwa kwa jitihada hizi.

Daktari Christoph Shako, mmoja wa viongozi katika kamati ya kupambana na ebola mkoani ituri anaamini kuwa ni mila potofu.

Jamii nyingi ya watu wa maeneo ya Beni wamekuwa na mitizamo hasi kuhsu ebola,walio wengi husema kuwa kuwa Ebola si ugonjwa wa kawaida na uliletwa tu kwa manufaa ya watu kujilimbikizia pesa.

Madaktari wanaopambana na ugonjwa wa ebola nchini humo wamewaeleza wanakijiji waliopoteza mama au watoto wao kuwa hawawezi kuwazika jamaa zao kwa utaratibu wa kitamaduni.

"Ni kama hadithi kusikia kwamba mtu ameambukizwa virusi vya ebola na baadae kupata matibabu na kisha kupona".

Mama mjane ambae mume wake alifariki kutokana na ugonjwa wa ebola na kisha kufariki. Aliambukizwa virusi na kisha akapona.

Sasa ana hamasisha wanakijiji kuhusu umuhimu wa kukubali kuwa ebola ipo na kwamba umuhimu pia wa kuachana na mila potofu.

Tamaduni zimekuwa zikikinzana ua kugongana na maelekezo ya madaktari katika mchakato wa kupambana na ugonjwa wa Ebola.

"Baadhi wamekuwa na imani kwamba mgonjwa wa ebola anaweza kupona kwa kuombea au kwa usaidizi wa waganga wa jadi, jambo ambalo limekuwa likichangia ongezeko la maambukizi katika baadhi ya maeneo". Omar kavota ni mratibu wa shirika la CEPADHO mjini goma na ambae amekuwa akihamasisha watu kuhusu ebola.

Kumekuwa na ukosefu wa imani miongoni mwa jamii zilizopo katika maeneo yaliyoathirika na Ebola, baadhi wakiwalaumu wageni kwa kuzuka na kusambaa kwa mlipuko wa maradhi hayo.

Hali hiyo inachangia juhudi za kukabiliana na mlipuko huo kuwa ngumu kwa mujibu wa kamati ya kupana na ugonjwa wa ebola katika majimbo yenye mizozo ya Ituri na Kivu.

Lakini je raia wakawaida wanamaoni gani kuhusu ugonjwa wa ebola ?

Hata hivyo mashirika ya kiraia pamoja na ya kupigania haki za binadamu nchini humo yamekuwa yakiwarai raia kuelewa hali ilivyo na kuachana na mila potofu. Dufina tabu ni mratibu wa shirika la ASVOCO Mjini Goma.

Makundi ya waasi yenye silaha pia yamekuwa yakishambulia mara kwa mara vituo vya tiba vya Ebola na kutatiza huduma za afya na matibabu na kuwauawa madaktari na wauguzi.

Tangu kutangazwa kwa janga la Ebola agosti 2018 hapa nchini, Takimu kutoka wizara ya afya hapa nchini inasema kuwa idadi ya visa vilivyoripotiwa ni 3,313 mkiwemo 3,195 vilivyothibitishwa.

Idadi ni 2,203 huku watu waliotajwa kupona wakiwa 1078.