Jinsi ya kuacha uraibu wa pombe katika sikukuu ya Krismasi

Jade and Melissa
Maelezo ya picha,

Jade na Melissa

"Inawezekana kuwa ni viigumu sana kusema kuwa unapaswa kuwa mtu wa namna fulani wakati wa likizo."

Kwa upande wake Melissa, Sikukuu ya Kristimas huwa ni sherehe kubwa kwake siku zote, usiku wa kuamkia sikukuu hiyo huwa ndio muda anaopenda kwenda kwenye matembezi zaidi.

Melissa anasema kuwa alianza kuwa anatoka usiku wa krismasi kwa ajili ya burudani tangu akiwa na miaka 17 na sasa ana miaka 29.

"Hata siku moja sikuwahi kufikiria kuwa hii ni siku kuu ninahitaji kuwa na familia yangu na wao wanataka kuniona".

Usiku wa krismasi kwangu ilikuwa shangwe juu ya shangwe.

"Ninakunywa sana pombe na kila wakati huo wa mwaka unapofika ni kama ndio muda wake wa kuonyesha uwezo wangu wa kunywa kupinduukia", nilikuwa sijali."

Inawezekana si Melisa peke yake ambaye anayesherekea sikukuu ya krismasi kwa kunywa kupita kiasi na kuona hiyo ndio krismasi imetimia.

Krismasi inapaswa kusheherekewa vipi

"Krismasi ni sherehe inayohusu familia," Melissa alisema, "lakini wakati mwingine huwa ninahisi kuwa sikukuu hii ni ya kula na kunywa, ndio maana napata wakati mgumu mara nyingine".

Kwa sasa Melisa anapata matibabu ya uraibu aliyonayo kuhusu namna ya kusheherekea krismasi.

Jade ambaye ni dada yake Melisa anasema kuwa ilikuwa ngumu kubadili mtazamo wa Melisa kuhusu maana ya krismasi.

"Tunapenda sana siku kuu ya Krismasi" Jude alieleza.

Anasema kuwa Krismasi ni siku ya kipekee kwa kuwa anapokea zawadi na kukaa na familia yake.

Krismasi huwa inamfanya awe mtu mwenye furaha sana .

Huku Melisa kwake anaona hana furaha kama wengine wanavyofurahi.

"Ninafanya kile ambacho kinapaswa kufanywa wakati wa Krismasi kwa sababu ni sikukuu ya Noeli lakini huwa ninajihisi mpweke na ninakosa furaha yangu."

Chanzo cha picha, Melissa Rice

Maelezo ya picha,

Melissa na Jade wanatarajia kusherekea sikukuu ya mwaka huu ya krismasi kuwa ya furaha

Jade anasema wakati anawekea nia ya kupona na uraibu wa pombe, amewekea nia ya kuacha kwenda kutembea na marafiki usiku kwa ajili ya burudani licha ya kuwa ni jambo gumu.

Anasema ameamua kufanya mambo tofauti na marafiki zake ambao ni wanywaji wa pombe kwa muda wa siku kadhaa.

"Inawezekana kuwa jambo zuri kuacha madawa au kunywa pombe?"

Anasema alitumia muda mwingi sana kufurahi na marafiki kwa kunywa pombe kupita kiasi na amebaini kuwa hakuna umuhimu wowote.

"Krismasi ya sasa, ni kuonekana tofauti na kupona," anasema Melissa, "inaweza kuwa nzuri mara 100 zaidi ya sikukuu zote za krismasi zilizopita.

Kila mtu anayenizunguka anategemea makubwa kutoka kwangu."

Na Melissa anasema kutokunywa pombe kutaweza kunisaidia kufurahia sikukuu hii vizuri zaidi bila gharama kubwa na hata kwa upendo zaidi: " Nina mpwa wangu, ninapenda kumuangalia akifungua zawadi yake, awali sikujua hilo ila sasa najua kuna umuhimu.."

Mtaalamu wa masuala ya ijamii anasema, sikukuu hii ya Krismasi ni vyema ni muda mzuri zaidi ikiwa familia zikijumuika pamoja na watu wakiwa hawajanywa pombe na kusheherekea kwa amani na furaha na familia zao.

Mtaalamu wa jamii amesisitiza mambo matatu ya kuzingatia kusheherekea sikukuu hii:

1.Jiandae - Ni vyema kuandaa akili yako kuwa unataka usinywe kilevi na unataka kusheherekea sikukuu hii namna gani?Mahali gani ni salama kwenda.

2. Jumuika na watu ambao wanakujali.

3. Krismasi ni muda wa kujumuika na kufurahi hivyo haikikisha kuwa haujitengi