Jinsi madhila yanavyowasukuma watoto kutaka kujiua

Jinsi madhila yanavyowasukuma watoto kutaka kujiua

Idadi ya watoto wanaojidhuru na kujaribu kujiua inaongezeka katika kambi ya wakimbizi ya Lesbos, nchini Ugiriki, wanasaikolojia wanaofanya kazi katika kituo hicho wanaeleza.

Takribani watu 18,000 wanaishi kwenye kambi hiyo kwa sasa, japo kambi hiyo ilitengenezwa ili kuhudumia watu 2,000 tu. Idadi ya wakimbizi wanaowasili kwenye visiwa vya bahari ya Agea nchini Ugiriki imekuwa ikiongezeka kaatika siku za hivi karibuni, wengi wao zikiwa ni familia zinazokimbia vita.