Makundi ya waasi bado yanahatarisha maisha ya watu wa mashariki mwa Jamuhuri ya Congo

vikosi vya Umoja wa mataifa (MONUSCO)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Vikosi vya Umoja wa mataifa (MONUSCO)

Makundi ya waasi ndani na nje ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya congo, yamekuwa tishio kubwa kwa usalama wa raia katika sehemu za mashariki mwa taifa hilo la afrika ya kati ambalo limekuwa na mizozo ya vita kwa miongo kadhaa.

Jeshi la Congo pamoja na vikosi vya Umoja wa mataifa (MONUSCO) vimekuwa vikifanya juhudi za kupambana na waasi kupitia operesheni za kijeshi dhidi ya wanamgambo wakiwemo wa kundi la ADF na FDLR bila mafanikio hadi sasa.

Mwandishi wa BBC, Byobe Malenga, alituandalia makala ifuatayo.

Uhaba wa usalama umekuwa kilio kikubwa kwa raia wa mashariki mwa DRC kutokana na vita vya mara kwa mara, uporaji wa mali pamoja na mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na makundi ya waasi wa ndani na wa nje ya nchi.

Maeneo yanayo athirika zaidi ni mikoa ya Kivu kaskazini, kivu kusini, mkoa wa ituri na Tanganyika.

Chanzo cha picha, Reuters

"Hali hiyo sio tete tu katika maeneo hayo ya Beni, lakini pia katika maeneo ya Minembwe huko mkoa wa kivu ya kusini ambapo kumekuwa na vita vya mara kwa mara na raia kuuawa,"

Huyu ni mmoja wa raia kutoka mji wa Beni, anaeleza hali anayoishi kwa sasa.

Hata hivyo wanaharakati wa haki za binadamu wanadai kwamba jeshi ndilo lakulaumiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Baadhi ya makundi yanaundwa na raia wa nchi hiyo, lakini kuna makundi mengine makubwa ambayo yanafadhiliwa ama kupambana za serikali za nchi jirani.

Hivi karibuni, makundi makubwa ya waandamanaji yalichoma ofisi za meya wa mji wa Beni na kushambulia vituo vya MONUSCO mjini Beni, Butembo na GOMA katika kueleza kero zao za kutaka vikosi vya umoja wa mataifa Monusco kuondoka nchini DRC.

Ni mwezi mmoja na wiki kadhaa sasa toka jeshi la taifa lianzishe operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya uasi hapa nchini, kwa lengo lakutokomeza makundi hayo, kundi la ADF na FDLR yakiwa mstari wa mbele.

Hata hivyo Jemedari Leo Kasonga msemaji wa jeshi nchini DRC, amewaelezea wanahabari mafanikio na hatua zilizofikiwa za operesheni hizo.

Licha ya serikali kujinadi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa dhidi ya makundi ya waasi, mashirika ya kiraia yanasema kuwa kuna mapungufu na ni lazima jeshi likubali kusaidiwa na vikosi kutoka Monusco ao kutoka mataifa mingine .

Maelezo ya sauti,

Je makundi ya waasi wa DRC yanaweza kumalizwa?

Hivi karibuni shirika la Cepadho lilichapisha ripoti inayoelezea mauaji ya watu 150 katika kipindi cha wiki 5.

Hali hiyo inajiri wakati kukishuhudiwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Ebola katika mikoa ya Ituri na kivu kaskazini - ugonjwa uliochangia vifo vya zaidi ya watu 2200.

Hali hivyo imekuwa ikiwapa wasiwasi watu wengi na baadhi wanahofia kuwa huenda hali ikiwa mbaya zaidi iwapo serekali pamoja na jumuia ya ukanda wa maziwa makuu, hazitachukua hatua za haraka.