Changamoto za kiafya zilivyojeruhi taifa la DRC

Ebola
Maelezo ya picha,

Mtoto akipatiwa chanjo DRC

Mwaka 2019 umekuwa mwaka wa changamoto kubwa za kiafya kwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Nchi hiyo ilikabiliwa na janga la Ebola na pia Surua au Ukambi.

Mwandishi wa BBC, Mbelechi Msochi kutoka DRC amekua akifatilia kwa kina Janga hili.

Akianza kuangazia janga la ebola ambalo linazungumziwa zaidi na vyombo vya habari licha ya kwamba surua ndio ugonjwa uliosababisha maafa zaidi nchini.

Katika juhudi za kupambana na janga hilo, Kongo ilipata chanjo kwa mara ya kwanza dhidi virusi hivyo ambavyo tangu mwaka 2008, umesababisha vifo vya zaidi ya raia 2000 huko mashariki mwa Kongo.

Kwa mujibu wa Jean Jacques Muyembe, mratibu wa serikali husika na na kupambana na ebola, utafiti huu ulianzishwa mwaka 2008, mwezi wa Novemba kwa ushirikiano na shule ya umma nchini Marekani.

Ugunduzi huu ulipokelewa kwa shangwe kwa baadhi ya mashirika yanayochangia katika juhudi za kupambana na ebola.

Viongozi wa nchi za maziwa makuu zilizopakana na maeneo ya mashariki mwa Kongo waliingia na wasiwasi, lakini hatua za tahadhari zikaidhinishwa katika eneo hilo.

Mfano katika nchi jirani inayopakana na Kongo - Rwanda hivi karibuni imeanza kutoa chanjo kwa raia wake wanaovuka mpaka na kuingia DRC haswa katika eneo la kivu kaskazini ambapo virusi vya ugonjwa huo .

Tanzania, Uganda na Kenya ni mifano ya mataifa jirani ambayo pia yalizindua mpango wa ukaguzi wa Ebola katika maeneo ya mipakani.

Mpango huo uliidhinishwa kuwasaidia maafisa kusambaza kwa haraka taarifa kuhusu iwapo kumegunduliwa visa vyovyote vya Ebola.

Lakini ndani ya Congo kwenyewe pia wapinzani walianza kuchangia katika uhamasishaji kwa raia kuhusu hatari ya ebola.

Martin fayulu mpinzani mkuu wa rais felix tshikedi, alizundua mradi wake wa kutoa uhamasishaji kwa wafuasi wake kuhusu hatari ya ebola.

Maelezo ya picha,

Mgonjwa wa Ebola na wauguzi

Lakini mbali na janga la ebola, zaidi ya watoto elfu tano walifariki mwaka huu 2019 kutokana na janga la surua ambalo lilienea nchini DRC.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa huo ndio janga linalosambaa kwa kasi mno.

Ugonjwa huo wa surua nchini DR Congo umekua idadi iliyo mara mbili ya wagonjwa waliofariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika kipindi cha miezi 15 iliopita.

Serikali ya Kongo ilikabiliwa na changamoto za kifedha pia na vifaa vya kusafirisha chanjo katika majimbo tofauti.

Serikali ya DRC kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO imezindua chanjo ya dharura mwezi Septemba inayowalenga watoto 800,000.

Kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba, watoto milioni 4 tayari wamepewa chanjo, lakini wataalam wameonya kwamba idadi hiyo ni chini ya nusu ya jumla ya watoto nchini humo na kwamba chanjo zilizopo hazitoshi.

Maelezo ya picha,

Wasaidizi wa Afya wakiwa wamejinga kwa ugonjwa wa Ebola

Wengi ya wale walioathirika na ugonjwa huo ni watoto wachanga.

Inakadiriwa kwamba jumla ya watu 110,000 duniani hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.