Tetesi za soka Ulaya Jumapili 29.12.2019:Eriksen, Pogba, Richarlison, Moyes, Giroud

Christian Eriksen alijiunga Tottenham mwaka 2013 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Eriksen alijiunga Tottenham mwaka 2013

Klabu ya Manchester United wanasubiri hadi mwisho wa msimu ili wamsaini kiungo wa Tottenham na Denmark, Christian Eriksen, 27, akiwa mchezaji huru hii ni kwa mujibu wa Sunday Telegraph.

Nae Carlo Ancelotti huenda akazuia jaribio la Manchester United la kutaka kumsajili mchambuliaji kutoka Brazil Richarlison, 22, hata kama Mashetani hao watatoa pauni milion 70.

Real Madrid imemwambia Zinedine Zidane asahau kuhusu kumchukua Paul Pogba, 26, kutoka Manchester United kwa sababu kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kama atasajiliwa atamnyima nafasi kiungo anae kuja kwa kasi kutoka Uruguay Federico Valverde,

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji mwenye ndoto, Alexander-Arnold, 21

Beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 21, anasema kuwa anataka kubaki katika klabu ya Liverpool kwa muda wake wote kama mcheza soka, ili awe mkongwe katika klabu hiyo.

Kwa upande mwingine David Moyes na Tony Pulis ndio wanatajwa kuongoza kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrin baada ya kufungishiwa virago vyake na Wagonga Nyundo wa London West Ham United

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexander-Arnold, 21

Bosi wa Juventus Maurizio Sarri anatamani sana kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud, 33, kutoka klabu yake ya zamani ya Chelsea.

Barcelona inasema malalamiko ya kisheria ya Arturo Vidal dhidi ya klabu, juu ya madai ya kulipwa fidia ni jaribio la kiungo huyo wa Chile, 32, kulazimisha kutimkia Serie A katika klabu ya Inter Milan Januari.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa Nigeria, Victor Osimhen, 20

Liverpool wameonesha nia yao ya kumtaka kiungo Lille na Victor Osimhen kiuongo wa Nigeria, 20.

Fiorentina anahitaji sana kumsajili beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29, msimu ujao wa majira ya joto. (La Nazione, Football Italia)

Beki wa Southampton na Denmark Jannik Vestergaard, 27, anatarajiwa kusajiliwa na klabu yake ya zamani Werder Bremen mwezi January. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa zamani wa Barcelona Andres Iniesta, 35

Kiungo wa zamani wa Barcelona Andres Iniesta, 35, amekataa ofa kutoka ligi ya Marekani kutoka katika klabu za LA Galaxy, Miami na Montreal Sounders nakubakia kwenye timu ya Japan Vissel Kobe.. (Sky Sports)

Nae Carlo Ancelotti huenda akazuia jaribio la Manchester United lakutaka kumsaini mchambuliaji kutoka Brazil Richarlison, 22, hata kama Mashetani hao watatoa pauni milion 70.

Image caption Cristiano Ronaldo

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo anasema kuwa anataka kujaribu kuwa muigizaji mara baada ya kustaafu soka.

kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amependekeza klabu hiyo kumrudisha beki wa timu hiyo na Uingereza Nat Phillips, 22, ambaye yupo kwa mkopo Ujerumani Stuttgart kwa muda.

Swansea wanataka kumsaini kiungo wa Bristol City mwenye umri wa miaka 23 Kasey Palmer kwa mkopo mnamo Januari.

Nao Bayern Munich, Juventus na Paris St-Germain waonyesha nia ya kumsaini kipa wa Ujerumani, Marc-Andre Ter Stegen, 27, kutoka klabu ya Barcelona.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii