China kuchunguza virusi vinavyosababisha mlipuko wa ugonjwa wa ajabu

Mji wa Wuhan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlipuko wa ugonjwa wa ajabu umetokea mji wa Wuhan

Mamlaka ya China imeanzisha utafiti kuchunguza virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ajabu ambao umewaambukiza watu kadhaa katika mji wa Wuhan.

Kesi za watu 44 zimeripotiwa na kuthibitishwa mpaka sasa, visa 11 kati yake vinatajwa kuwa hatari zaidi, maofisa wamesema .

Mlipuko wa ugonjwa huo umefanya mji wa Singapore na Hong Kong kuanza kuchunguza watu wanaosafiri kutoka mji huyo.

Ugonjwa huu umezua hofu mtandaoni na kuhusisha virusi hivyo kuwa unaweza kupelekea kuwa na mtindio wa ubongo na madhara mengine yanayoweza sababisha vifo.

Uwezekano wa ugonjwa huo kufanana na ugonjwa wa 'sars' ambo uliua watu zaidi ya 700 ulimwenguni kote mnamo 2002-03, baada ya kutokea nchini China.

Kumekuwa na uvumi kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha ugonjwa huu kuwa unaambukiza kwa kasi sana.

Polisi wa Wuhan police amesema kuwa watu wanane wameadhibiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao bila ya kuwa na uhakika kuhusu ugonjwa huo.

Tume ya afya ya Wuhan imesema kuwa inafanya uchunguzi wa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Hotuba yake katika mtandao umesema kuwa tayari imeangazia vyanzo vya maambukizi ya ugonjwa huo na dalili za ugonjwa huo lakini hotuba hiyo haikutaja kuwa unafanana na ugonjwa wa 'Sars' ambao uliwahi kusambaa duniani kote na kuua watu huku ukiwa umeanzia China.

Vilevile hakutaja kuwa kuna maambukizi ya kati ya binadamu na mwanadamu.

Licha ya kuhusisha maambukizi hayo na soko la samaki, jambo ambalo lilipelekea mamlaka kutaka kufanya usafi katika maeneo hayo.

Msemaji kutoka shirika la afya duniani (WHO) amesema kuwa wana taarifa kuhusu ugonjwa huo na walikuwa wanawasiliana kwa karibu na serikali ya China.

"Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea maambukizi ya virusi hivyo, na sababu nyingine zinahusishwa na mambo yanayofahamika kusababisha dalili za ugonjwa ," msemaji huyo aliongeza kuwa. "WHO inaangalia kwa karibu mlipuko huo na itaweza kutoa taarifa zaidi watakapozipata. "

Hofu ya kutokea kwa ugonjwa wa zamani

Mlipuko wa ugonjwa huu wa ajabu umewafanya watu kukumbuka ugonjwa wa ajabu wa kuambukiza ambao ulitokea miaka 18 iliyopita.

Kwa sasa , shirika la afya limeikosoa China kwa kutoa taarifa ya visa vichache vya wagonjwa walioambukizwa na ugonjwa wa Sars ambao ulitokea jimbo la kusini.

Ugonjwa huo uliozuka mwaka 2002-03 virusi vyake vilisababisha vifo vya watu zaidi ya 8,000 katika mataifa 26 na kuua watu 349 China na wengine 299 huko Hong Kong.

Wasafiri pia wanadhaniwa waliambukizwa kwa kiwango kikubwa kwa sababu ugonjwa huo ulikuwa unasambaa kwa kasi sana kabla ya mtu kupata tiba hospitalini.

China ilimfukuza waziri wake wa afya wakati huo kwa kushindwa kukabiliana na janga la ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Sars ulitokomezwa tangu Mei 2004.