Msemo wa 'usiache mbachao kwa msala upitao' una maana gani katika vyombo vya bahari

Urithi Wetu—UDSM Haki miliki ya picha Urithi Wetu—UDSM

Ngalawa inatajwa kuwa ni chombo imara zaidi baharini kinachotengenezwa na wazawa tangu karne ya 17 na 18 .

Wataalamu wa enzi na enzi wanaamini kuwa Ngalawa itaendelea kuepo karne na karne licha ya vijana wa sasa kutopendelea taaluma hiyo.

Tafiti zimeweka makadirio ya karibu ya kupotea kwa chombo hicho. Lakini katika kuhakikisha utamaduni huo unaendelea, chuo kikuu cha Dar es salaam, kimeanzisha mradi 'Urithi wetu' ili kuwawezesha wazee kuwafundisha vijana utalaam huo.

Ukizungumzia vyombo vya asili vya usafirishaji wa bahari huwezi kuacha kuzungumzia Ngalawa, mtaalamu wa chombo hiki mzee Juma Hamada anasema kuwa anapenda kazi yake na anaifanya kwa ufanisi.

Anasema kuwa si Ngalawa peke yake ambazo wanatengeneza, wanatengeneza pia Jahazi, Mashua, mitumbwi, Dau na vyombo vingine vingi.

Yeye anasema kuwa vyombo hivyo bado vina nafasi kubwa kwa sababu ya hali ya maisha ni ngumu, watu wengi ni maskini hata kama kuna boti za mashine lakini lazima tanga iwepo.

"Hata kama kuna teknolojia mpya imekuja lakini hatuwezi kutupa vyombo vyetu vya zamani, hii ni sawa na kusema huyu mama wa zamani nimtupe au baba wa zamani nimtupe, sisi waswahili tunasema

Usiache mbachao kwa mstari upitao"

Huwezi kusikiliza tena
Utamaduni wa uchongaji Ngalawa umekuwa ukienziwa sana mjini Bagamoyo

Mzee Hamada anasema Ngalawa ni chombo cha kwanza kusafiri kutoka Bagamoyo mpaka Zanzibar na ikumbukwe kuwa kuna maskini na matajiri.

Ameongeza kusema kuwa Ngalawa ni chombo cha awali kabisa, hivyo ni utamaduni ambao hawawezi kuuacha na katika kuhakikisha hilo wameanza kuwafundisha vijana namna ya kutengeneza chombo hicho.

Chama chao wanakiita chama boma.

Hata mtu ukisema vyombo vyao ni hatari lakini ikumbukwe kuwa "hatari huwa inafika kwa kuandikwa, watu wanakufa hata kwenye ndege, hata ikiwa meli au ngalawa.

Miaka mingapi umesikia ngalawa imezama na watu wamefariki?"

Alisisitiza kusema kuwa kufa ni kufa kule kule, siku hizi wana makoti ya kujiokolea na vyombo vya uokozi lakini anaona kuwa hakuna tofauti kati ya vyombo vya zamani vya sasa.

Image caption Mradi wa Urithi wetu

"Sisi tuna uwezo wa kutengeneza hata meli ya mbao.

Kulikuwa na chuo cha kufundisha kuchonga maboti lakini kimekufa, tumeona ufundi utapotea ndio maana tukaamua kuwakusanya vijana na kutengeneza vyombo hivi."

Jitihada za kutunza utamaduni wa Ngalawa

Image caption Ngalawa, chuo kikuu cha Dar es Salaam

Dr. Elgidius Ichumbaki ni mtaalam wa masuala ya kale kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, anasema kuwa wameanzisha mradi huu wa kuendeleza vyombo vya asili kwa kuwaendeleza vijana wadogo wajifunze na kuweza kunusuru historia hii.

"Tumekuwa na mradi wa 'Bahari yetu urithi wetu' unaofadhiliwa na serikali ya Uingereza ili kuwawezesha wazee wa zamani kuwafundisha vijana.

Tunataka vyombo wanavyovitengeneza kuwa zalishi, watengeneze vifaa hivyo na kutumika kusafirishia wageni katika utalii wa baharini.

Ngalawa ni mti mmoja mkubwa ambao unachongwa na kuweza kutembea lakini, miti hii inaanza kupotea.

Kuna namna mbili ya kupotea kwa Ngalawa , moja ni miti wanayotumia kutengeneza Ngalawa kunaweza kupotea na pili ni ujuzi nao unaweza kutengeneza vyombo hivyo vya asili kupotea.

Tunategemea kuwa baada ya miaka 10 chombo hiki kinaweza kupotea, lakini sababu kuu ni miti kupotea na ujuzi na upatikanaji wa vyombo vya kisasa.

Kwa nini Ngalawa ni muhimu?

Chombo kama Ngalawa kina uwezo wa kipekee kwa sababu kinaweza kutumika katika maji marefu bila kuzama, hata ikipigwa na wimbi Ngalawa huwa haizami kwenda chini.

Unaweza kukaa hata siku mbili baharini ndani ya Ngalawa hata kama imeingia maji.

Kuna wavuvi wengi wanatumia Ngalawa, si kwamba vyombo havipati shida lakini ni mara chache sana utasikia Ngalawa imepinduka.

Image caption Razaki Changezi anajifunza kutengeneza ngalawa

Razaki Changezi mwenye umri wa miaka 24, anasema kazi hii ya kutengeneza Ngalawa ni kipaji, yeye ana miaka minne anajifunza kutengeneza vyombo vya asili vya bahari.

Licha ya kuwa yeye ana aledge(uzio) wa bahari, lakini anapenda kutengeneza vyombo vyake.

Anasema kuwa bahari huwa ina ulevi mkubwa sana, si jambo rahisi kutumia vyombo vya bahari.

Lakini vilevile Razaki anasema kuwa vijana wengi wanakuwa wagumu kujiunga na fani hiyo kwa sababu, vijana wanapenda kujifunza vitu kwa haraka haraka .

"Sisi vijana tuna ueleo wa harakaharaka, tunaiogopa kazi hii kwa sababu ina mlolongo mrefu na vitendea kazi havijaboreshwa".

Ngalawa imekuwa ikitumika kama meza katika migahawa

Miaka ya hivi karibuni, Ngalawa imepata umaarufu mkubwa kutengenezwa kama meza katika sehemu za burudani.

Yawezekana kizazi kijacho baada ya miaka 10 wataifahamu Ngalawa kama aina ya meza tu lakini sio chombo cha kusafiria na inawezekana hata sasa kuna kizazi ambacho hakifahamu uwepo wa chombo cha aina hiyo.

Haki miliki ya picha SAMAKI SAMAKI INSTAGRAM
Huwezi kusikiliza tena
Katika kisiwa cha Kilwa kuna wakati ilikuwa dola inayojitawala na kusifika kwa utajiri

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii