Ukweli kuhusu chanjo ya HPV na dhana potovu?

HPV vaccine

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Maelezo ya picha,

Wasichana na wavulana wote wanapaswa kupata kinga hiyo

Je, kuna maana gani kwa watu kuchoma chanjo ya HPV.

Chanjo ya HPV inazuia maambukizi ya virusi ambavyo husababisha saratani ya shingo ya kizazi.

Baadhi ya watu wanaposikia kuhusu chanjo ya HPV huwa tunahusisha na maambukizi ya ngono au mtu kuwa mchafu.

Utafiti unaonyesha kuwa wanawake ndio wanapewa chanjo hii zaidi kuliko wanaume.

Virusi hivi vinaishi kwenye ngozi pembezoni mwa uke na mtu unaweza kupata maambukizi kwa njia ya ngono na hata kama ukitumia kondomu, unaweza kupata magonjwa ya zinaa.

Ingawa mtaalamu kutoka taasisi ya Trust nchini Uingereza, bi. Kate Sanger,anabainisha kuwa anafafanua kuhusu chanjo hiyo, na kusema maambukizi yake unaweza kuyanafananisha zaidi na homa ya kawaida kuliko magonjwa mengine ya zinaa, hivyo hatupaswi kuwa na hisia hizo juu ya chanjo hiyo.

Vilevile ubaguzi ambao upo unawaadhiri wanawake zaidi na hali hiii inaweza kufanya maamubukizi kukua zaidi.

Lakini nani yuko hatarini kupata maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi.

Kama ni wote, wanawake kwa wanaume, kwa nini wanawake wanasisitizwa zaidi kufanya vipimo zaidi ya wanaume

"Niliambiwa kuwa kama umeenda kuchomwa chanjo ya HPV basi wewe ulikuwa mchafu, kuchoma chanjo ya HPV haina maana kuwa una shida yeyote. haimaanishi kuwa uko tofauti na watu wengine," alisema.

"Ni sawa na kupata mafua bila ya kuwa na dalili zozote ."

Chanzo cha picha, Jo's Cervical Cancer Trust

Maelezo ya picha,

Watu wanapaswa kuhamasishwa kufanya vipimo vya HPV

Nicole Davidson, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Suffolk, alisema kuwa alifanya vipimo vya shingo ya uzazi kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Sasa hivi ana watoto wawili na aliamua lakini anapata matibabu ya virusi vya shingo ya uzazi.

Alipobaini kuwa ugonjwa aliokuwa nao ulitokana na saratani ya shingo ya uzazi, alipata msongo wa mawazo zaidi.

Amekuwa na mpenzi wake kwa kipindi cha miaka mitano na hakuwahi kuulizwa kuhusu historia yake ya kingono, hali hiyo ilimfanya ajisikie vibaya.

"Nilihisi kuwa nimejisababishia kupata ugonjwa huo mwenyewe. kama nisingefanya ngono basi nisingepata saratani ya shingo ya uzazi," alisema.

Wanawake na wanaume, wote kwa pamoja wanaweza kupata maambukizi ya HPV, ingawa wanaume wengi hawafahamu hili kwa sababu hawafanyi vipimo.

Zaidi ya asilimia 40 ya wanawake waliambiwa kuwa kuwa na maambukizi ya saratani ya shingo ya uzazi inaweza kusababisha madhara katika mahusiano yao ya kimapenzi, haswa walilengwa wanawake wenye umri mdogo zaidi.

Na asilimia 22 walisema kuwa watakwa na mahusiano na wenza ambao wana HPV kama wao na nusu yake waliamua kuvunja mahusiano na wenza wao .

Mpango wa chanjo ya HPV kwa wasichana ni jambo jipya hata kwa wazazi, kwa sababu baadhi ya wazazi huwa wanahoji kama haupewa chanjo hiyo kwa nini ampe mtoto wake.

Hii inaonyesha wazi kuwa elimu zaidi kuhusu chanjo hii inahitajika katika jamii kwa sababu maambukizi haya yanaweza kutokea tu, si lazima ufanye kitu fulani ndio upate.

Kwanini chanjo ya HPV ni muhimu?

Saratani ya shingo ya uzazi huwaathiri zaidi ya wanawake nusu milioni kila mwaka na husababisha vifo vya wanawake laki mbili na nusu kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Ni mojawapo ya saratani inayowashika wengi hii leo lakini pia ni mojawapo ya saratani inayoweza kuzuilika.

Chanjo dhidi ya HPV hulinda usalama dhidi ya maambukizi yanayohusishwa kwa karibu na saratani hiyo, na ukaguzi wa mapema husaidia kutambua seli kabla hazijageuka saratani.

Dhana potovu kuhusu virusi vya HPV

Chanzo cha picha, Getty Images

Dhana: Unaweza kupata virusi vya HPV kwa njia ya kujamiiana pekee

Ukweli: HPV sana sana huenezwa kwa njia ya kujamiana lakini pia mtu anaweza kupata virusi hivyo kugusana kimwili hasa maeneo ya utupu na mtu aliye navyo.

Dhana: HPV ni inaashiria mtu ni mzinifu

Ukweli: 80% ya watu watapatikana na virusi vya HPV wakati mmoja katika maisha yao, ni rahisi kupata virusi hivyo na kuvisambaza kwa mto wa kwanza utakayefanya mapenzi nae

Dhana: HPV inamaanisha niko na maradhi ya saratani

Ukweli: Kuna karibu aina 200 ya HPV. Karibu aina 40 ya virusi hivyo huathiri maeneo ya utupu, hii inamaananisha virusi hivyo vitaishi maeneo hayo ya mwili na baadhi ya virusi hivyo huenda vikasababisha magonjwa ya zinaa. Karibu aina 13 ya virusi hivyo huenda vikasababisa saratani ya shingo ya uzazi na aina nyingine ya saratani kama vile ya mdomo au koo lakini visa hivyo ni vichache.

Dhana: Utajua ikiwa una virusi vya HPV

Ukweli: HPV haina dalili zozote na wakati mwingine mfumo wa kinga ya mwili huweza kukabiliana na maambukizi. uchunguzi wa shingo ya uzazi unaweza kubaini seli zozote tumbo