Coronavirus: Wachina washauriwa kuzingatia usafi

Msafishaji mjini Wuhan Haki miliki ya picha Getty Images

Picha ya mtu aliyefunga kitambaa cha kuziba pua na mdomo ''mask'' ili kujizuia kupata virusi ni sehemu ya kinga dhidi ya maambuki ya ugonjwa.

Kitambaa hicho cha kuziba mdomo ambacho ni maarufu katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya kujizuia maambukizi, sasa kinatumika sana China baada ya mlipuko wa virusi vya corona ambapo watu wamepewa ushauri wa kuejiepusha na mahali palipo na msongamano wa watu.

Wataalamu wa afya wameelezea namna 'mask' hizo zinavyoweza kufanya kazi ili kuzuia virusi.

Kuna baadhi ya ushahidi ambao unadhania kuwa mask hizo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi kati ya mtu na mtu.

Mask ilianza kutumika kwa mara ya kwanza katika hospitali mwishoni mwa karne ya 18, lakini zilikuwa hazitumiki katika sehemu za umma mpaka mlipuko wa mafua ulipotokea Uhispania mwaka 1919 na kuuwa watu zaidi ya milioni 50.

Dkt David Carrington, wa chuo kikuu cha St George, mjini London, aliiambia BBC kuwa "'mask zinazotumika wakati wa operesheni au upasuaji huwa haziwezi kufanya kazi vizuri katika maeneo ya umma kuzuia watu kupata maambukizi ya virusi vya bakteria wa hewa ambao wanaambukiza, kwa sababu zina nafasi za wazi na zinaacha macho wazi.

Lakini zinaweza kupunguza maambukizi kwa kiasi fulani ya kuwakinga watu katika maambukizi ya mkono na mdomo.

Utafiti uliofanywa kutoka New south Wales ulipendekeza kuwa watu huwa wanashika nyuso zao mara 23 kwa saa.

Haki miliki ya picha Getty Images

Jonathan Ball, profesa wa 'molecular virology' katika chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa : "Katika tafiti moja ambayo ilifanywa hospitalini, inaonyeshha kuwa mask ya sura huwa nzuri kwa kuzuia maambukizi kama ilivyobuniwa.

Wabunifu waliotengeneza mask hiyo waliitengeneza kwa namna ambayo inaweza kuzuia vimelea vya hewani.

Ingawa , ukiangalia ufanisi wake kwa ujumla katika msongamano wa watu, takwimu zinaonyesha utofauti mdogo - Vilevile si rahisi kwa mtu kukaa na mask kwa muda mrefu ," Prof Ball aliongeza.

Dkt Connor Bamford, wa taasisi ya afya ya Wellcome-Wolfson, iliyopo chuo kikuu cha Queen Belfast, alisema kuwa "utekelezaji wa kuweka mazingira safi ndio hatua rahisi zaidi ambayo inaweza kufanya kazi kwa uhakika".

Huwezi kusikiliza tena
Uchina yathibitisha virusi vya corona vinaweza kusambazwa

"Kuziba mdomo wakati unapiga chafya, kunawa mikono, na kujizuia kuziba midomo kwa mikono kabla ya kunawa, kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi kupata virusi", alisema.

Watu wanapaswa kuzingatia:

  • Kuosha mikono mara kwa mara na maji yaliyochemshwa na sabuni
  • Kuepuka kushika macho na pua kadri uwezavyo
  • Kufanya mazoezi na kula chakula bora

Dkt Jake Dunning, mkuu wa masuala ya afya nchini Uingereza alisema kuwa: "Ingawa kuna watu ambao wanahisi kuvaa mask usoni kutasaidia watu kupata maambukizi, kuna ushahidi mdogo sana kuwa kitendea kazi hicho kinaweza kuwanufaisha watu wakiwa nje kwa sababu imebuniwa kwa ajili ya kufanya kazi kwenye huduma za afya.

Alisema pia mask hizo hazijavaliwa vizuri, kubadilishwa kila wakati kunaweza kuwa salama haa katika mazingira ya kazi.

"Utafiti unaonyesha kuwa mask hiyo ilivaliwa kwa muda mrefu huwa inapongeza nguvu ya ufanyaji kazi wake, alisema.

Watu wangezingatia zaidi kufanya mazingira yao kuwa safi, kama hilo suala la usafi wangelipa kipaumbele, alisema Dkt. Dunning.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii