Je,Sultan Qaboos alikuwa kiongozi wa Zanzibar pia?
Huwezi kusikiliza tena

Chanzo cha undugu wa Oman na Zanzibar

Kifo cha Sultani wa Omani Qaboos kimegusa hisia za wengi ulimwenguni, lakini nje ya Oman eneo jingine ambalo kifo hicho kimewagusa wengi ni kisiwa cha Zanzibar kilichopo katika bahari ya Hindi.

Wazanzibari wengi wameomboleza kifo chake katika hali ya kuonyesha kuwa alikua kama kiongozi wao.

Waliandaa dua katikakati mwa Zanzibar Stone Town na kutuma salam zao za rambirambi katika mitandao ya kijamii.

Waoman wengi na Wanzanibari wameungana kwa njia mbalimbali ikiwemo kuoana kutokana pia na historia pana ya nchi hizo mbili kuanzia miaka ya 1600

Mada zinazohusiana