Samatta ajenga ari ya wengi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Mbwana Samatta: Mamia wajitokeza Mbagala kuangalia mechi ya Aston Villa vs Leicester

Mechi kati ya Aston Villa na Leicester city ilikuwa na mvuto wa aina yake nchini Tanzania hapo jana usiku.

Baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samata kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Aston Villa.

Mbwana Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya Ulaya. Huko mtaani alikokulia Samatta, watu walikusanyika katika uwanja wa mpira ili kufuatilia mechi hiyo kwa pamoja.

Hamu kubwa, matarajio na macho ya wengi hapa ni kwa nyota wao Mbwana Ali Samatta

Wananchi hawa wametoka mitaa mbalimbali ya eneo la Mbagala mjini Dar es Salaam kuja kuonyesha mapenzi yao makubwa kwa Sammata.

Samatta alianzia kucheza soka katika kiwanja hiki wakati anasoma shule ya jirani hapa hadi alipofikia kucheza soka ya kulipwa.

Tangu Mbwana Sammata asajiliwe na Aston Villa na kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England, timu imejipatia umaarufu na kuongeza washabiki nchini Tanzania, kupitia Mbwana Samatta ambaye ameleta matumaini mapya kwa watanzania na mashabiki wa soka Afrika Mashariki.

Hii ni mechi ya kwanza Samata kucheza baada ya kusajiliwa na Aston Villa.

Ingawa Samatta hakubahatika kufunga magoli katika mchezo huu lakini kwa hapa Mbagala na Tanzania kwa ujumla, Samata anasalia kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengi wenye malengo yakufanikiwa katika mpira wa miguu.