'Unapozuiliwa kyohwaso [gereza] unakuwa sio binadamu tena'

'Unapozuiliwa kyohwaso [gereza] unakuwa sio binadamu tena'

"Nilipoteza matumaini… Niliwaza kujitoa uhai mara nyingi sana.Nililia na kulia sana ," alisema.

"Unapozuiliwa kyohwaso [gereza] unanyimwa uraia wako," anasema Jeon. "Unakuwa sio binadamu tena. Huna tofauti mnyama." Siku moja alimnong'onezea Kim maneno ambayo yangelibadilisha maisha yao daima .

"Nataka kukusaidia dadangu. Huenda ukafariki gerezani. Njia pekee ninayoweza kukusaidia ni kukutoa hapa," alisema. Lakini raia wengi wa Korea Kaskazini, kama Kim wamezoea kutoaminiana. Alidhani huenda ni njama.

"Kwa hiyo nilimkaripia, kwa kusema: 'Wewe ni Jasusi?' Unapata nini kunichunguza na kutaka kuniharibia maisha?' Lakini alisisitiza kuwa yeye sio jasusi."Hatimaye Jeon alimhakikishia kuwa hataki kumsaidia yeye pekee kutorokea Korea Kaskazini bali yeye pia anataka kuandamana naye.