Coronavirus: Wazazi wanapaswa kuwaambia ukweli watoto wao

Mtoto akipiga chafya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mlipuko mkubwa kama wa corona unaweza kuwafanya watoto kuwa na hofu zaidi

Kila siku kuna ripoti mpya kuhusu mlipiko wa virusi vya corona vinavyosambaa kwa kasi duniani kote.

Hofu inazidi kutanda kwa watu wengi kuhusu hatari za ugonjwa huu, watoto wakiwa miongoni mwa watu hao ambao kila kukicha wanaomba ushauri kwa wazazi wao wakiwa na maswali mengi.

Je, ni namna gani unaweza kuongea na watoto kuhusu mlipuko huu wakati wanaposema wana hofu na kuogopa ?

Waondoe hofu

Dkt Punam Krishan, ambaye ni daktari wa familia nchini Uingereza mwenye mtoto wa miaka sita, anasema ni muhimu kumuondoa hofu na kumuelea kuwa hali hiyo ni sawa na mtu anapopata mafua au kipindupindu na kutapika.

Anaamini kuwa wazazi wanapaswa kuwa wawazi, kuwaeleza ukweli kuhusu jambo hili badala ya kuwaficha, na yeye anafanya hivyo kwa mwanae.

Dkt Richard Woolfson, ni mwanasaikolojia wa watot anaamini kuwa kuongea na watoto kuhusu suala kubwa kama la mlipuko wa corona huwa inategemea na umri wa mtoto.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ni muhimu kuwaondoa hofu watoto

"Watoto wadogo, kuanzia miaka saba na kushuka chini wanaweza kuwa wanasikia kila kitu lakini wasielewe ni nini ambacho kinaendelea.

Hali hii inaweza kuwatisha sana watoto."

Watoto wadogo ni muhimu kuwapa uhakika wa kile kinachoendelea na kuwaambia kuwa kila kitu kitaenda kuwa sawa.

Baadhi ya watu wataathirika na janga hili lakini tutakuwa sawa tu.

Hatua za kufuata

Wakati Dkt Woolfson alipokiri kuwa bora kuwaambia ukweli ingawa ni vyema kutowafanya wawe na hofu zaidi.

Unapaswa kuwapa ujasiri kuwa kila kitu kitakuwa sawa na hakuna haja ya kuwa na hofu.

Ni muhimu kuwafundisha namna ya kujikinga na maambukizi na kuwafanya wahisi kuwa wanaweza kujilinda katika hali hii.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kuwafundisha watoto jinsi ya kujilinda kwa usafi na faida zake

Alisema ni muhimu kuwaambia watoto wadogo kuwa kuna vitu ambavyo vinaweza kulinda afya zao na wanachopaswa kufanya ni kuosha mikono na mambo mengine ya usafi.

Dkt Krishan anakubali kuwa kuzungumza na watoto jinsi ya kujikinga na maambukizi ni jambo muhimu ili wajilinde wenyewe.

Ni vyema wajifunze kujilinda wenyewe kwa kujua hatua muhimu za kuzichukua badala ya kuwaficha au kuwashtua.

Kuwapa uhakika kuwa kila kitu kitaenda kuwa sawa na kuwafundisha mikakati ya kujikinga wao na familia kwa ujumla.

Kujikinga

Pamoja na kuwakumbusha watoto kuwa ni muhimu kuzingatia usafi ni suala ambalo linaweza kuondoa hofu, lakini watoto kwa kawaida tu wanapenda kushika vitu na kula vitu kwa pamoja na kunywa pamoja kwa kuchangia, mfano kinywaji kimoja wanaweza kunywa katika birauli moja watoto watatu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kuchangia chakula kwa watoto kunaweza kusababisha maambukizi

Kuchangia kwao kwa chakula kunaweza kusambaza maambukizi hivyo ni muhimu kufundishwa kuacha tabia hiyo.

Kuwafundisha usafi watoto kutasaidia kulinda jamii nzima.

Taarifa ghushi

Kuna taarifa ghushi au feki ambazo zinaweza kuwapa hofu zaidi watoto.

Lakini mzazi ana ushawishi mkubwa zaidi kwa mtoto mdogo pale anapozungumza naye, hivyo ni muhimu mtoto na mzazi kuzungumza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

watoto wanaweza kupata taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii au marafiki

Wazazi wanaweza kuwalinda watoto wao wakiwa nyumbani lakini wakiwa shuleni huwa ni ngumu.

Kutakuwa na simulizi nyingi za uongo zinazoendelea kusambaa kuhusu mlipuko huu hivyo ni muhimu kumpa uhakikishia mtoto wako ukweli wa kile ambacho kinaendelea.

Vijana

Vijana huwa wanapata taarifa kutoka maeneo mbalimbali na hawategemei sana kuelezwa na wazazi wao.

Huwa wana namna yao ya kupata taarifa kutoka kwa marafiki, na huwa ni ngumu kumueleza kijana wa miaka 14 kuwa kila kitu kiko sawa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Vijana huwa hawategemei sana kupata taarifa kutoka kwa wazazi

Mtoto mwenye umri mkubwa kidogo anaweza kukubishia, na kutokubaliana na kile ambacho unawaambia.

Ingawa ni muhimu kuwaeleza haijalishi wako umri gani?