Uchaguzi wa Tanzania 2020: Wapinzani wakutana faragha na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam

Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumaliza mazungumzo

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Maelezo ya picha,

Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amekutana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.

Magufuli amekutana na mwanasiasa mkongwe na mwanachama wa ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia na mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya mazungumzo nao.

Viongozi hao wa upinzani walikutana kwa nyakati tofauti na rais Magufuli.

Kupitia Ukurasa wa Instagram, Ikulu ya Tanzania imetoa kipande cha mahojiano na Maalim Seif ambaye hakueleza kwa kina kilichozungumzwa baina yao, akisema kuwa yaliyozungumzwa hawezi kuyaweka hadharani.

"Mimi na mheshimiwa rais tumekutana na kubwa ni kuzungumzia mambo ya nchi yetu, vipi tutaendelea kuifanya Tanzania kuwa nchi ya amani, nchi ya salama, nchi ya upendo kwa watanzania wote," amesema Maalim Seif na kuongeza "Sasa kuna mengine tumezungumza mimi na rais, yamo ndani na huwezi kuyaweka hadharani, ikitokea haja ya kukutana tena tutakutana."

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Maelezo ya picha,

Rais Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia

Lipumba, Mbatia wamezungumia nini?

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa, Prof Lipumba amempongeza rais Magufuli kwa ahadi yake kuwa Uchaguzi Mkuu utakuwa huru na wa haki na kuwataka wanachama wote wa CUF kujiandaa kushiriki uchaguzi huo.

"Kwa upande wake Mhe. James Francis Mbatia pamoja na kufurahishwa na dhamira ya Mhe. Rais Magufuli juu ya Uchaguzi Mkuu kuwa huru na wa haki ametaka wanasiasa waache kukamiana na kuchochea mambo hasi dhidi ya Taifa, na badala yake waungane kuendeleza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ikiwemo kuboresha elimu, upatikanaji wa nishati na mengine yenye maslahi mapana kwa wananchi," imeeleza sehemu ya taarifa ya Ikulu.

Tanzania inatarajiwa kuingia kwenye uchaguzi baadae mwezi Oktoba.

Vyama vya upinzani nchi Tanzania vimekuwa vikimkosoa Magufuli na utawala wake kwa kuwaminya.

Vyama hivyo vimezuiliwa kufanya mikutano ya hadhara isipokuwa kwa wawakilishi wa maeneo kama wabunge.

Juma lililopita, vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa Mwenyekiti wa Chadema alikamatwa (na baadaye kuachiliwa) akihutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake licha ya kuwa na kibali kwa kuwa alizungumzia kuhusu Tume ya Uchaguzi.

Tahadhari ya virusi vya corona

Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

Maelezo ya picha,

Profesa Ibrahim Lipumba akiagana na rais Magufuli

Katika kuzingatia ushauri wa Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu, Rais Magufuli na viongozi hao wa walisalimiana bila kushikana mikono.

Magufuli na Maalim Seif badala ya kupeana mikono waligongeana miguu, huku viongozi wengine wote akisalimiana nao kwa ishara.

Hatua hiyo ni ya kujihadhari dhidi ya virusi vya corona.

Hakuna mtu ambaye amethibitika kuwa na virusi vya corona nchini humo.

Virusi hivyo tayari vimeshathibitishwa kuingia katika nchi tano za Afrika ambazo ni Misri, Algeria, Nigeria, Morocco na Senegali.

Zaidi ya watu 3,000 wamefariki duniani kote, wengi wao wakiwa raia wa Uchina ambapo