Coronavirus: Athari ya ugonjwa huu katika Soka ya Ulaya

Michezo mbalimbali yafutiliwa mbali kwasababu ya virusi vya Corona Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michezo mbalimbali yafutiliwa mbali kwasababu ya virusi vya Corona

Virusi vya Corona vyaendelea kuzua hofu. Bila shaka tuko katika nyakati zisizo za kawaida.

Mlipuko wa virusi vya Coona umesababisha michezo mingi tu kufuiiw ambali nchini Uingereza na kote duniani ikiwemo katika mchezo wa soka Uingereza. Jinsi mambo yalivyokuwa Ijumaa.

Janga la ugonjwa wa Corona limesababisha mechi nyingi kote duniani kufutiliwa mbali ndani ya saa 24.

Ijumaa, ligi ya Premier ilikuwa ndo moja ya mashinsan ya mpira wa soka mashabiki walikuwa wanasubiri hatma yake baada ya mkutano wa dharura kuitishwa.

Matokeo yake Ligi ya Premier na EFL ikatangaza kwamba hakuna tena michuano ya mpira wa soka mpaka Aprili.

Ukweli ni kwamba hakutakuwa na michezo yoyote ya mpira wa soka Uingereza katika kipindi cha wiki tatu zijazo huku mwanahabari wa BBC akisema kwamba kurejelelwa kwa ligi ya Premier League na EFL 3-4 April ni jambo ambalo lisilokuwa na uhakika.

Mchuano pekee ya soka uliokuwa umepangwa wikendi hii ilikuwa ni Wales v Scotland, lakini ukaahirishwa

Pia ikatangazwa kwamba mashindano ya London Marathon yaliyokuwa tafanyike Aprili yameahirishwa hadi Oktoba.

Maneja wa Arsenal Mikel Arteta ahahisi vizuri kwa sasa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alhamisi ilitangazwa kwamba Mikel Arteta amepata virusi vya Corona

Maneja wa Arsenal Mikel Arteta amesema kwamba sasa anahisi vizuri baada ya kuthibitishwa kuwa anavirusi vya Corona.

The Gunners wamesitisha mazoezi yao huku wale waliokuwa wametangamana na Arteta siku za hivi karibuni wakitakiwa kujitenga na wengine.

'' Asanteni kwa maneno yenu na usaidizi wenu ," raia huyo wa Uhispania, 37, ameandika kwenye mtandao wake wa Twitter. "Sote tunapambana na changamoto kubwa mabyohaijawahi kutokea hapo kabla.

"Afya ya kila mmoja wetu ndiyo jambo la msingi kwasasa. Tulindane kwa kufuata maagizo," aliongeza.

"kwa pamoja tutapita hili."

Athari ya kuahirishwa kwa Soka ya Uingereza sababu ya Coronavirus na Mwandishi wa BBC Spoti Simon Stone

Huenda kukawa na machaguo matatu pekee.

Msimu huu utangazwe kwamba umefutiliwa mbali wote na kuanza tena mwaka ujao na timu zilezile zilizokuwa kwenye msimu huu kwenye daraja lile lile,

Ama timu zingine zipandishwe na zingine zishushwe daraja, ama kwa kutumia matokeo ya msimu huu jinsi yalivyo kwa sasa

Ama kuongezwe mechi za ziada kuamua matokeo.

Machaguo yote haya yana utata na ndio sababu msimao mzuri ni kumaliza kampeni inayoendelea ingawa hakuna anayejua hilo litafanyika lini.

Kuna michuano tisa ya Premier inayotakiwa kuchezwa, na mingine mitatu ya makundi katika kombe la FA, na Ulaya.

Kulingana na gazeti la Times Jumamosi, mwenyekiti wa FA Greg Clarke aliiambia ligi ya Premier kuwa haoni uwezekano wa michuano ya ndani nyumbani kukamilika msimu huu.

Je kuna uwezekano kiasi gani wa msimu huu kuafutiliwa mbali kabisa?

Maoni ya mwandishi wa BBC Spoti Simon Stone:

Bila shaka hili sio tamanio la ligi na vilabu vingi kwamba litokee.

Kuna athari nyingi sana zinazotokea katika maamuzi kama hayo.

Hakika ni kwamba hakuna anayejua michezo hii itaahirishwa mpaka lini. Lakini pindi itakaporejea nifikiria kwamba kitakachotangulia ni kumaliza msimu huu kwanza.

Bado haijafahamika ikiwa wachezaji wataendelea na mazoezi au la.

Nini kitakachotokea kwa mashabiki ambao wameshanunua tiketi?

katika hali kama hii tiketi zinaweza kurejeshwa ikiwa mechi hazitakuwepo - na vilabu watazingatia mashabiki ambao hawawezi kubadilisha tarehe zao kwasababu ni jambo ambalo hawakulitarajia wakati wananunua tiketi hizo.

hata hivyo, baadhi ya vilabu zimeshiriki mechi nne au tano tu. Tiketi za msimu hicho ni kitu tofauti. Msimu bado haujakamilika, hadi kufikia sasa, sioni ikiwezekana watu kurejeshewa pesa zao. Lakini jambo hili huenda likaangaziwa zaidi katika kipindi cha wiki mbili au tatu zijazo.

Ronaldo atuma Ujumbe

Haki miliki ya picha Getty Images

kamba ambavyo huenda mumesoma, mchezaji wa Juventus Daniele Rugani amethibitishwa kuwa na viusi vya Corona na kwasasa anendelea vizuri.

Matokeo yake ni kwamba wafanyakzi wengi wa Juventus na wachezaji kwa sasa wako katika karantini ya binafsi.

Aliyekuwa mchezaji wa dunia wa mwaka Cristiano Ronaldo ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii Ijumaa:

''Kwa sasa dunia iinapitia kipingi kugumu ambacho kinata sote kuwa makini. Leo hii ninazungumza na nyinyi sio kama mchezaji wa soka lakini kama mtoto, baba, mwanadamu mwenye wasiwasi kuhusiana na kile kinachokumba dunia kwa sasa...'' ''Ningependa kutuma salamu zangu za rambirambi kwa yeyote ambaye amepoteza mpendwa wake, niko pamoja na wale wanaougua virusi hivi kama mchezaji wa timu tangu Daniele Rugani na pia naendelea kuunga mkono juhudi za dhati za wtaalamu wa afya ambao wanahatarisha maisha yao kusaidia wengine.''

Sergio Ramos

"Tuangalie kwa mtazamo mwengine, kufurahia na familia," ameandika Sergio Ramos mchezaji wa real Madrid kwenye Instagram.

Timu ya Real Madrid wako katika karantini baada ya mchezaji mmoja wa timu hiyo ya mpira wa kikapu kupatikana na virusi vya Corona.

'Kila aliyeathirika namtakia uponyaji wa haraka'

Ujumbe huu ni kutoka kwa mchezaji wa Tottenham Dele Alli: "Katika hali ya sasa maisha na afya vinapewa kipaumbele, mpira wa soka utarejea dunia itakapokuwa tayari! Namtakia kila aliyeathirika afueni ya haraka na natumai sote tutarejea kama kawaida haraka iwezekanavyo''

Ikiwa coronavirus itaendelea kwa miezi ijayo, je hii inamaanisha hakuna michuano itakayochezwa kabisa?

Mwanahabari wa BBC Spoti anachambua.

Hilo linawezekana. Kiuhalisia, michuano huenda ikachezwa wikendi hii. Ni vilabu ndio ambavyo vimefanya uamuzi huo - serikali imesema Alhamisi kwamba mechi huenda zikaendelea kwa sasa.

hakuna anayejua hali ya sasa itaendelea hadi lini. Sioni kama kuna mechi itakayochezwa hadi mlipuko wa virusi vya corona utakapodhibitiwa, ambapo wataalamu wa afya wanasema kwamba hilo linaweza kuchukua wiki 10 hadi 14.

Kwa kufuatilia ushauri wa kimatibabu, sioni kama kuna mtu anayetarajia hali hii kubadilika katika kipindi cha wiki tatu zijazo na hivyobasi, kuna uwezekano mkubwa hali ya sasa ikaendelezwa kuliko kuondolewa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii