Ni miaka ishirini tangu waumini 700 kujiteketeza Uganda kwa kuamini ni mwisho wa dunia

The four cult leaders Haki miliki ya picha .
Image caption Miaka 20 imepita tangu tukio lililoteketeza watu 700 (kutoka kushoto mpaka kulia) Ursula Komuhangi, Credonia Mwerinde, Joseph Kibwetere na Dominic Kataribabo

Judith Ariho anasema kuwa huwa hatoi machozi yeyote anapokumbuka tukio ambalo liliuwa mama yake na ndugu zake wawili pamoja na ndugu zake wengine wanne ambao walikuwa wamejifungia katika kanisa.

Machi, 17 , ni miaka 20 imepita, mamia ya wanachama wa dhehebu la Amri Kumi za Mungu nchini Uganda walijifungia katika kanisa moja, na kisha kujitekekeza kwa moto saa za mchana.

Takwimu za polisi zinasema kwamba zaidi ya watu 700 walikufa, huku kukiwa na walakini kwamba huenda idadi ilikuwa ni zaidi ya hiyo.

Makao makuu ya kanisa hilo yapo Kanungu, kusini-magharibi mwa Uganda. Waumini waliambiwa wauze mali zao zote kwa sababu mwisho wa dunia ulikuwa umefika.

Ni miongo miwili sasa imepita lakini bado tukio hilo ni kidonda kikubwa kwa bi.s Ariho, ambaye a naonekana kuwa amekubali kile kilichotokea kwa kutotaka kufikiria tena tukio hilo.

Image caption Picha za kanisa lililotekea moto nchini Uganda

Watu waliouwawa walikuwa waumini wa kanisa la Amri Kumi za Mungu ambao waliamini kuwa dunia imefika mwisho.

"Huu ni mwisho wa dunia", kwa sababu kitabu kimoja cha Mungu kiliandika kuwa Machi 17, 2000.

Miaka ishirini ijayo , hakuna mtu aliyeshtakiwa kuhusishwa na mauaji hayo ya waumini na viongozi wake, haijafahamika kama kuna viongozi wa kanisa hilo ambao wapo hai au la yaani hakuna kilichobainika mpaka sasa.

Anna Kabeireho, ambaye bado anaishi eneo la milimani, hajasahau tukio hilo kuanzia hata harufu ya moto uliokuwa unafuka majira ya asubuhi siku ya ijumaa.

"Kila kitu kilikuwa kimefunikwa kwa moshi na harufu ya nyama mbichi ilikuwa imetanda. Yaani harufu kama ilikuwa inaingia kwenye mapafu," anakumbuka.

"Kila mtu alikuwa anakimbilia katika bonde la maji. Moto ulikuwa unaendelea.

Miili mingi ilikuwa imeungua na hata hawakujulikana walikuwa ni kina nani.

"Tulikuwa tunafunika pua kwa majani ya migomba ilikuzuia harufu. Kwa miezi kadhaa hatukuweza kula nyama."

Kanungu ni sehemu yenye ardhi ambayo ina rutuba , lakini amani iliondoka baada ya kuzuka kwa moto huo.

Haki miliki ya picha BBC/Patience Atuhaire

Mapadre na watawa waliotengwa

Imani ambayo iliwafanya viongozi wa kikaresmatikis Credonia Mwerinde, mhudumu wa zamani kilabu cha pombe na mfanyabiashara wa ngono na mfanyakazi wa zamani wa serikali Joseph Kibwetere, ambaye alisema kuwa amepata maono kutoka kwa bikira maria tangu mwaka 1980.

Kundi hilo la kidini ambalo linaheshimu amri kumi za Mungu na kahubiri habari za Yesu.

Ishara ya ukiristo katika kundi hilo la kikristo ambalo lilikuwa halina uhusiano mzuri na kanisa katoliki lili na wahudumu wake ni mapadri na watawa ambao walikuwa walikuwa wametengwa na kanisa wakiwemo Ursula Komuhangi na Dominic Kataribabo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabaki yaliyopatikana baada ya kanisa kuungua

Waumini walikuwa kimywa, walipokuwa wanatumia njia ya kuwasiliana.

Bi. Ariho, mwenye umri wa miaka 41, alijiunga na kundi hilo pamoja na familia yake akiwa na miaka 10.

Mama yake ambaye alikuwa mjane alikuwa anahangaika kuwalewa watoto wake watatu.

Mmoja alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kichwa kila mara.

Aliingia katika kundi la Kibwetere kwa ajili ya maombi.

Jumuiya hiyo ilichukua familia yote na kuisaidia katia mahitaji yao kuanzia kwenye ada za shule mpaka chakula.

Familia ya bi. Ariho ilikuwa na waumini kama 1000 ambao walikuwa wanatoka njie kidogo ya mji wa Rukungiri.

"Maisha yetu yalizungukwa na sala na kilimo tu,"alisema.

"Tulifanya kila kitu ilii kujizuia kutenda dhambi. Wakati mwingine ukifanya dhambi unapaswa kusali rozari mara 1,000.

Ilikuwa kama adhabu na ulikuwa unaomba rafiki zako au familia kukusaidia kusali rozari.

Haki miliki ya picha BBC/Patience Atuhaire
Image caption Mawe ambayo yalifananishwa na bikira maria

Anasema kuwa kuna familia ambayo ilipoteza mama na watoto 11

Bi. Ariho hajaenda Kanungu tangu mwaka 2000 aliolewa na familia ambayo iikuwa haiamini kundi hilo.

Lakini anakumbuka jinsi alivyouwa anasali wakati huo na jinsi viongozi wao Mwerinde na Komuhangi walivyokuwa wanawaongoza.

Kama mtu asipofuata sheria , wanawake wawili walilia machozi ya damu.

Inaonekana viongozi hao walikuwa wanahusika na mauaji na utesaji wa waumini.

Kabla ya kuanzisha kundi lake la imani, Kibwetere alikuwa mtu mwenye mafanikio makubwa na alikuwa muumini wa kawaida wa kanisa katoliki.

Haki miliki ya picha BBC/Patience Atuhaire
Image caption Mabaki ya kanisa la Amri za Mungu

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC