Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 24.03.2020: Rice, Rose, Edouard, Bellingham, Alaba, Osimhen, Tonali

Jose Mourinho Haki miliki ya picha ANP Sport/Getty Images

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amekuwa akisaidia wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona kwa kuwapelekea chakula wazee karibu na uwanja wa mazoezi wa Spurs katika eneo la Enfield. (Football.London)

Arsenal inakusudia kujipanga kwa msimu ujao kwa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Celtic ambaye ni raia wa Ufaransa Edouard, 22. (Mirror)

Newcastle inatarajia kumsaini moja kwa moja beki Danny Rose, 29, pindi dirisha la usajili likifunguliwa. (I Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Declan Rice (kulia) akimkaba mshambuliaji wa Man City Kun Aguero

Klabu ya Chelsea inavutiwa kumsajili kiungo mkabaji wa West Ham na England Declan Rice, 21, katika dirisha la majira ya kiangazi. (Sky Sports)

Manchester United wamepata anguvu mpya ya kumsajili kinda wa Birmingham Jude Bellingham, 16, baada ya Borussia Dortmund kufuta mipango yao ya kutaka kumsajili. (Mirro

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alaba anatazamiwa kukataa ofa ya kujiunga na Man City

Beki wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 27, anatazamiwa kugoma kukataa ofa ya kujiunga na Manchester City mwishoni mwa msimu ili ajiunge na miamba ya Uhispania Real Madrid au Barcelona. (Bild, via Sports Mole)

Mechi za Ligi ya Premia zinaweza kuchezwa nje ya jiji la London pale ligi itakapofunguliwa kwa kuwa jiji hilo lina idadi kubwa ya wagonjwa wa virusi cya corona. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Victor Osimhen

Mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21,anapigiwa upatu kuwa "kipaumbele" cha klabu ya Manchester United katika dirisha lijalo la usajili. (Le10 Sport, via Star)

Manchester City wanataka kumsajili kiungo wa Brescia na Italia Sandro Tonali, 19. (Corriere dello Sport, via Sport Witness)

Tottenham wanavutiwa kumsajili kiungo wa QPR Eberechi Eze, 21, wakati klabu za Crystal Palace na Sheffield United, ambaye walianza kuoesha nia ya kumsajili kutokuwa tayari kulipa kitita cha pauni milioni 20 ambacho QPR wanakitaka. (Express)

Mada zinazohusiana