Virusi vya corona: Tanzania kufufua safari za ndege za abiria na watalii, je imejipanga vipi?

Virusi vya corona: Tanzania kufufua safari za ndege za abiria na watalii, je imejipanga vipi?

Tanzania litakuwa taifa la kwanza barani Afrika kuruhusu ndege za watalii na abiria wengine kutua nchini humo.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Rais John Pombe Magufuli, na inachukuliwa kama mojawapo ya mikakati ya kufufua sekta ya utalii ambayo ni ya pili katika kuchangia pato la kitaifa yani GDP.

Lakini Tanzania imejipanga vipi kuwapokea watalii hao?.

Ili kupata jibu, Mwandishi wa BBC Lynace Mwashighadi amezungumza na Waziri wa Utalii nchini Tanzania Hamisi Kigwangalla, ambaye kwanza alielezea ni wapi watalii hao watakakotoka...