Virusi vya Corona: Mapambano dhidi ya Corona DRC

Vendors and shoppers at Kituku market on the shores of Lake Kivu in Goma

Chanzo cha picha, Moses Sawasawa for Fondation Carmignac

Makala inayoonyesha kwa picha changamoto ambazo raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliana nazo katika mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

'Congo in Conversation' ni tovuti inayoonyesha mahangaiko wanayopitia watu wa taifa hilo katika upande wa kijamii na kiafya kutokana na janga hilo la afya.

Makala za ripoti ya picha na video zitakuwa znawekwa na waandishi wa habari na wapiga picha ambao wanaishio DR Congo, na wengi wao wakiwa raia wa nchi hiyo.

Tovuti hiyo inaandaliwa na taasisi ya Carmignac na mpiga picha raia wa Canada-Uingereza Finbarr O'Reilly.

Taasisi hiyo ya Carmignac inatoa ufadhili kwa watu kila mwaka kuangazia masuala ya haki za binadamu na mazingira.

O'Reilly alitunukiwa mara 11 katika tuzo za uandishi wa picha za Carmignac. Ikiwa sehemu ya tuzo hiyo , mpiga picha alipanga kutoa ripoti ya picha ya DR Congo ya mwaka 2020.

Lakini kufungwa kwa mipaka kutokana na mlipuko wa corona , yeye na timu nzima ya tuzo hizo walibidi wafikirie tena namna ya kuripoti katika nchi hiyo.

Na hii ikafaya Kongo kuwa kwenye mtandao huo wa Conversation

Chanzo cha picha, Justin Makangara for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Mtu akiwa amevalia mavazi ya kujikinga na maambukizi ya corona katika mlango wa kuingilia jengo la Gombe lililopo mji mkuu wa DRC, Kinshasa. Mtu huyo alikuwa anatoa elimu kwa watu kukaa kwa umbali na kupimwa joto wakati wanaingia na kutoka katika jengo hilo

Chanzo cha picha, Justin Makangara for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Watu walivyokuwa hawachukui tahadhari wakati mlipuko wa virusi vya corona umeanza kuingia

Mratibu wa mradi huyo alikuwa anatokea London, O'Reillyalikuwa akifanya kazi na waandishi wa habari wengine nchini humo ili kupata picha za video na kawaida na taarifa hizo zilikuwa zikichapishwa mtandaoni.

"Kwa muda mrefu , habari kutoka Afrika zilikuwa zinaandikwa na wageni na mara nyingi zilikuwa hazielezi uhalisia wa mambo bali tabia za ukoloni na ubaguzi katika kusimulia taarifa hizo zilikuwa zinaonekana katika uwakilishi," alisema O'Reilly.

"Tunashukuru , tumeanza mabadiliko kwa miaka ya hivi karibuni wakati ambao waandishi wengi wa Afrika wanatumia majukwaa ya mtandaoni kusimulia habari zao. Kwa sauti zao wenyewe na kufafanua mawazo yao."

Pamoja na kwamba nchi yangu iko kwenye marufuku ya kutoka nje, lakini mamilioni ya raia wa Congo huwa wanategemea kipato kisicho rasmi kuweza kuishi.

Chanzo cha picha, Justin Makangara for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

soko moja mjini Kinshasa.

"Tangu mtu wa kwanza kutangazwa kuwa na virusi vya Corona nchini DR Congo, taarifa za uzushi zimekuwa zikiibuka kuhusu virusi hivyo kusambaa katika mji mkuu wa Kinshasa," alisema Justin Makangara, mmoja wa wapiga picha.

"Jambo ambalo lilikuwa linaamikia kwa wengi kuhusu Covid-19 kuwa ni ugonjwa wa watu matajiri '.

"Ubaguzi uliibuka kwa watu wachache wakiwemo wapenzi wa jinsia moja kwa madai kuwa virusi hivi vya corona vimekuja kwa sababu ni adhabu kutoka kwa Mungu dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja.

"Walakini, juhudi zinazofanywa katika mapambano dhidi ya janga hili licha ya mapambano ya kiuchumi na kijamii yanayonaendelea nchini humu, kwa utengenezaji wa vitambaa na misaada inayoendelea hapa na pale kusaidia walio katika hatari zaidi".

Chanzo cha picha, Moses Sawasawa for Fondation Carmignac

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa , nusu ya watu wa Afrika watapoteza ajira zao.

Chanzo cha picha, Moses Sawasawa for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Wachuuzi katika soko la Kituku ufukweni mwa ziwa Kivu.

Chanzo cha picha, Ley Uwera for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Vendors at a street market in Goma.

"Nikiwa mpiga picha mdogo wa Congo, Ninajivunia kushiriki katika mapambano dhidi ya mlipuko huu wa dunia ,"alisema Moses Sawasawa.

Maelezo mengi yanaeleza hali ya kisiasa ambayo imekuwa ikiathiri kwa miongo kuiaminisha dunia lakini licha ya vita, vijana wa Kongo wana vipaji vingi.

" Kwangu mimi, jambo sahihi kuhusu mlipuko huu ni kuwa ninaweza kusema ukweli na kuonyesha kile ambacho watu wanakabiliana nacho katika kipindi hiki cha janga pamoja na kueleza hali ya kiuchumi na kijamiiilivyo katika nchi yangu."

Chanzo cha picha, Justin Makangara for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Siku ya Jumapili, Aprili 5 majira ya saa tatu usiku. Gombe ilikuwa inajiandaa kwa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku s 14-

Chanzo cha picha, Justin Makangara for Fondation Carmignac

Covid-19 sio mlipuko ambao DR Congo inapambana nao kwa sasa.

Tangu Januari 2019, zaidi ya watoto 6,500 walifariki kwa surua katika nchoi hiyo, na watu 335,000 wameambukizwa,kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani (WHO) .

Zaidi ya miezi 18 nchi hiyo imekuwa ikikabiliana na ugonjwa wa ebola , janga la pili kubwa duniani katika historia - watu 3,453 waliugua ugonjwa huo na vifo vilikuwa 2,273.

Chanzo cha picha, Finbarr O'Reilly for Fondation Carmignac

"Kama ukimuangalia kijana wa nchi hii, wanajihangaikia wenyewe kutatua matatizo yao ," alisema O'Reilly.

"Hawakubaliani na uongozi mbaya na kunyanyaswa kupata haki ."

Chanzo cha picha, Finbarr O'Reilly for Fondation Carmignac

"Vijana wanachukua jukumu la serikali , katika upande wa kutoa elimu na huduma za kiafya ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

"Na kwa sababu Congo ilipitia wakati mgumu wa mlipuko wa Ebola , wakati huu walikuwa wana ujuzi katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko."

Chanzo cha picha, Finbarr O'Reilly for Fondation Carmignac

Chanzo cha picha, Finbarr O'Reilly for Fondation Carmignac

Maelezo ya picha,

Jeneza lililobeba maiti ya mtu aliyekufa kutokana na Ebola

Picha kwa idhini ya Congo in Conversation