Je,Trump yuko mashakani kwa msimamo wake kuhusu ubaguzi wa rangi?

Trump holds a Bible that was carried from the White House by his daughter Ivanka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Viongozi wa dini wamelaani vikali picha ya Trump nje ya kanisa

Kura kadhaa za maoni zinaonesha kuwa Trump yupo nyuma ya mgombea urais wa Democrat Joe Biden kwa wigo mpana.

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Kuna ripoti kuwa kambi ya kampeni ya Trump imeandamwa na migogoro, na urais wake umekumbwa na janga baada ya janga.

Je changamoto hizi kwa Trump ni za muda tu ama uwezekano wa kuchaguliwa tena ni mdogo?

Donald Trump ni mwanasiasa asiyetabirika.Miaka minne iliyopita aliingia kikaangoni na kuonekana kutofaa - lakini akaweza kupindua matarajio ya wengi- akashinda tiketi ya urais kwa chama chake na kushinda uchaguzi mkuu.

Safari ya namna hiyo, kama inavyotarajiwa, inampa mtu kujiamini zaidi katika maamuzi.

Katika hali ya kawaida, ni rahisi kuona namna ambavyo Trump alipata ushindi miaka minne iliyopita baada ya kupita kwenye tanuri la kashfa na magomvi na kudhani kuwa atafanya hivyo pia mwaka huu.

Wataalamu walikosea miaka minne kwenye tathmini zao. Trump alikea sahihi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakika Trump alikuwa sahihi katika baadhi ya mambo. Aliingia ulingoni akiwa mgeni wa siasa katika kipindi ambacho raia wengi walikuwa wamechoshwa na mfumo wa siasa za nchi hiyo. Akatumia mwanya huo ipasavyo kushinda uchaguzi.

Miaka minne mbele, Trump anaamini mbinu zake za 2016 zitamsaidia Novemba 2020 - bado anauaminisha Umma kuwa yeye si mwanasiasa wa kawaida ambaye anaminyana na mpinzani ambaye ni mwanasiasa wa kawaida.

Mbinu zake zinakubalika na wafuasi wake, ambao walijitokeza kwa wingi kupiga kura 2016. Wahafidhina na wapiga kura ambao hawana msimamo thabiti walimpigia kura wakitaka kujaribu bahati yao kuleta mabadiliko.

Kwa sasa, Trump anajulikana kwa wapiga kura

Wafuasi wake wanakadiriwa kuwa ni asilimia 30 mpaka 40 ya wapiga kura wote, kwa mujibu wa kura za maoni - idadi hiyo haimtoshelezi kurejea White House - hususan kama ataendelea kupoteza imani ya wazee, wasomi wa mijini na watu wa dini.

Baadhi ya matendo yake ya sasa pia ni zaidi ya mbinu zake za 2016 - mathalani kuzua tashwishi, kuchochea magomvi kutokana na masuala ya kijamii, kuibua dhana potofu na kujibu mashambulizi kwa kila anayemkosoa.

Wiki mbili zilizopita, vikosi vya askari walisambaratisha watu ili kuacha njia wazi nje ya Ikulu ya Marekani muda mfupi tu kabla ya rais Trump kupita kwenda kupiga picha nje ya kanisa huku akiwa ameshikilia biblia.

Tangu wakati huo ameonekana akiendelea kutetea hatua yake kwa kufananisha na jinsi ilivyokuwa rahisi kwa vyombo vya usalama kuondoa watu katika eneo la ikulu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waandamanaji walirushiwa mabomu ya machozi ili kuacha njia kwa rais kupita kwenda kanisani

Kwa muda kidogo viongozi na maafisa ambao hawakuwa na sare wamekuwa wakijiweka mbali kidogo na tukio hilo.

Baadhi ya maafisa wa jeshi wastaafu akiwemo katibu wa ulinzi James Mattis, alitaja hatua hiyo kuwa ya kipuuzi.

Naye katibu wa sasa wa ulinzi Mark Esper na mkuu wa jeshi Mark Milley amekiri kuwa alikosea kuungana na Rais Donald Trump wakati wa alipotembea kuenda kanisa lililopo karibu na Ikulu ya Marekani ambalo liliharibiwa na waandamanaji.

Tukio hilo la Juni tarehe moja na ambalo lilizua utata lilionesha "taswira kwamba jeshi linajihusisha na siasa za ndani ya nchi", Jenerali Mark Milley alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kama atashindwa uchaguzi mwezi Novemba, haitakuwa kwa sababu ya kufanya mabadiliko makubwa ya sheria ambayo yalikuwa daraja kwake kisiasa" ameandika Rich Lowery, mhariri wa jarida 'the conservative National Review'.