Wachezaji wa EPL kuvalia fulana za 'Black Lives Matter’

Wachezaji wa Ligi Kuu ya England watavalia jezi iliyochapishwa maneno 'Black Lives Matter'

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wachezaji wa Ligi Kuu ya England watavalia jezi iliyochapishwa maneno 'Black Lives Matter'

Wachezaji wa Ligi Kuu ya England watavalia jezi iliyochapishwa maneno 'Black Lives Matter' mgongoni katika mechi 12 za mwanzo ligi hiyo itakaporejelewa Juni 17.

Ligi ya Primia pia itamuunga mkono mchezaji yeyote atakayeamua 'kupiga goti' kabla ama wakati mechi ikiendelea.

Wachezaji nchini Ujerumani pia walichukua hatua kama hiyo kuwaunga mkono watu wanaopinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd.

"Sisi, wachezaji tumekuja pamoja kwa lengo moja tu la kukomesha ubaguzi wa rangi," taarifa ilisema ujumbe uliotolewa na klabu hizo.

Katika ujumbe wa pamoja kutoka klabu 20, wachezaji hao waliongeza kuwa wamejitolea kuungana na "jamii ya kimataifa, kuhakikisha ulimwengu una heshimu na kuwapatia watu wote nafasi sawa bila kujali misingi ya rangi ya ngozi ya mtu ama mahali wanakotoka".

Nembo ya 'Black Lives Matter' itachapishwa kwenye fulana ya kila mchezaji hadi msimu utakapokamilika pamoja na kuwapongeza wahudumu wa afya kwa juhudi Zao kabambe wakati wa mlipuko wa virusi vya corono.

Wachezaji wa Klabu kadhaa za Ligi ya Primia tayari wameonekana 'wakipiga goti' wakiwa kwenye mazoezi katika picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Wanaharakati wa shirika moja la kupinga ubaguzi wa rangi lilikuwa limetoa wito wachezaji wapewe uhuru wa wa kupiga goti wakiwa uwanjani kama ishara ya kupinga ubaguzi.

Shirikisho la kandanda nchini Uingereza limesema litatumia "busara" kufanya kushirika maandamano kama hayo.

Wachezaji wanne, miongoni mwao mshambuliaji wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, awali walichunguzwa na mamlaka ya Bundesliga kwa kuonesha wazi anaunga mkono maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd,46, mikononi mwa polisi mwezi uliyopita.

Hakuna hata mchezaji mmoja aliyechukuliwa hatua baada ya shirikisho la kandanda chini Ujerumani kusema kuwa litaendelea kuruhusu hatua hiyo katika wiki kadhaa zijazo.

Ligi ya Primia itarejelewa Juni 17 lakini bila mashabiki uwanjani baada ya kusitishwa kwa miezi mitatu kutokana na janga la corona.

'Ni mwanza mzuri, lakini nataka kuona matokeo halisi'

Kiungo wa zamani wa England, Newcastle na Spurs Jermaine Jenas, ambaye alicheza mechi 280 za ligi ya Primia kati ya 2002 na 2013, anatumai kampeini hiyo ya kushinikiza mabadiliko itaendelea zaidi ya mechi hizo 12.

Akizungumza na BBC BBC Radio 5 Live, alisema: "Ni wazoo Zuni kwamba klabu zote na wachezaji wao wamekuja pamoja na kusema hiki ndicho kitu tunachotaka.

Nadhani ni ujumbe muhimu kwa sababu Ligi ya Primia ni maarufu sana duniani.

Maelezo ya sauti,

Jadon Sancho aonesha tisheti ilionadikwa haki kwa George Floyd

"Naunga mkono kampeini hii kwa sababu inajumuisha wadau wote. Lakini swali linaloulizwa na kilt mtu ni: nini kitakachofuata?

"Nini kitakachofuata baada ya mechi hizo 12?

Inamaana juhudi hizi zitafifia hivyo tu?...

Ama tutashuhudia mabadiliko ya kweli uwanjani na katika nyumba zetu?

"Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu ukosefu wa makocha Waafrika ama kutopewa nafasi.

Tunachohitaji ni kukomesha mjadala huu kwa kuanza kutekeleza suala la [usawa] katika kiwango cha uajiri wa wasimamizi, katika klabu kubwa za FA."