John Nzenze: 'Mwanzilishi wa ‘bendi bora Afrika’

John Nzenze and Daudi Kabaka

Chanzo cha picha, The Standard

Maelezo ya picha,

John Nzenze (kushoto) na Daudi Kabaka (kulia) swalianza maisha kwa kazi ya uhudumu hotelini

John Nzenze,mwanamuziki nguli wa Kenya ambaye anazikwa Jumamosi ya leo, alipata umaarufu hata kabla ya nchi kaputa uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopiita.

Mwana muziki huyo ambaye alisifika kwa upigaji gita na kucheza densi alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliofanya mtindo wa miondoko ya Twist kupata umaarufu nchini Kenya miaka ya 1960 na 1970.

"Unapokuwa mtu mashuhuri, unakuwa mwenye kiburi, na kwa kiburi changu nilianzisha bendi yangu mwenyewe, bendi ya Air Fiesta Matata," alisema kwenye mahojiano ya Januari.

Bendi hiyo ilijumuisha- wakimbizi kutoka Congo, ambayo sasa inafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - ilipata umaarufu wa kimataifa miaka michache badae ya kuundwa kwake.

1968, iiliorodheshwa kuwa bends ya tatu bora katika tamasha la muziki wa Afrika nchini Algeria, na mwaka uliyofuata ikakita kambi Ethiopia kwa miezi kadhaa kumtumbuiza kiongozi wa chi hiyo Haile Selassie.

Mwaka 1971, Idhaa ya BBC Africa iliitambua bendi hiyo kama bendi bora barani Afrika katika hatua ambayo iliifanya kupata mualiko wa tamasha ya muziki nchini Uingereza mwaka uliyofuata ambapo walishiriki jukwaa moja na James Brown na kundi la Osibisa.

Chanzo cha picha, President Records

Maelezo ya picha,

Bendi ya Air Fiesta Matata ikitumbuza nchini Uingereza 1972

Lakini safari hiyo ndio ilikuwa mwisho wa bendi hiyo, kwani baadhi ya wanachama wake - Wakenya na Wacongo - waliamua kubakia Uingereza.

"Safari ya kurudi nyumbani [Kenya] ilipowadia, Wacongo walisema wako radhi kuwa wakimbizi Uingereza badala ya Kenya… na hapo ndipo bendi ilisambaratika. Tulitengana London," Nzenze alisema.

Lakini muziki wake uliendelea kukua hata alipoamua kuimba peke yake aliporudi Kenya, na baadaye kujiunga na bendi zingine na kufanya kazi kama mtayarishi katika Studio ya Philco Studio mjii Nairobi Kenya.

Nzenze alianzaje kukuza tasnia yake ya muziki?

Alizaliwa mjini Nairobi wakati Kenya ikiwa iatawaliwa na waingereza mwaka 1940, Nzenze alisomea mjini magharibi mwa Kenya, ambako ndio asili ya wazazi wake.

Alimaliza elimu yake ya sekondari, na baada ya hapo akapata ajira katika hoteli.

Wakati wa ujana wake alianza kupiga gitaa ambayo ilikuwa ya baba yake, ambaye alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya reli.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

John Nzenze amekulia Nairobi tangu miaka ya 1940

Katika hoteli inayofahamika kwa jina la Norfolk Hotel, alipata kazi ya kuhudumia chakula yaani weita, Nzenze alianza maisha akiwa anaishi na mfanyakazi mwenzie Daudi Kabaka, ambaye walikuwa wanaimba na kurekodi nyimbo pamoja katika chumba chao hicho.

Lakini Nzenze alikuwa hafurahii kuwa sifa zote zinaenda kwa Kabaka hata kwa nyimbo ambazo alitunga mwenyewe tu.

Alitaka kurekodi nyimbo zake na zifahamike redioni kama vile Kabaka, na hiyo ikamfanya aende kutafuta kundi moja la wanamuziki kutoka katika kampuni nyingine ya kurekodi muziki na kufanikiwa kurekodi wimbo wake wa kwanza Angelike.

Kwake Nzenze wimbo wake wa Angelike ambao alikuwa una maudhui ya mapenzi kuchezwa redioni ilikuwa si suala la fedha tu bali bali jambo hilo lilikuwa na maana kubwa katika maisha yake.

Angelike, wimbo ambao ulipata umaarufu mkubwa, wimbo aliokuwa anaimbiwa mpenzi kurudi nyumbani licha ya changamoto nyingi nyumbani.

Pembe tatu za upendo

Lakini kabla ya kuimba wimbo wa Angelike, aliimba wimbo na Kabaka kuhusu Agneta,mpenzi wake ambaye pia alitokea kuwa mpenzi wa rafiki yake - ingawa hakujua wakati huo.

Alikuwa ni muiombaji wa taratibu na uimbaji wake wa kimahaba, kusifu na mara nyingine aliwaimbia wanawake aliowapenda.

"Kama huwezi kumfanya mwanamke afurahi, muziki wako hauwezi kuwa na thamani kubwa. Kama wanawake watapenda wimbo wako hata wanaume pia watapenda wimbo huo," alisema.

"Tulikuwa vijana wadogo na tulikuwa tumezungukwa na mapenzi," aliongeza.

Alikosoa muziki wa leo

Nzenze anasifia muziki wa bendi na kukosoa muziki wa sasa ambao ni wa kidigitali, anasema muziki huu wa sasa haujawasaidia wanamuziki kuwa wabunifu na kutumia talanta yao vilivyo.

"Wanamuziki wengi hawawezi hata kukwambia nota za muziki wao;ni muangozaji muziki tu ndio anafahamu," alisema.

Aliongeza kusema kuwa muziki wao ulikuwa unakaa muda mrefu kwa sababu ya maudhui.

"Nilikuwa natengeneza muziki haswa, sio muziki nikitengeneza leo na kesho haupo sokoni," aliiambia BBC Swahili mwaka 2015.

Chanzo cha picha, The Standard

Maelezo ya picha,

John Nzenze performs during Mashujaa (Heroes) Day celebrations in October 2018.

Miziki mingine aliyoimba Nzenze na kupata umaarufu ni Ninamulilia Susanna, Veronica, Ni Vizuri kuwa na Bibi na Marashi ya Warembo .