Kiongozi mwafrika atafanya mabadiliko gani katika Shirika la Biashara Ulimwenguni

  • Zawadi Mudibo
  • Mhariri wa biashara Afrika
Composite image of the three candidates

Chanzo cha picha, Getty Images

Wagombea watatu kati ya wanane wanaowania kuwa kiongozi anayefuata wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) ni Waafrika, lakini kuna tofauti gani kuwa na Mwafrika kwenye usukani na kutaleta mabadiliko gani barani?

Kuna hisia inayoongezeka kati ya wanadiplomasia wa Kiafrika kwamba mtu kutoka bara anapaswa kuwa katika uongozi wa moja ya taasisi kuu za uchumi duniani.

Wakati Mmarekani amekuwa akiongoza Benki ya Dunia kila wakati, Mzungu akiwa anaongoza Shirika la Fedha Duniani, Mwafrika hajawahi kuchukua wadhifa sawa.

Lakini ikiwa mmoja kutoka Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria, Amina Mohamed wa Kenya au Abdel-Hamid Mamdouh wa Misri atatoka kwenye mchakato wa uchaguzi mrefu kama mkurugenzi mkuu wa WTO, bara linaweza kuhisi kwamba linacheza kwenye ligi sawa na wengine wote ulimwenguni.

WTO huweka sheria za biashara ya ulimwengu na huamua katika mizozo ya kibiashara kati ya mataifa. Pia, kulingana na tovuti yake, inapaswa kuendeleza "biashara wazi kwa faida ya wote".

Uwezo wa shirika lenye makao yake Geneva kupata makubaliano ya ulimwengu ya kanuni za msingi ambazo kila nchi husaini umetiliwa shauku katika miaka ya hivi kariuni lakini kiongozi wa WTO ana ushawishi mkubwa.

Mkurugenzi mkuu anahudhuria mikutano ya G20 na G7 (mataifa tajiri zaidi duniani) na anaweza kutekeleza makubaliano kati ya viongozi wa ulimwengu.

Lakini kuna zaidi ya kupatikana kwa kiongozi huyu katika Afrika kando na wasifu wa kidiplomasia?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiwanda cha nguo nchini Kenya

Ingawa jukumu la Mkurugenzi Mkuu huhusisha usimamizi, kiongozi wa Kiafrika anaweza kusaidia kuhakikisha kuwa masilahi ya bara yanazingatiwa katika shughuli za WTO.

Mazungumzo ya biashara yanaweza kuonekana yenye kuzidi muda na kufanyika faraghani, lakini matokeo yake yanaweza kugusa maisha ya kila mtu.

Kutoka kwa mfanyibiashara mdogo ambaye huvuka mpaka mra kadhaa kwa mwezi, hadi kwa mteja akinunua bidhaa iliyoagizwa nje kwenye soko, kwa mtu aliye na kazi katika tasmnia ya utengenezaji- wote wanaathiriwa na sheria za biashara.

Barani Afrika, biashara inaonekana nguzo ya ukuaji, njia ya maendeleo endelevu na kama zana ya kutokomeza umaskini.

"Misaada ya nje haitafaidi Afrika. Kama mahali pengine popote katika historia ni biashara," anasema David Luke, mkuu wa kituo cha sera za biashara katika Tume ya Uchumi ya UN ya Afrika.

"Kwa hivyo Waafrika wa kawaida wataelewa kuwa mwafrika anayeongoza WTO anaonyesha tunazingatia biashara."

Bi Okonjo- Iweala aliambia BBC kwamba anajali zaidi mwafrika wa kawaida katika sera zake. Alisema kuwa alitaka "kujua jinsi ya kupata wanawake na vijana, ambao wako nyuma ya injini hizi za ukuaji barani Afrika, kufaidika zaidi na biashara ya ulimwengu".

Chanzo cha picha, Getty Images

Alikuwa na nia ya kuhakikisha kuwa bara linaondoka katika kusafirisha malighafi na badala yake linajishughulisha mno na "kuongeza thamani kwa bidhaa tunazozalisha kwa soko la kimataifa.

Kwa mfano, tunaagizia asilimia 94 ya dawa kwenye bara wakati tunaweza kuzalsiha haa Afrika."

Bi Mohamed, ambaye amewahi kuwa waziri wa biashara na wa maswala ya nje nchini Kenya, aliambia BBC kwamba anaweza kuleta "mtazamo mpya" ambao ulikuwa "pana [na] unaojumuisha kazi hiyo.

Lakini hakutaka kuhukumiwa wala kuonekana kama kiongozi wa kiafrika au mwanamke tu, bali kama kiongozi mzoefu [na] mjenzi wa makubaliano"

Kwa upande wake Bw Mamdouh, ambaye amekuwa akifanya mazungumzo kwa niaba ya Misri tangu mwaka wa 1985, alisema uzoefu wake mkubwa katika shirika hilo la biashara utamwezesha kuona jinsi gani unaweza kulisaidia bara lote zaidi.

"Ajenda yangu kwa Afrika itakuwa kuwajumuisha waafrika zaidi katika mfumo wa biashara," alisema.

"Pia nitatoa wito kwa viongozi wa kisiasa katika nchi za kiafrika kuzingatia sera zao za kibiashara."

Maelezo ya video,

Watu 8 wameteuliwa kuwania wadhfa wa mkurugenzi mpya wa Shirika la biashara Duniani WTO

Lakini dhahiri katika jibu hili ni kwamba ingawa mkurugenzi mkuu wa WTO anaweza kushawishi marais, yeye hawezi kuwalazimisha kutenda kwa njia fulani!

Walakini, lijapo suala la kusaidia kutambua sera kubwa ya biashara ya Afrika- Mkataba wa Biashara Huria (Huru) ya Bara la Afrika (AfCTA)- mkuu wa WTO anaweza kuchukua jukumu.

Makubaliano hayo ambayo utekelezwaji wake umeahirishwa kutokana na janga la virusi vya covid- 19, unatarajia kuanzisha eneo kubwa zaidi la biashara huria duniani.

"Hii itahakikisha bidhaa za hali ya juu zaidi kutoka bara, na hivyo, kuweka pesa zaidi katika mifuko ya watu na kusaidia kutokomeza umaskini wa muda mrefu," mtaalam wa biashara Bw Luke alisema.

Sheria na malengo ya AfCTA yanaambatana na yale ya WTO, na kiongozi wa kiafrika wa shirika la biashara anaweza kusaidia kuielekeza kuelekea misaada zaidi kwa bara.

Hiyo inaweza kuwa katika kutoa msaada wa kiufundi, uchambuzi wa biashara na utaalam wa sera, na kuleta ndoto ya biasharahuria Afrika kuwa kweli.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani

Lakini kama vile Afrika inaelekea katika mazingira huru ya biashara, matamshi ya ulinzi katika maeneo mengine ya ulimwengu yanaonekana kuongezeka.

Vita vya biashara kati ya Marekani na China, na sera za Rais wa Marekani Donald Trump za kutekeleza mfumo wa kuipa kipau mbele dhidi ya wandani wa kibiashara, almarufu "America First", zinaonekana kugeuza wimbi dhidi ya imani ya biashara huria.

Vikwazo vilivyowekwa kwa sababu ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona pia vimeathiri harakati usafirishaji huduma na bidhaa muhimu kwa wanaozihitaji. Kwa kuongezea, kukataa kwa Marekani kuidhinisha uteuzi au kuteuliwa tena kwa viongozi/ majaji wa WTO wanaosimamia rufaa dhidi ya maamuzi ya shirika hilo, imeiweka katika hali ya sintofahamu. Pia inatishia kudhoofisha WTO kwa jumla.

Ufanisi wa WTO katika kuanzisha sheria mpya za msingi ambazo nchi zote zinaweza kukabiliana pia umekuwa changamoto.

Mnamo mwaka wa 2001, WTO ilizindua mazungumzo yanayoitwa "Mazungumzo ya Doha", ambayo yalitakiwa kkuandaa mipangilio mipya ya kusaidia mataifa yanayoendelea.

Karibia miongo miwili baadaye, mazungumzo yenyewe hayajafua dafu. Huu ndio muktadha ambao kiongozi ajaye wa shirika hili atakayeingia madarakani mnano Novemba mwaka huu atakumbana nao.

Kwa kuzingatia hilo, jukumu la haraka la mkurugenzi mkuu mpya ni kuimarisha WTO na kurudisha imani kwa shirika. Itahitajika mtu aliyeamua bila kujali ni wapi wanatoka.

Ikiwa mmoja wa waafrika watatu atafanikiwa katika kinyang'anyiro cha kuwa bosi wa WTO basi juhudi za kulisaidia bara zinaweza kutumbukia nyongo iwapo atashindwa kuimarisha shirika hili.