Wanawake wajitosa kwenye sekta ya madini na kuondoa dhana kwamba ni ya wanaume pekee

Wanawake wajitosa kwenye sekta ya madini na kuondoa dhana kwamba ni ya wanaume pekee

Mgodi wa kwanza Afrika unaoendeshwa na wanawake pekee. Wanawake kutoka kijiji cha Karoi, nchini Zimbabwe, wamejitosa katika sekta ya madini. Kulingana na Kituo cha Uzalishaji Madini Afrika, takriban asilimia 40 hadi 50 ya wanawake Afrika wanajitahidi kuvunja dhana ya kwamba sekta hiyo ni ya wanaume pekee kwa kujiunga na sekta ndogo ndogo za madini.