Virusi vya corona: Changamoto ya kumuuguza mama wakati wa corona

Virusi vya corona: Changamoto ya kumuuguza mama wakati wa corona

Janga la Covid-19 limesababisha changamoto chungu nzima kote duniani. Lakini Sam Loko - 26, ambaye hana ajira anaishi katika kitongoji duni cha Mathare huko Nairobi nchini Kenya, anamuuguza mama yake mwenye maradhi ambayo yamekuwa vigumu kutibika hasa wakati huu wa janga la corona. Mama yake ana matatizo ya shinikizo la juu la damu, kiharusi pamoja na kupoteza fahamu na janga la corona.