Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Sababu zilizopelekea ACT-Wazalendo kubadili msimamo wao

Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Sababu zilizopelekea ACT-Wazalendo kubadili msimamo wao

Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ameapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Hatua hiyo imefanyika kama sehemu ya makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kufanya kazi baada ya uchaguzi wa 2010.

Shughuli hiyo mbali na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali pia walikuwepo viongozi waandamizi wa ACT-Wazalendo akiwamo kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, katibu mkuu, Ado Shaibu na naibu wake, Nassor Ahmed Mazrui pamoja na makamu mwenyekiti- Zanzibar , Juma Duni Haji.

Zuhura Yunus alizungumza na Maalim, mwanzo akimwuuliza licha ya kutokubaliana na uchaguzi mkuu, kwanini wamebadili msimamo na kukubali kujiunga kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.