Utamaduni wa ajabu wa jamii ya Hadzabe, Tanzania

Utamaduni wa ajabu wa jamii ya Hadzabe, Tanzania

Imezoeleka kwenye jamii nyingi barani Afrika ni wajibu wa msingi kwa wanaume kujenga nyumba lakini kwa jamii ya Hadzabe nchini Tanzania mambo ni tofauti kwasababu kujenga nyumba ni wajibu wa wanawake na wasichana.

Yaani mama hushirikiana na mabinti zake na ni wajibu wao kukusanya miti na nyasi na kujenga nyumba na hukuna kushirikiana na kaya nyingine.

Kila mmoja na familia yake na iwapo binti ataolewa basi mama yake na mama mkwe wake watashirikiana kuwajengea wanandoa hao wapya nyumba yao ya kwanza.

Eagan Salla ametuandalia taarifa ifuatayo...