Simulizi ya kuogofya ya mwanamke aliyemchoma moto mpenzi wake

Chdinma sitting room as fire catch am
Maelezo ya picha,

Nyumba iliyoteketezwa Nigeria kwasababu ya mgogoro wa kimapenzi

Hebu fikiria umelala na mpenzi wako ukiwa umemuegemea, ambaye kabla ya kulala mlikuwa na furaha tu na ghafla unaamka na kujikuta umeungua.

Mwishoni mwa juma hili, jijini Dar es Salaam tuhuma za mwanamke kuchoma moto nyumba kwasababu ya mapenzi zazua taharuki kubwa haswa baada ya mpenzi wake kufariki akiwa ndani.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam imethibitisha kumshikilia Grace Mushi mwenye umri wa miaka 25 kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake Hamisi Abdalla maarufu kwa jina Zungu.

Kamanda wa Kanda hiyo Muliro Jumanne alisema majira ya saa nane na nusu usiku, Julai 16, 2021, Grace anadaiwa kummwagia petroli mpenzi wake na kisha kuwasha moto na hivyo kupelekea Hamis Kufariki.

Uchunguzi wa awali umedai kuwa walikuwa na mgogoro wa kimapenzi.

"mtuhumiwa aliamka usiku na kumfungia ndani Khamis kisha kumwaga petroli na kuichoma moto nyumba hiyo kitendo kilichosababisha kifo cha mwanaume huyo".

Tukio la aina hiyohyo lilitokea nchini Nigeria la mwanamke kumchoma mpenzi wake kwa mafuta ya Petroli.

Simulizi ya kuogofya iliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu kwa kijana mmoja kwa jina Elvis Chidinma Omah, mtaalamu wa madawa huko mjini Makurdi, katika jimbo la Benue , katikati magharibi mwa Nigeria.

Elvis Chidinma Omah na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 17-alikuwa katika mahusiano ya mapenzi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kila siku penzi lao lilikuwa linakuwa na walihaidiana kuishi pamoja milele, walihaidiana kuoana na kifo ndicho kitakachowatenganisha.

Lakini msichana alianza kukosa matumaini hayo baada ya rafiki yake kumwambia amemuona mchumba wake akipeleka zawadi za harusi kwa msichana mwingine kijijini.

Ingawa Omah alikanusha madai hayo , ila mpenzi wake hakuwa ameridhika na maelezo yake na lengo lake likawa ni kuvunja uhusiano wao kwa kuchoma moto nyumba.

Nyumba iliyochomwa kwasababu ya hasira za mapenzi

Maelezo ya picha,

Nyumba ya Chidinma iliyounguzwa na Esther

Omah alimpenda msichana huyo aliyekuwa nae katika mahusiano kwa kipindi kinachokaribia miaka mitatu.

Msichana huyo aliwaambia polisi kuwa mwanaume huyo alimpa ahadi nyingi ikiwemo ya kumuoa, na kila kila kitu kilikuwa kinaendelea vizuri mara ghafla mwanaume akaanza kubadilisha mawazo.

Alipopata ujauzito wake, anasema Chidinma Omah alianza kubadilika na kuanza kufuatilia wasichana wengine.

Kwasababu ya mapenzi yake na nia ya kumuoa, alijitoa kwa kila kitu.

Baadae akamwambia atoe mimba, akatoa ya kwanza na ya pili alivyoambiwa atoe tena alikasirika sana kuwa wamepoteza mtoto mwingine.

Msichana huyo alikuwa anaanza masomo ya chuo kikuu, wakati alipoombwa na Omah mahusiano yao yawe kama awali.

Alikataa kwenda kwa mwanaume huyo lakini alivyoombwa sana kwenda kumuona, alienda na dumu la mafuta ya petroli na kibiriti siku ya Jumapili na kuficha katika mlango wa nyumba ya Omah.

Maelezo ya picha,

Elvis Chidinma Omah, kabla hajaunguzwa na mpenzi wake

Msichana huyo alipofika alipika chakula kitamu na hakuonesha dalili zozote za kuchukizwa na jambo lolote.

Msichana aliwaambia waandishi kuwa alisubiri apate usingizi na ilipofika majira ya saa nane usiku siku ya Jumatatu, Januari 11, 2021, alichukua petroli a kumimina kwenye chumba chake na kukimbilia kanisani.

Omah aliamka na kupiga kelele, baadhi ya majirani wanaume walimkimbiza hospitali .

Msichana huyo sasa yuko chini ya ulinzi na atapelekwa mahakamani baada ya uchunguzi.

Wiki za hivi karibuni , matukio ya wapenzi kuchomana moto yanaongezeka katika jimbo la Benue.

Nicodemus Nomwange, 40, alijichoma moto yeye na mpenzi wake Shiminenge Pam , na mwanamke mwingine alimchoma moto mpenzi wake huko Gboko.