Tetesi za soka Ulaya Jumanne 02.02.2021:Upamecano, Caleta-Car, Marcelo, Williams, Costa, Zidane

AFC Wimbledon inafikiria kumchukua Emma Hayes - kocha wa timu ya wanawake ya Women's Super League ya Chelsea - kama kocha wa kwanza mwanamke katika timu ya soka ya kulipwa kwa wanaume nchini Uingereza. (Express)
Liverpool ilikuwa na euro milioni 23 kama dau lao wakati inamwania beki wa kati wa Croatia Duje Caleta-Car, 24, kiwango kilichokataliwa na Marseille. (RMC Sport, via Team Talk)
Dayot Upamecano
Mtendaji mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amesema kuwa Liverpool na Chelsea ndiyo timu mbili za Ligi ya Primia ambazo zinashindana naye katika kumsajili mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 22. (Mirror)
Lakini Liverpool imekosa kidogo tu fursa ya kumsajili beki wa kati wa Lyon Marcelo baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kukumbwa na matatizo ya kuwa na majeruhi kulikowafanya kuamua kutomruhusu raia huyo wa Brazil, 33, kuhamia kwingineko. (Sun)
Liverpool ilikataa hatua ya mwisho ya Southampton ya kutaka kumsajili mlinzi wa Wales Neco Williams, 19, kwa mkopo. (Sky Sports, via 90 Min)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City haikuwa na nia ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uhispani Diego Costa kwa uhamisho wa bure licha ya mchezaji huyo aliyekuwa Chelsea, 32, kuhusishwa na tetesi za kutaka kuhamia klabu hiyo. (Mail)
Kiungo wa kati wa Scotland Billy Gilmour, 19, ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Thomas Tuchel cha Chelsea katika kipindi cha nusu msimu baada ya kocha wake mpya kufurahishwa na mchezo wake wakati wa mazoezi. (London Evening Standard)
Chanzo cha picha, EPA
Edin Dzeko
Manchester United haikufikiria kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Roma na timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina Edin Dzeko, 34, ambaye alikuwa mshambuliaji wa Manchester City, wakati wa uhamisho mnamo mwezi Januari licha ya mapendekezo ya vyombo vya habari vya Italia. (Express)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ni lazima ashinde Ligi ya Mabingwa ili awe na uhakika wa kuendelea kuwa kocha wa timu hiyo. (AS)
Manchester United ilitupilia mbali nia ya Southampton, Newcastle na West Ham ya kutaka kumsajili Brandon Williams kwa mkopo ili kuendelea kuwa na mlinzi huyo wa Uingereza, 20, Old Trafford. (Sun)
Kuendelea kujiamini kwa Manchester City katika safu ya kiungo wa kati kumeiwezesha kumruhusu mlinzi wa Uingereza Taylor Harwood-Bellis, 19, kujiunga na Blackburn kwa mkopo. (Manchester Evening News)
Steve Bruce amemuambia Matt Ritchie ajitahidi zaidi baada ya siku ya mwisho ya uhamisho kwa winga huyo wa Scotland, 31, kuelekea Bournemouth kugonga mwamba. (Newcastle Chronicle)
Kiungo wa kati wa Aston Villa, 17, Carney Chukwuemeka anafuatiliwa na Manchester United na Liverpool. (Times, via Birmingham Mail)

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 1.02.2021: Chalobah, Maitland-Niles, Eriksen, Ramos, Upamecano, Ndombele
Leicester iko mbioni kusajili wachezaji wa England, Liverpool inalenga beki wa kati, West Brom inataka kusajili wachezaji wawili, Newcastle inafuatilia kwa karibu makubalino ya mkopo na mengine mengi.