Kwanini wanasayansi wanataka kuwaua 'viboko wa dawa za kulevya?

A hippo seen near Hacienda Napoles in 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Viboko wanne walioletwa na Pablo Escobar waliwekwa katika hifadhi ya binafsi

Pablo Escobar ni jina ambalo limekuwa likijaribiwa kusahaulika huko Colombia kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Mhalifu aliyepata umaarufu mkubwa zaidi, alikuwa muasisi wa mtandao wa dawa za kulevya mnamo 1980 na aliwahi kufahamika kama miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani .

Escobar anakumbukwa pia kwa vurugu alizokuwa akizifanya kwa kuvunja sheria za Colombia, ikiwa ni pamoja na utekaji, kulipua mabomu na mauaji.

Lakini nguli huyo wa biashara ya dawa za kulevya aina ya cocaine anahusishwa na wanasayansi kwa kile wanachokiita bomu la ikiolojia lililowahi kutokea.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ni karibu miaka 30 tangu kifo chake, lakini bado Pablo Escobar ni maarufu nchini Colombia

Kundi la viboko ambao waliletwa na Escobar katika hifadhi binafsi miongo kadhaa iliyopita, na sasa wameongezeka.

Kwa mujibu wa wanasayansi, wanasema viboko hao wapo katika maeneo yote ya taifa hilo katika mto Magdalena.

Katika chapisho la jarida la uhifadhi wa biolojia lililotolewa Januari 17 , linasema kikosi cha wanasayannsi kilidai kuwa kuwapunguza wanyama hao ndio suluhu pekee ya kutunza mazingira.

"Ukweli huko wazi kuwa wanawaonea huruma wanyama hawa, lakini wanasayansi wanapaswa kuwa wakweli tu," Mtaalamu wa biolojia wa Colombia Nataly Castelblanco, mmoja wa waandishi ameiambia BBC.

"Viboko hawa waliletwa Colombia na kama hatutawaua sehemu ya wanyama hao sasa , tukishindwa kuwadhibiti hali itaweza kuwa mbaya ndani ya miaka 10 au 20."

Tatizo la ukuaji

Kuibuka kwa viboko hawa maarufu kama "cocaine hippos" wanajumuishwa moja kwa moja na kuuliwa kwa Pablo Escobar na kikosi cha usalama cha Colombia mwaka 1993.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jumba la Escobar ambalo lilikuwa na sehemu ya kuhifadhia viboko

Baada ya kifo chake, Hacienda Napoles, jumba lake la kifahari lililokuwa na ukubwa wa kilomita 250 Kaskazini Magharibi mwa Colombia katika mji mkuu wa Bogota, lilifungwa na mamlaka.

Waliifunga hifadhi yake binafsi ya wanyama - ingawa baadae ikawa sehemu ya hifadhi maarufu.

Wanyama wakali waliokuepo kwenye hifadhi hiyo binafsi walipelekwa kwenye hifadhi nyigine katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Lakini sio viboko.

"Ilikuwa ni zoezi gumu kuwahamisha kutoka sehemu moja mpaka nyingine, walihofia kuwa wanaweza kufa," Castelblanco alisema.

Badala yake waliendelea kuwatunza walipo.

Kwa miaka kadhaa, wanasayansi wamejaribu kuwahesabu viboko wanaoishi katika mikondo ya maji Colombia'. Wakadiriwa kuwa kati ya 80 mpaka 120.

"Ni eneo ambalo lina viboko wengi zaidi nje ya Afrika, ambao wapo katika eneo ambalo si asili yao " mtaalamu wa wanyama na hifadhi Carlos Valderrama ameielezea BBC.

Na namba inakadiriwa kuwa kubwa zaidi.

Mapema mwaka 2034, kama hawatapunguzwa watafikia idadi ya zaidi 1,400 kwa ujumla wao wa kike na wakiume.

Katika utafiti huo, kama wanyama hao watauliwa 30 kila mwaka basi hatari itapungua.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Makazi ya Pablo Escobar yalikuwa ya kifahari

Lakini viboko hawa wamekuwa tatizo?

Castelblanco anaeleza kuwa 'viboko wa dawa za kulevya' wapo katika eneo ambalo si asili yao.

Wanyama hawa asili yake sio Kusini mwa Amerika - na hawana utaratibu kama wa wanyama wengine wa kuwauwa watoto wao wenyewe kama ilivyo kwa wanyama kama simba au mamba.

Hii ina maanisha kuwa viboko hao wanazaliana sana.

Ongezeko la idadi yao na ukuaji wao huwa inategemea hali ya hewa, kama barani Afrika, ni rahisi kudhibitiwa na ukame jambo ambalo halipo Colombia.

Vilevile mazingira ya Amerika ya Kusini yanawafanya wakue kwa haraka .

"Utafiti unaonyesha viboko hawa wanazaa katika umri mdogo tofauti na viboko waliopo Afrika," Castelblanco alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kama hawatapunguzwa watafikia idadi ya zaidi 1,400 ifikapo 2034

Utafiti wa wanasayansi umegundua kuwa kuna athari za mazingira zinazoaminika kutokea kutokana na uwepo wa viboko hao.

"Viboko hao walioenea katika mito yote ya Colombia, katika maeneo ambayo maelfu ya watu wanaishi ," mtaalamu wa biolojia ameeleza.

'Uwepo wao ni kama filamu'

Castelblanco na wenzie sio wanasayansi wa kwanza kupendekeza kupuguzwa kwa viboko hao, lakini ikumbukwe pia kuna wale wanaopinga wazo hilo la kuwaua viboko hao.

Enrique Ordoñez, mtaalamu wa biologia chuo kikuu cha Colombia, alisema viboko hao wa "dawa za kulevya" wanaleta matumaini duniani katika idadi ya viboko waliopo .

Ni vyema kufanya mpango wa kuuawa bakteria kama njia ya kupunguza idadi yao .

Chanzo cha picha, Courtesy of Carlos Valderrama

Maelezo ya picha,

Viboko hao ni wakali

Lakini utaratibu huo sio rahisi na una gharama kubwa.

Mwaka 2009, walifanya zoezi hilo la kwa 'viboko wa dawa za kulevya' wa kiume kama sehemu ya utafiti ili kuona namna watakavyoweza kupunguza idadi ya viboko hao.

"Tunaongelea mnyama ambaye anaweza kuwa na uzito wa tani tano na mkali sana ," Valderrama alisema.

Somo pekee ambalo tulikutana nalo ni kuua vijidudu pekee silo suluhu haswa ukizingatia gharama yake.

"Viboko wengi wanaishi porini . Si rahisi kuwapata wote kiurahisi."

"Wakati huohuo wakiwa bado wanazaliana. Na kiboko wa kiume anazaa na wa kike zaidi ya mmoja ," Valderrama aliongeza.

Tishio la vifo

Ni jambo gani linaizua mamlaka kuchukua hatua kwa haraka?Jibu rahisi ni maoni ya umma.

Watu wanawapenda hao "viboko wa dawa za kulevya ", Nataly Castelblanco ameelezea mtazamo wako.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raia wengi wa Colombia wanapinga uamuzi huo wa kuwaua "cocaine hippos"

"Ni kawaida kwa binadamu kupinga mauaji ya wanyama kwa kuwa huwa wanavutiwa nao." Familia nyingi huwa zinaenda kuwaangalia.

Lakini ukiachilia mbali suala la mazingira, viboko si wanyama rafiki kabisa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwaka jana vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa mkulima mmoja alijeruhiwa vibaya na kiboko karibu Hacienda Napole.

Viboko ni miongoni mwa wanyama wanaojitokeza katika orodha ya wanyama hatari zaidi duniani, mwaka 2016 iliripoti kuwa viboko wanaua watu wapatao 500 kila mwaka barani Afrika.

Lakini hakuna nchini Colombia hakuna kesi ya binadamu kuuliwa na kiboko,ingawa mwaka jana vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa mkulima mmoja alijeruhiwa vibaya na kiboko karibu Hacienda Napole.

"Mpaka sasa bado viboko wanaishi vizuri Colombia licha ya kutolewa wito wa kupunguzwa"

Ni miaka takribani 30 baada ya kifo cha Pablo Escobar, "Viboko wa dawa za kulevya" pia wanawakilisha uwepo wa nguli wa biashara ya dawa za kulevya nchini Colombia.