Upungufu wa nguvu za kiume na athari za matumizi ya mitishamba isiyoidhinishwa kisayansi
Baadhi ya wataalamu wa afya nchini Tanzania wanakiri kuwepo kwa ongezeko la watu wenye matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume.
Hali hii imeelezwa kuwa chanzo cha baadhi ya watu kuamua kutumia dawa za kisasa na hata za mitishamba ambazo mara nyingi zinakuwa hazijafanyiwa utafiti wa kutosha, hivyo kutotibu tatizo.
Utafiti uliofanywa mwaka 2016 na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, unaonesha takriban mwanaume mmoja kati ya wanne ana tatizo la nguvu za kiume.
Utafiti huo ulifanyika kwa wanaume elfu kumi na nane mia nne arobaini na mmoja (18,441) huku umri wa waliochunguzwa ni miaka 47.
Mwandishi wetu Aboubakar Famau amefanya mahojiano na daktari bingwa wa mfumo wa mkojo, Remigius Rugakingira kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijiji Dodoma na kwanza alimuuliza nini hasa maana ya upungufu wa nguvu za kiume?