COP26: Tunastahili kupunguza ulaji wa nyama?

d

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkutano wa COP26 unaendelea huko Glasgow - moja ya mikutano mikubwa zaidi ya dunia kuwahi kuandaliwa kuhusu njia za kuzuia kuongezeka joto duniani. Nyama inatajwa katika moja ya maswali yanayojibiwa kwenye makala haya. Pamoja na suala hilo la nyama, Mwandishi wa BBC wa Reality Check, Chris Morris na mwandishi wa mazingira Matt McGrtah wanajibu baadhi ya maswali yako.

Kwa nini tusiwe na mfuko wa kimataifa kusaidia nchi maskini kufikia sifuri katika uzalishaji wa hewa chafu? Robert Patterson, Darlington.

Chris Morris anajibu:

Hii ni sehemu ya mjadala ulio sasa kuhusu ufadhili katika masuala ya hali ya hewa. Mwaka 2009, nchi tajiri zilisema zitatoa dola bilioni 100 kila mwaka kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2022. Lakini hazijatimiza ahadi zao na sasa zinadai kuwa zitafikia ahadi hiyo ifikapo mwaka 2023.

Nchi maskini zinahitaji pesa hizo kusaidia kutatua athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinazokabiliana nayo kwa sasa. Lakini pia zinahitaji pesa hizo kuhakisha kuwa uchumi wao unatumia nishati safi wakati zinaendelea kukua.

Kama ni watu wanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa kipi kinafanyika kuzuia kuongezeka kwa watu? Gaye Schmidt, Perth, Australia

Chris Morris anajibu:

Kuongezeka kwa watu hakusababishi mabadiliko ya hali ya hewa. Lakini ni uzalishaji mkubwa wa hewa chafu ambazo zinachania kuongezeka joto duniani. Na watu matajiri zaidi duniani ambao ni asilimia kumi huchangia huzalishaji wa hewa chafu kuliko watu maskini duniani ambao ni asilimia 50.

Kuna ukweli kusema kuwa idadi ya watu haitazidi kuongezeka duniani kwa sababu raslimali zinazidi kupungua. Lakini matumizi makubwa yamechangia mabadiliko ya hali ya hewa kuliko idadi ya watu inayoongezeka duniani.

Uwekaji viwango vya ulaji nyama na usafiri wa ndege waweza kuleta ufanisi? kutoka, Geneva

Chris Morris anajibu:

Ulaji nyama hasa nyama ya ng'ombe, kusafiri kwa ndege vina athari kwa mazingira.

Ulaji wa hamburger mbili kwa wiki kwa mwaka huzalisha kiwango cha hewa chafu sawa na kitokanacho na kuweka joto kwa nyumba moja nchini Uingereza kwa siku 95. Na safari ya ndege kutoka London hadi New York na kurudi huzalisa karibu tani 0.67 ya hewa ya kaboni. Hiyo ni asilimia 11 ya hewa anayozalisha mtu anayeishi nchini Uingereza kwa mwaka.

Kinadharia sheria kwa ulaji nyama au usafiri kwa ndege zinaweza kuleta mabadiliko lakini hakuna uungwaji mkono wa hilo kufanyika. Nchini Uingereza kamati ya mabadiliko ya hali ya hewa inayoishauri serikali imependekeza kuwa watu wanastahili kupunguza ulaji nyama kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2030 na asilimia 35 ifikapo mwaka 2050.

Utumiaji wa kodi kufanya bidhaa zingine kuwa ghali itakuwa njia bora zaidi kuliko kutumia sheria.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuna manufaa yoyote yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa? Mike Bell, Germany

Matt McGrath anajibu:

Huenda kuna baadhi ya manufaa yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa, lakini wanasayansi wa masuala ya hali ya hewa kwa haraka wamekataa kwa sababu yanaelemewa sana na athari mbaya. Manufaa yatayojwa sana ni kwamba dunia yenye viwango vya juu vya kaboni itasababisha mimea kukua kwa haraka na mikubwa. Hii inafahamika kama CO2 fertilisation effect.

Hata hivyo utafiti uliochapishwa mwaka uliopita ulionyesha kuwa hali hii inazidi kupungua na kwamba madai kuwa itapunguza kuongezeka joto siku zinazokuja haiungwi mkono na ushahidi wowote.

Tunaweza kuwa na imani gani kwa mkutano wa COP26 wakati ambapo dunia hata haikushikamana kwenye ugavi kwa chanjo? Mahesh Nalli, London

Matt McGrath anajibu:

Kuna mambo sawa kati ya majanga na mabadiliko ya hali ya hewa lakini kuna tofauti pia. Vile tumeona katika kipindi cha miezi 18, nchi zinaweza kuzuia maambukizi ya Covid kwa kupunguza usafiri wa watu kati ya nchi.

Hatua kama hiyo haitafanikiwa wakati wa kuongezeka viwango vya joto vinavyosababisha athari kwa nchi tajiri na pia maskini.

Wakati ambapo suala la chanjo litasuluhishwa kwa wakati na pesa, suala la mazingira linahitaji mabadiliko ya kila aina katika maisha yetu kuanzia nishati, chakula na mavazi.

Maya Yossifova, Vienna, Austria Kuna athari gani itokanayo na gesi ya methane katika mabadiliko ya hali ya hewa? Maya Yossifova, Vienna, Austria

Matt McGrath anajibu:

Methane ni gesi chafu ambayo huzalishwa kutoka maeneo asilia kama yale yenye maji na pia kutokana na shughuli za binadamu kama kilimo na uchimbaji mafuta. Ni mchanganyiko wa gesi za kaboni na haidrojeni na huzifanya kuwa na uwezo wa kushika joto ambayo ni moja ya sababu kuu za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa mujibu wa shirila la utabiri wa hali ya hewa duniani, viwango vya gesi ya methane angani vilifikia 1,889 kwa kila bilioni mwaka mwaka 2021. Viwango vya gesi ya kaboni ni mara 200 zaidi lakini methane inatajwa kuwa mara 80 zaidi katika kusababisha kuongezeka joto dunaini katika kipindi cha miaka 20.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa mapema mwaka huu ilisema jitihada za kupunguza methane zinastahili kuangazia njia za kupunguza kuvuja gasi hiyo kutoka maeneo kama visima vya gesi, kupunguza utupaji wa chakula, kuboresha uvugaji na kuwashauri watu kutumia lishe yenye kiwango cha chini cha nyama na maziwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mfumo wa kibebari ulio duniani unakinzana na mabadiliko ya hali ya hewa na hitaji la uwepo wa mitindo ya maisha iliyo safi? Andrew, Exeter

Matt McGrath anajibu:

Kulingana na baadhi ya wataalamu, kama vile mwanauchumi Lord Stern , mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuonekana kama kufeli kwa masoko. Hii ni kwa sababu biashara hazigharamii uhabifu ambao zimesababisha kwa mazingira.

Jitihada za kimataifa za kutatua mabadiliko ya hali ya hewa kwa miongo miwili iliyopita imeangazia zaidi katika kuunganisha ubebari na kupunguza ongezeko la joto duniani - kwa mfano kuwawekea gharama kwai gesi ya kaboni na kumfanya mchafuzi alipe kuhakikisha kuwa uzalishaji wake umezuiwa.

Lakini kuna ushahidi kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kuwezesha hatua hizi kufanikiwa.

Mkutano wa COP26 unahitaji watu 25,000? Watazalisha kiwango kikubwa cha CO2 , ni kwa sababu gani mambo mengi yasifanywe kwa njia ya mitandao?

Matt McGrath anajibu:

Janga linaweza kutajwa kama wakati muafaka kwa Umoja wa Mataifa kutumia teknolojia kwa majadiliano, na majaribio yalifanywa wakati wa maandalizi kwa mkutano wa COP mwezi Juni yaliyodumua kwa wiki tatu. Kwa bahati mbaya mambo hayakuenda sawa, changamoto za tofaui ya masaa na teknolojia vilioyesha kuwa haitawezekana.

Kutokana na hilo nchi nyingi zinazoendelea zimesisitiza kuwepo mkutano wa ana kwa ana. Zinahisi kuwa itakuwa rahisi kwa sauti zao kupuuzwa kwa mikutano ya Zoom.

Kuna ushahidi uliopo kuwa hili hufanikiwa. Wakati wa mkutano wa mwaka 2015, uwepo wa nchi za visiwa na nchi zinazokumbwa na matatizo ilichangia kufikiwa makubaliano ya kupunguza viwango vya joto kwa nyuzi joto 1.5 kwenye makubalino ya Paris.