Marufuku ya uvaaji hijabu mahakamani yaondolewa Ubelgiji

mm

Mahakama nchini Ubelgiji imeondoa kikwazo cha kuvaa hijabu mahakamani.

Serikali ya Ubelgiji, ikijibu onyo la Baraza la Mawaziri la Ulaya, imefanya marekebisho ya kifungu cha 759 cha kanuni ya adhabu ya nchi hiyo, inayokataza uvaaji wa hijabu mahakamani.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke ambaye ni Muislamu kuomba kufanya kazi Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu mwaka 2018 na kulazimishwa kuvua hijabu yake, lakini alikataa.

Mahakama ya Strasbourg imeamua kuwa uamuzi wa Ubelgiji kumzuia mwanamke Muislamu kuvaa hijabu mahakamani ni "kukiuka uhuru wa dini".

Majaji pia waliamua kwamba hijabu inaweza kuvaliwa kwa msingi wa "uhuru wa imani".

Baadhi ya majaji wamesema kwamba marufuku hiyo inapaswa kutekelezwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Serikali ya Ubelgiji, kwa kujibu onyo kutoka kwa Baraza la Ulaya, ilirekebisha Kifungu cha 759 cha Kanuni ya Adhabu ya karne ya 19.

Sheria hiyo ilitungwa kipindi ambacho kila mtu nchini Ubelgiji alivaa kofia, ambayo ilimtaka mtu yeyote anayefanya kazi mahakamani kuwa huru, kuwa kimya na kuonesha heshima."

Kelstman, mkurugenzi wa Kituo cha fursa sawa, alisema: "Mabadiliko yamefanyika hatimaye. Tunakaribisha hatua hii kuelekea haki za binadamu."