Wafugaji wanaowakata mbwa masikio ili kuvutia soko katika mitandao ya kijamii

Dogs

Chanzo cha picha, : SONS_OF_ADAM Instagram

Uchunguzi wa BBC umegundua kuwa mitandao ya jamii inawapa msukumo baadhi ya wafugaji kuwakata masikio watoto wa mbwa ili wavutie.

Ukataji huo wa masikio unahusu kuondoa sehemu ya sikio kwa sababu za urembo.

Mfugaji mmoja alimuambia mwandishi wa uchunguzi wa BBC kuwa ukataji huo unaunda muonekano wa kuvutia kwa mbwa huyo aina ya bully.

Ukataji huo ni haramu nchini Uingereza, lakini wafugaji wanatoa paspoti bandia kwa mbwa kuonesha kuwa ulifanywa nchi za ng'ambo.

Wakati wa uchunguzi, mfugaji mmoja alijitolea kumuuzia mwandishi wa habari za uchunguzi kutoka BBC Wales mtoto wa mbwa kwa pauni 13,000, na kuzungumza kuhusu kumkata maskio mbwa huyo, zoezi ambalo limepigwa marufuku nchini Uingereza chini ya sheria ya maslahi ya wanyama.

Paula Boyden kutoka shirika la kutete maslahi ya mbwa anasema kuwa hakuna haki kabisa kwa zoezi hilo na kwamba itaacha mbwa wakiwa na matatizo ya kiafya na tabia.

"Tumeyaona pia matatizo ya kiafya kwa kuwa mbwa huwasiliana kwa kutumia maskioa yao na bila ya maskio hayo wanakumbwa na ugumu wa kufanya hivyo na wamiliki wao au na mbwa wengine."

Chanzo cha picha, Moheiz Adam/SONS_OF_ADAM Instagram

Maelezo ya picha,

Moheiz Adam alimuuzia mwandishi mbwa kwa £13,000

Wachunguzi kutoka BBC Wales waliwawafuatilia wafugaji kadhaa ambao huchapisha picha za mbwa walikatwa masikio katika mitandao ya kijamii.

Mfugaji mmoja Moheiz Adam alisema "ni aibu" kuwa ukataji huo wa masikio ni haramu kwa kuwa unampa mbwa "muonekano wa kuvutia".

Alijitolea kumuuzia mwandishi wa siri mtoto wa mbwa kwa paunia 13,000, akisema atakuwa na paspoti za microchip.

Chanzo cha picha, Hope Rescue

Wakati wa mawasiliano ya simu kwa njia ya video, Bw Adam alimbeba mbwa huyo, na akionesha masikio yake alisema: "hayo yote yatatolewa."

Akizungumza kuhusu ushahidi huo wa BBC, Daniella Dos Santis, rais wa zamani wa chama cha madaktari wa wanyama cha Uingereza alisema alisumbuliwa sana ni kile kilifichuliwa.

"Ukataji maskio ni haramu na haufanywi kwa sababu yoyote ila kwa sababu za muonekano na mjadala wote unahusu vile hawa mbwa wanaonekana, ni kwa hadhi tu. Hakuna manufaa yoyote ya kiafya kwa mbwa hawa ."

Baadaye Bw Adam alisema licha ya kwamba angependa maskio ya mbwa yakatwe, ilikuwa ni haramu na hajawai kupangaa hilo kufanywa".

Chanzo cha picha, Joshua Harty

Mfugaji mwingine Joshua Harty, kutoka Cardiff akimuambia mwandishi wa habari wa uchunguzi kuwa yeye pia anaweza kupanga ukataji huo ufanywa na pia kupatikana kwa pasipoti ya kigeni na microchip.

"Kukatwa masikio na paspoti na chip hugharimu karibu pauni 500…daktari wangu huvipata kutoka Uturuki.

"Nimepeleka mbwa kwa maonyesho huko Ireland, Uhispania, na hivyo lazima nivuke mipaka, na nimebeba paspoti hii na nimekuwa nikipita kila wakati. Sijawai kukumbwa na tatizo," alisema,

Daniella Dos Santos alisema kile Bw Harty alikuwa anapendekeza ni uhalifu," ni haramu kabisa, ukataji maskio, paspoti bandia na kila kitu kuhusu haya ni mfumo haramu, alisema.

"Tena kuwaona wanyama hawa kama bidhaa za kutengeneza pesa badala ya viumbe walio hao."

Alisema sababu ya hili kufanyika ni kwa sababu kuna mwanya unaoruhusu uagizaji wa mbwa waliokatwa masikio.

Picha za mitandao ya kijamii

Chanzo cha picha, Hope Rescue

Vanessa Waddon kutoka shirika la kushughulikia maslahi ya mbwa amekuwa akiwatunza watoto wa mbwa waliokatwa masikio baada ya kuokolewa kutoka kwa mfugaji haramu na baraza la Cardiff.

Mbwa hao walitajwa kuwa wa thamani ya pauni 1,500 zaidi baada ya masikio yao kukatwa.

Bi Waddon anasema nahofu kuwa mahitaji yao yanachochewa na washawishi wa mitandao ya kijamii wanaochapisha picha wakiwa na mbwa waliokatwa maskio, akimtaja mcheza soka Marcus Rahsford, mwanamuziki Leigh-Anne Pinnock na mcheza filamu Jack Fincham.

"Wakati watu hawa mashuhuri wanachapisha picha mitandaoni, watu hufikiri oh yule anaonekana vizuri labda nitapata kama yule," alisema.

Huenda watu watu hao mashuhuri waliwanunua mbwa hao kwa njia halali, kuna watu wanawakata mbwa masikio kinyume na sheria nchini Uingereza ili kutumiza mahitaji.

BBC Wales waliwatafuta wawakilishi wa Bw Rashford, Bi Pinnock na Bw Fincham Lakini hawakupata jibu lolote.

Vizuizi kwa mauzo

Seriklia ya Uingereza imesema mswada wa wanyana wa Kepti utazuia uagizaji wa mbwa waliokatwa maskio na watoto wa mbwa wa umri wa chini ya miezi sita.

Msemaji wa serikali ya Wales alisema wana mpango wa miaka mitano wa kukubaliana na ufugaji haramu kwa mbwa, zikiwemo sheria mpya na kufuatilia maendeleo yake kwa karibu.

Lakini Bi Boyden anasema ikiwa wafanyakazia wa mipakani hawatawakagua mbwa wanaoingizwa, sheria hiyo haitafanya kazi.

Bi Waddon aliongeza: Tunafanya kazi na maafisa bora, Lakini hawana rasilimali za kuchunguza visa vyote ambavyo vimeripotiwa kwao. Unaweza kuwa na sheria bora lakini iwapo haitumiwi haiwezi kamwe kuwa yenye ufanisi.