Fahamu silaha mbili ambazo Urusi imezitegemea kutwa  eneo kubwa mashariki mwa Ukraine

th

Chanzo cha picha, Getty Images

 Urusi imefauku kuuteka mji wa hivi punde mashariki mwa Ukraine wa Lysychansk na kuipa  na kuipa afueni ya kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya Donbas .

Hata hivyo hilo halijawashanfgaza wengi hasa baada ya jeshi la rais Vladmir Putin kuanza kutegemea matumizi ya silaha mbili ambazo zimeipa Ukraine hasara kubwa kupitia mashambulizi makali na yanayosababisha maafa .Moja ni kombora la Kh-22 (X-22) Pamoja na ndege ya kivita inayotumiwa kulirusha Tupolev-22.

Makombora yaliyotumiwa katika mashambulizi ya Urusi katika eneo la Odesa na  kusababisha vifo vya takriban watu 19, akiwemo mtoto mmoja, yalikuwa ya aina sawa na yale yaliyotumiwa dhidi ya jumba la maduka la Kremenchuk  Jumatatu wiki jana  Ukraine imesema.

Wizara ya ulinzi ya Kyiv ilizitaja silaha hizo kuwa ni Kh-22 (X-22) - aina ya kombora la zamani la kusafiri lililotengenezwa miaka ya 1960.

Tulilitazama kombora hilo kwa undani zaidi mapema wiki hii - wachambuzi wa masuala ya ulinzi wanapendekeza matumizi yake yanamaanisha kuwa Moscow inapoteza makombora ya kisasa zaidi.

Yanarushwa kutumia ndege za kivita za  Tupolev-22,  na ni silaha ya masafa ya kati na katika hali yao ya asili hayakuwa sahihi. Kwa miaka mingi mfumo wa mwongozo ungeweza kuboreshwa, lakini hatujui ikiwa hii inatumika kwa silaha zilizofyatuliwa hivi majuzi. 

Moscow inakabiliwa na changamoto na kile inachokiita, mifumo yake ya "usahihi wa juu wa kuzinduliwa kwa hewa". Vikwazo vinamaanisha ugavi wa vifaa  vilivyoagizwa umekauka. Na injini zinazoendesha baadhi ya makombora zilitengenezwa hapo awali huko Ukraine, kwenye mtambo mmoja katika mkoa wa Kharkiv.

Sehemu ya tatizo kwa Ukraine ni kwamba makombora mara nyingi hurushwa ndani ya eneo la Urusi, huku ndege zikiwa ndani ya mwavuli wa ulinzi wa anga wa Urusi.

Hii inafanya makombora kuwa magumu kunaswa , hivyo basi haja ya Ukraine kuwa na ulinzi bora wa anga ili kukabiliana nayo.

Hilo litatokea hivi karibuni.

Wiki jana , Rais wa Marekani Joe Biden alisema mifumo ya ulinzi wa anga ya Magharibi itatolewa kwa Ukraine kama sehemu ya kifurushi kipya cha msaada cha Marekani cha $800m (£665m).

Unaweza pia kusoma

Sifa  kuu za Kh-22

Hili ni kombora la masafa ya kati lililotengenezwa katika enzi ya Vita Baridi vya miaka ya 1960, awali ili kushambulia meli kubwa za kivita.

Pia kulikuwa na aina nyingine ya kufanya  mashambulizi ya ardhini, lakini katika siku hizo ilikuwa na  vifaa vya vita vya nyuklia. Makombora kama hayo sasa yanaweza kuwekwa vichwa vya kawaida makombora .

Silaha  yenyewe ni kubwa, imejaa kioevu, ni ya hali ya  juu sana - lakini, haswa, sio sahihi kwa viwango vya leo.

Data yoyote ya eneo lengwa itawekwa kabla ya kuzinduliwa, badala ya "kurusha". Asili ya kina kidogo ya pembe ya athari ya kombora hili inaashiria zaidi asili yake ya kusafiri, badala ya kombora la balistiki, ambalo hufuata njia ya kimfano.

 

Kombora hilo lilizinduliwaje?

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Matokeo ya shambulio la kombora huko Kremenchuk

Saa chache baada ya shambulio la Jumatatu, Kamandi ya Jeshi la Anga la Ukraine ilitoa maelezo ya jinsi shambulizi hilo lilivyotekelezwa .

Kh-22 zilirushwa kutoka kwa ndege za  Tupolev katika eneo la Kursk magharibi mwa Urusi, takriban kilomita 300 (maili 185) kutoka eneo la shambulio .

Hii ni sehemu ya mtindo unaojulikana katika vita hivi, ambapo ndege za Urusi hurusha makombora ndani ya eneo la ulinzi la eneo la Urusi, kwa kutumia safu ya makombora ya kupaa kufikia shabaha zilizo umbali wa mamia ya maili.

Mwishoni mwa juma, ndege za  Urusi pia zilirusha makombora ya kasi huko Kyiv kutoka Bahari ya Caspian - umbali wa maili 900. Mashambulizi sawa na hayo yalizinduliwa kutoka eneo moja dhidi ya Odesa mwezi Aprili.