Kutupeleka Rwanda haukutuzuia kufika Ulaya

Mengesha

Chanzo cha picha, BBC / DERRICK EVANS

Maelezo ya picha,

Bahabelom Mengesha, ambaye kwa sasa anaishi Zurich, alipelekwa Rwanda na Israel mwaka 2014

Huku Uingereza ikiendelea na mpango wake wa kuwatuma waombaji wa uhamiaji nchini Rwanda, BBC imesikia Ushahidi kwamba, mwaka 2017, wakimbizi waliopelekwa huko na Israel   waliondolewa haraka na sasa wako Ulaya. 

Bahabelom Mengesha, mwenye umri wa miaka 36 Mueritrea, anafahamu  fika hali halisi ya kupelekwa Rwanda nan chi nyingine. :Lakini kuishi kwake pale kama mkimbizi kulikuwa ni kwa kipindi kifupi. 

Alikuwa ameondoka Eritrea kutoroka vita mwak 20o7 na kuhamia Israeli kuomba uhamiaji. Miaka saba baadaye, alipokonywa hati yake ya uhamiaji na aliambiwa achaguwe kurejeshwa nyumbani , kwenda katia mahabusu ya wahamiaji au achukue dola 3,500 na kuwekwa kwenye ndege ya safari moja kuelekea Rwanda.  

Nilihisi kwamba sikuwa na chaguo lolote, aliiambia BBC, kutoka Uswidi, ambako amekuwa akiishi kwa miaka saba iliyopita.

 "Hakuna mtu ambaye angeweza kujitolea kwenda gerezani," anasema Bahabelom . "Kurusi Eritrea, ambako kufungwa ni sehemu ya utamaduni, pia hili haliwa chaguo."

 Kwahiyo alichagua Rwanda.

 Lakini muda mfupi Bahabelom  alibaini kuwa hakuwa nakaribishwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki . Mara baada ya kuwasili katika mji mkuu , Kigali aliambiwa kuwa ni lazima aondoke tena kuelekea nchi jirani ya Uganda – na kwa bila garama.

 Haikuwa wazi ni nani aliyekuwa anapanga kufukuzwa kwake Rwanda-na kufukuzwa kwa wahamiaji wengine tuliozungumza nao- lakini Bahabelomanaamini maafisa wa Rwanda walihusika.

 Hadhi ya Rwanda kama mahali salama kwa wakimbizi imekuwa ikihojiwa, baada ya Uingereza kusaini mkataba na nchi hiyo kuwahifadhi wanaomba uhamiaji waliowasili kwenye fukwe zake. Mataifa ya magharibi yametoa onyo kuhusu rekodi ya haki za binadamu. 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Serikali ya Uingereza ilikuwa tayari imeandaa ndege ya kuwapeleka waombaji uhamiaji Rwanda mapema mwezi huu

Hatahivyo, kulikuwa na tofauti muhimu baina ya mkataba wa Uingereza nan chi hiyo na ule wa Israeli. 

 Mpango wa Israeli wa kuondoka’’kwa hiari’’ulitoa ndege ya kwenda Rwanda iwapo mtu angechagua kwenda, lakini mpango wa Uingereza ni  wa lazima .  Na tofauti na Uingereza , ambayo ilitangaza mpango huo wazi kwa umma, Israeli haikuwa na makubaliano  yoyote rasmi na Rwanda.

 Lakini waomba uhamiaji Waeritrea na Wasudan wapatao  4,000   waliokuwa  Israel walipelekwa Rwand ana Uganda kati ya mwaka 2013 na 2018, kabla mpango huo wa siri kusitishwa. 

 Bahabelom alisafirishwa kwa ndege hadi  Kigali Septemba 2014.

 "Kutumwa Rwanda haikutuzuwia kufika Ulaya," anasema, akielezea jinsi walivyokwenda kutoka Rwanda hadi Uganda.  "Na hatukukomea pale."

  BBC imezungumza na waomba uhamiaji kadhaa ambao walipelekwa Rwanda kutoka Israel. Wote walishiriki katika mpango wa kati yam waka 2014 na 2016 na sasa wanaishi Ulaya.Kando na hao walau tunafahamu mhamiaji mmoja ambaye anaishi ndini Uingereza. Wengine waliohojiwa na wataalamu wa uhamiaji wametoa maelezo yanayofanana.  

 Wengi walizungumzia kukutana na mwanaume mmoja kwenye uwanja wa ndege wa Kigali anayeitwa ‘’John’’. Ushahidi huu ni wa miaka kadhaa kwahivyo haiwezekani kuuthibitisha iwapo John alikuwa ni yule yule kwa miaka yote.

 Walielezea kuwa wakati huo nyaraka zao zilichukuliwa na watu walioonekana kuwa maafisa wa Rwanda, kabla ya kuchukuliwa kwa gari hadi katika hoteli ambayo ilikuwa na walinzi na ambapo walizuiwa kuondoka.  

 Wakati huo waliambiwa walipe had idola 500 ili wasafirishwe katika makundi hadi kwenye mpaka wa Uganda.

 Magari yalikuwa yanawasubiri upande wa pili wa mpaka wa Uganda kwa ajili ya kuwasafirisha hadi Kampala. Pia ilibidi walipie garama ya nauli. 

 Lakini hawakuwa na kazi au nyaraka , ambazo wanasema wahitaji kutumia kuendelea kusafiri- kujiunga walisema wanahitaji kuendelea kusafiri ili kujiunga na njia maarufu wanazotumia wahamiaji kutoka Afrika na Mediterranean kufika Ulaya.

 Bahabelom anasema hakuhisi kuwa angechagua kuishi nchini Rwanda.

  "Wakati unapoaambiwa kulipa hii na uende, bila shaka utafanya kile ulichoambiwa  ."

Mwombaji mwingine wa uhamiaji kutoka Eritrea, Mebrahtom Tesfamichael, anasema alimuuliza "John" kuhusu kile kinachoendelea.

Chanzo cha picha, BBC / DERRICK EVANS

Maelezo ya picha,

Mebrahtom Tesfamichael anasema alijaribu kugundua ni kwanini walikuwa wanasukumwa nje ya nchi   

"Nilikuwa na mazungumzo ya faragha naye…" anasema  Mebrahtom, ambaye pia aliwasili Kigali mwaka 2014 baada ya kuishi miezi tisa katika kituo cha mahabusu cha nchini Holot Israel . "'Lazima utoke hapa,' alisema. Nilijibu 'Kwanini tuondoke? Wakati tulipoondoka Israeli, walituambia tunapata hadhi ya ukimbizi nchini Rwanda na huko ndiko tnapoenda kuishi.' Alisema tu kwamba ' Labda unaruhusiwa kukaa kwa siku tatu. Baada ya hapo lazima uwe umeondoka.'"

Tesfay Gush, raia wa  Eritrean ambaye  aliwasili Rwanda Februari 2015, anaamini kuwa maafisa wa Rwanda na wasafirishaji wa binadamu walikuwa wanashirikiana  the Rwandan officials and traffickers were working in tandem na ushirikiano.

"Kama mwanaume wa Kiafrika binafsi nilifikiri ningetendewa haki, na kuhudumiwa  [katika Rwanda]," anasema. Lakini aligundua kuwa hakukaribishwa wakati alipshuhudia kuwa maafisa wa usalama na raia wanafanya kazi pamoja 

"Hawakututaka sisi pale."

"Kwa kawaid wakati mtu fulani anapokusaidia katika kuvuka mpaka huwa inafanyika kwa siri, lakini watu hawa walifanya hili wazi. Kwa mfano wakati tulipofika kweye vituo vya ukaguzi na kuwasilisha nyaraka tulipita bila kuzuiwa. Ndio maana ninadhani walikuwa ni maafisa."

Ilipoombwa kuzungumza, serikali ya Rwanda ilisema kuwa haifahamu kuhusu madai ya aina hiyo. Msemaji alisema serikli itachunguza madai hayo. 

"Yoyote atakayebainika kuvunja sheria zetu za viwango vya maadili atawajibishwa. Serikali ya Rwanda inashugulikia usalama wa watu wake, na yeyote anayekuja nchini mwetu, ni kipaumbele cha kwanza, na hao ni pamoja na wakimbizi na wahamiaji wa kiuchumi."

Ahadi hewa

Bahabelom hatimaye aliwasili Ugiriki katika boti dogo na akasafiri kwa njia ya barabara hadi Uswidi. Sasa anaishi mjini  Zurich, anakaribia kufanya mtihani wa amwisho ili kuwa fundi wa mabomba aliyesomea. Anahisi mwenye bahati akijilinganishwa na wengine waliopelekwa na Israeli nchini Rwanda ambao pia walijiunga na safari ya wahamiaji kuelekea Ulaya.

 "Ninawafahamu walau watu 10 au zaidi ambao walipoteza maisha yao nchini Libya, ambao walikatwa vichwa  na Daesh [Kikundi cha Islamic State],au kuzama baharini ."

Mtaalamu mmoja wa mpango wa Israeli, Dkt Yotam Gidrom, anasema wakati taarifa ya mpango wa kuhamishwa kwa wahamiaji uliposambaa katia jamii za wahamiaji, zilitambuliwa njia za kujiunga na njia ya usafirishaji haramu wa wahamiaji ya kwenda Ulaya. 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kulikuwa na maandamano ya umma nchini Israeli wakati serikali ilipojaribu kuifanya rasmi sera ya kuwarejesha nyumbani wahamiaji kuwa

Wataalamu wanaonya kwamba kuwapeleka katika nchi ya tatu watu kunaweza kuwafanya wawe katika hatari zaidi ya kutendewa vibaya na wasafirishaji haramu wa binadamu.

 "Hatari za kuwafukuza watu wanaotafuta uhamiaji…na kuwapeleka katika nchi ambazo hawazifahamu na ambazo huenda hazina mawasiliano n ani hatari ," Steve Symonds, wa  Amnesty International, aliiambia BBC.

 Mfumo wa serikali ya Uingereza wa wakimbizi wa Rwanda, ni wanajaribio wa miaka mitano unaolenga kuwapeleka baadhi ya wahamiaji kwa ajili ya kufanya mchakato na kuishi huko kwa muda mrefu.  

 Serikali ya Rwanda ilisema kuwa makubaliano na Uingereza  "hayawezi kulinganishwa kabisa"na mpango wa Israeli ambao "ulisitishwa wakati ilipokuwa wazi kuwa haukuweza kufanya kazi".

 "Chini ya mpango mpya, kutakuwa na usaidizi kwa ajili ya wahamiaji na nchi inayowapokea, unaogaramiwa  kifedha na serikali ya Uingereza," ilisema.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza inasisitiza kuwa utekelezwaji wake utasimamiwa kwa karibu. 

 "Ushirikiano wetu wa kidumia na wenye ubunifu na Rwanda utafuatiliwa kupitia kamati ya pamoja, ambayo itahakikisha wale wanaofanya safari hatari kuelekea Uingereza wanahamishiwa Rwanda kujenga upya maisha yao pale," msemaji aliiambia BBC.