Jinsi Urusi 'ilivyoishinda' Ukraine barani Afrika

A supporter of Malian Interim President wears a face mask of the President of Russia, Vladimir Putin, during a pro-Junta and pro-Russia rally in Bamako on May 13, 2022

Chanzo cha picha, Getty Images

Hotuba ya Rais wa Ukraine kwa makongamano na mabunge ya kitaifa duniani imekuwa sehemu ya kalenda ya kidiplomasia katika miezi michache iliyopita.

Lakini alipozungumza na Muungano wa Afrika (AU) siku ya Jumatatu ni wakuu wanne wa nchi pekee kutoka barani Afrika waliojiunga na mkutano huo mtandaoni, huku wengine wakiwakilishwa na wadogo wao au maafisa wa serikali.

Hatua hiyo ilikuwa dalili ya mapambano yasiyo sawa ambayo Kyiv inakabiliana nayo katika juhudi za kuwasilisha ujumbe wake katika bara la nchi 54 ambapo ina balozi 10 tu - robo tu ya uwepo wa Urusi.

Katika juhudi za kujaribu kubadili mitazamo ya Afrika kuhusu uvamizi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin,Bw Zelensky hawezi kutumia nguvu za kisiasa au kiusalama ikulinganishwa na za Moscow.Ukraine haina nguvu ya kijeshi duniani na si mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kama Urusi.

Kutokana na hili, viongozi wengi wa Kiafrika wamehitimisha kuwa hawawezi kuiga makabiliano ya moja kwa moja kati ya nchi za Magharibi na Moscow.

Hiyo ndiyo hali hasa sasa kwamba kuziba kwa usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kunachangia katika mgogoro mkubwa wa chakula tayari, unaoendesha bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na kuhatarisha mtiririko wa ngano, nafaka nyingine na mafuta ya kupikia kwa nchi za Kiafrika ambazo hazijitegemei vya kutosha.

Mapema mwezi huu Rais wa Senegal Macky Sall, mkuu wa sasa wa AU, alisafiri kwa ndege hadi kituo cha mapumziko cha Bahari Nyeusi huko Sochi nchini Urusi kujadiliana na Bw Putin jinsi ya kuondoa vikwazo vinavyozuia uuzaji wa chakula unaohitajika sana kutoka Urusi na Ukraine.

Hiyo ndiyo hali inayoshuhudiwa baada ya kuzibwa kwa usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kuchangia katika mgogoro mkubwa wa chakula, ambao umefanya bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kama vile ngano, nafaka nyingine na mafuta ya kupikia kwa nchi za Kiafrika kuongezeka.

Na wiki iliyopita Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alimpigia simu Bw. Putin kujadili jinsi bidhaa za kilimo na mbolea kutoka Urusi zinaweza kusafirishwa Afrika.

Mazungumza hayo yalizaa matunda kidogo ijapokuwa hayakuwa mafanikio madhubuti.

Maelezo ya picha,

Mnara wa ukumbusho wa jeshi la Urusi umewekwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wakati huo huo, kuna baadhi ya vidokezo vinavyoashiria kwamba uvamizi wa Ukraine unaweza kuleta matatizo katika ushiriki wa kijeshi wa Urusi barani Afrika, huku uvumi ambao haujathibitishwa wa baadhi ya wanajeshi wa kundi la mamluki la Wagner wakiamriwa nyumbani kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Hilo halitashangaza, kwa kuzingatia matakwa ya kampeni kali ya kijeshi katika eneo muhimu la Donbas.

Hata hivyo, hakuna dalili ya kupungua kwa uwepo wa Wagner nchini Mali - ambapo wapiganaji wake wameonekana mara kwa mara kwenye operesheni ya pamoja na vikosi vya kitaifa.

Muktadha mpya wa kimataifa wa kushangaza

Zaidi ya hayo, mikataba rasmi ya usalama na kijeshi ya Urusi barani Afrika inaimarishwa, licha ya mahitaji ya vita vya Ukraine.

Cameroon imekuwa shabaha ya hivi punde ya uvamizi huu. Waziri wa Ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo alikuwa mjini Moscow mwezi uliopita kuungana.

Waziri wa Ulinzi wa Cameroon Joseph Beti Assomo alikuwa mjini Moscow mwezi uliopita kuungana na mwenzake wa Urusi Sergei Shoigu kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi wa miaka mitano.

Makubaliano hayo yanajumuisha intelijesia, mafunzo na utaalam wa kushiriki katika kukabiliana na ugaidi na uharamia wa baharini. Mazoezi ya pamoja yanapangwa.

Hati hiyo haitaji chochote kuhusu usafirishaji wa silaha lakini inadokeza kuwa njia za ziada za ushirikiano bado zinaweza kukubaliwa.

Mpango wa mwaka 2015 ulikuwa tayari umetoa msaada wa Urusi wa silaha na vifaa vya anga - muhimu kwa mapambano dhidi ya wanajihadi katika eneo la Fari kaskazini mwa Cameroon.

Ijapokuwa makubaliano mapya na Moscow si maalum sana, inaonekana kuzua wasiwasi katika miji mikuu ya nchi za Magharibi.

Ndani ya wiki chache mkurugenzi wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa barani Afrika, Christophe Bigot, alisafiri kwa ndege hadi Yaoundé, akionekana kumhakikishia Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute kwamba Paris pia itaendelea kujitolea katika ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni na kupambana na ugaidi.

Maelezo ya picha,

Cameroon inapambana na uasi wa watu wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga na wanamgambo wa Kiislamu.

Makubaliano na Cameroon yalitiwa saini dhidi ya muktadha mpya wa kimataifa wa kushangaza - uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine.

Viongozi wa Magharibi sasa wanaichukulia Urusi kama tishio kuu la usalama, wakipinga misingi ya demokrasia na mfumo wa kimataifa unaozingatia sheria.

Hata hivyo, baadhi ya serikali za Afrika zinasitasita kukubaliana na mtazamo huu mbaya wa utawala wa Putin. Na hiyo haitumiki tu kwa zile kama vile Mali na CAR.

Kupanda kwa hisia dhidi ya nchi za Magharibi

Pia kuna washirika wa muda mrefu wa Kiafrika wa Magharibi ambao wamejizuia ukosoaji wa moja kwa moja wa vitendo vya Putin.

Senegal, kwa mfano, ilichagua kutounga mkono hoja ya Machi 2 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayoitaka Urusi kuacha kutumia nguvu dhidi ya Ukraine.

Cameroon ilipitisha msimamo sawa na huo, balozi wake katika Umoja wa Mataifa kwa busara alikwepa kikao ch abaraza hilo mapema mwezi Machi ili kukosa kura muhimu.

Mnamo tarehe 7 Aprili nchi hiyo pia haikushiriki wakati Baraza Kuu lilipopiga kura ya kusimamisha Urusi kutoka kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.

Maoni ya umma nchini pia huchukua sehemu kubwa katika misimamo kama hii.

Kuungana na Ufaransa, Marekani na Uingereza wakati mwingine sio msimamo maarufu zaidi katika bara hilo na serikali ya Cameroon, kama baadhi ya wenzake, inaonekana kuhitimisha kwamba ilipaswa kuzingatia hisia hizo maarufu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watu wengi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaunga mkono ushiriki wa kijeshi wa Urusi katika nchi yao

Hata hivyo, Cameroon imeenda mbele zaidi, ikichukua uamuzi makini wa kutia saini mkataba mpya wa ushirikiano wa kijeshi na Urusi huku jeshi ya nchi hiyo likiendelea kushambulia miji ya Ukraine.

Msimamo huu wa kipekee pengine unachnagiwa na hali tete nchini Cameroon.

Rais anayezungumza Kifaransa Paul Biya anakabiliwa na changamoto za kiusalama katika nyanja mbili: wakati serikali yake inapambana na Boko Haram yenye makao yake Nigeria na vuu vugu la Kiislam la Afrika Magharibi (Iswap) katika eneo la Kaskazini ya Mbali, pia iko katika mapambano ya muda mrefu kukandamiza uasi wa kutaka kujitenga katika mikoa miwili ya nchi hiyo inayozungumza Kiingereza, Kusini-Magharibi na Kaskazini-Magharibi.

Kando na Urusi, Cameroon pia ina makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa, Uchina, Brazil na Uturuki - na iliwahi kuwa na makubaliano na Marekani.