Mwanamume aliyerejea kutoka kwa wafu  

th

Chanzo cha picha, Ivan

Maelezo ya picha,

Ivan Skyba

Dereva teksi na baba wa watoto wanne, Ivan Skyba, alijikuta akitetea barabara ya mijini mwanzoni mwa vita. Aliepuka kifo mikononi mwa Warusi. Wanaume wengine wote wa Kiukreni pamoja naye hawakuwa na bahati sana. Waendesha mashtaka wanachukulia kile kilichotokea katika mji mdogo wa Bucha kama uhalifu wa kivita. Fergal Keane amekuwa akikutana na Ivan, manusura pekee.

Kuna hamu ya kufichua yote. Lakini Ivan anajua itakuwa kifo chake ikiwa atafanya hivyo. Joto ni la juu hapa  .Pumzi yenye joto ikipanda ndani ya hewa baridi itaunda ukungu mdogo na kuwatahadharisha wauaji. Tayari wanakagua miili ya watu ambao wametoka kuwapiga risasi, wakihakikisha kwamba wanapiga risasi ya mwisho ambapo wanaona dalili yoyote ya maisha. Anasikia mmoja wa Warusi akisema: "Huyo bado yuko hai!"

Ivan anajiuliza ikiwa wanazungumza juu yake? Labda ni moja ya wengine. Bado, anajitayarisha kwa risasi. Tayari anavuja damu kutokana na jeraha la ubavuni mwake. Mrusi mwingine anasema: "Atakufa peke yake!"

Lakini basi kuna risasi. Inapiga mtu mwingine. Mwanamume hupigana na matakwa tofauti katika wakati kama huo. Jeraha la risasi ubavuni mwake linauma sana. Lakini kulia kungekuwa mbaya. Yote hii itarudi baadaye katika ndoto. Lakini kwa sasa, atalala kati ya wafu. Atakuwa mtulivu kama wenzake waliouawa.

Unaweza pia kusoma

Ninakutana na Ivan Skyba katika kijiji kidogo kijijini Poland ambapo amepata makazi kwa ajili ya familia yake. Ana kazi. Watoto wanaishi mahali waliko bila hofu. Hali ya hewa ya joto imefika na jioni familia hutembea hadi kwenye bustani ya mahali ambapo Ivan huvua samaki katika ziwa. Michubuko kwenye uso na mwili wake imepona. Lakini usiku, baada ya kila mtu kulala, majeraha ya kumbukumbu yanafunguliwa. Ivan Skyba ndiye mtu aliyerudi kutoka kwa wafu.

Wakati yote yalianza katika masaa ya mapema ya 24 Februari, Ivan alikuwa akiendesha teksi yake huko Kyiv. Alisikia milipuko. Ivan alijitahidi kuamini kuwa kweli ilikuwa inatokea. "Sikufikiria inakuja," anasema.

Mtumaji alipiga simu na kusema teksi zote zinapaswa kurudi kwenye msingi. Ivan mwenye umri wa miaka arobaini na tatu amekuwa akifanya kazi yoyote ambayo angeweza kupata ili kumtunza mke wake na watoto wanne. Aliendesha teksi na wakati mwingine alifanya kazi kama ukarabati wa jengo. Wazo lake la kwanza asubuhi hiyo lilikuwa kupata hati za utambulisho wa familia hiyo. Ikiwa wangelazimika kukimbia, walihitaji pasipoti. Kwa haraka aliendesha kilomita 40 kuelekea Brovary walipokuwa wakiishi - na kutoka huko hadi Bucha ambapo mke wake na watoto walikuwa wakimtembelea mama yake. Hapo ndipo familia ingekaa hadi wafanye mpango.

"Uvumi tofauti ulikuwa ukienea kwamba [Warusi] walikuwa wanakaribia Bucha. Tulianza kupanga makazi kwenye vyumba vya pishi, na kuleta vitu huko."

Chanzo cha picha, Ivan

Maelezo ya picha,

Ivan (Kushoto)na rafiki yake Svyatoslav Turovsky na binti wa Ivan Zlata

Siku tatu baadaye, mnamo Februari 27, Warusi walifika karibu. Karibu mara moja walipata shambulio la kuvizia na mizinga ya Kiukreni. Safu ya askari wa anga wa Urusi walikuwa wamejipanga kwenye Mtaa wa Vokzalna wakati makombora yalipoingia yakipiga mayowe. Walirudi nyuma kwa muda. Lakini walikasirika, wakiamini kwamba baadhi ya wenyeji walikuwa wamewaambia wanajeshi wa Ukrain kuhusu eneo lao.

Kufikia sasa, kote Ukraine, watu walikuwa wakihamasishwa kutetea jamii zao. Bucha haikuwa tofauti . Ivan Skyba na rafiki yake, Svyatoslav Turovsky, baba mungu wa binti yake Zlata mwenye umri wa miaka miwili, walisikia kwamba baadhi ya watu waliopigana mashariki mwa mkoa wa Donbas dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi walikuwa wakiunda Bucha kitengo cha Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Ukraine. , wanamgambo wa kulinda jamii wakati wa vita. Wanaume hao wawili waliungana.

"Tulikuwa tukifanya kazi katika vituo vya ukaguzi, kuangalia nyaraka na kuhakikisha kuwa watu hawabebi silaha," anasema Ivan. "Tulikuwa tukisaidia kupanga njia salama za watu kutoka kwa sababu tulijua eneo hilo."

Kikosi cha Ivan kilikuwa na silaha duni. Walikuwa na bunduki moja, guruneti na darubini za kugawana kati ya wanaume tisa. Yeye na wenzake walifanya kazi kwa zamu kwenye kituo cha ukaguzi kwenye Mtaa wa Yablunska. Katika Kiukreni ina maana "barabara ya tufaha", kwa sababu ya miti ambayo inakaribia urefu wake wa karibu 6km. Wakati wa amani, ni mahali pazuri na ziwa la uvuvi. Baadhi ya nyumba zinarudi kwenye mashamba na bustani.

Pia ni eneo tata la ofisi ya zamani, iliyojengwa katika enzi ya Soviet, ambayo sehemu yake imebadilishwa kuwa maeneo ya kazi kwa biashara za ndani. jumba hili katika 144 Yablunska Street lilikuwa makao ya Warusi maarufu katika hadithi ya ukatili wa kivita.

Kufikia mapema Machi, Waukraine maelfu kwa maelfu walikuwa wakiitoroka nchi yao. Ivan na mke wake waliamua kujaribu kupata maficho katika  Bucha fkwa muda. Anaelezea hali miongoni mwa watu kama ya  ukaidi. 

"Hapakuw ana uwoga, Hakuna uwoga. Kulikuwa na hamu ya kuungana, kukusanyika. Tulikuwa tunatembea kila wakati. Tulipokuwa hatuko kazini, tulikuwa tunasambaza chakula kwa watu waliokuwa wamepata makazi pale, wanawake na watoto. Hapakuw ana mud awa kuogopa ." 

Hilo lilibadilika ghafla tarehe 3 Machi. Warusi walirrudi kwa nguvu "ikatika nusu ya pili ya siku, masaa ya chakula cha mchana".

Mara moja, Ivan na wengine walianza kuongoza magari yaende mbali na mwelekeo wa mashambulio ya Warusi. Kulikuwa na mashambulio ya kiholela. Maroketi yalikuwa yanaanguka.

Aliona gari jeupe aina ya Renault likiwa limeegeshwa na mwanamke na watoto walikuwa wamekwamaa ndani ya gari lililokuwa linaungua. Kulikuwa na wanaume wanane katika kituo cha ukaguzi cha Ivan na kwa kuwa Warusi walikuwa wanakaribia eneo hilo kwa haraka waliamua kujificha.  

Kituo cha ukaguzi kilichokuwa mkabada, katika mtaa wa 31 Yablunsk kulikuwa na nyumba ya Valera Kotenko. Mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 53 alikuwa amewapatia vinywaji vya moto na chakula. Alitoa wapa sasa makazi. Muda mfupi Warusi walikuwa nje. 

Chanzo cha picha, IVAN SKYBA

Maelezo ya picha,

Ivan kwenye kituo cha ukaguzi nje ya 31 Yablunska Street

"Tulikuwa tunawasikia na sauti za vifaa vyao zilikuwa zinasikika. Tulikuwa tumezingirwa," anasema Ivan. Wanaume walikuwa wananong’onezana. Hawakuweza kukimbia. Warusi walikuwa na ving’amuzi vya kung’amua picha ambavyo kusema kweli vingeweza kumg’amua mtu yeyote ambaye anajaribu kutoroka usiku. 

Wanaume walikuwa wamepata silaha zao chache na sasa walikwua wameamua kutunga hadithi – kama Warusi wangewapata wanesema walikuwa ni wajenzi wanaofanya kazi katika wilaya na wamekuwa wakijificha mapigano.  

Waliweza kuwatumia jumbe wake na wapenzi wao. Mmoja wao alikuwa ni , Anatoliy Prykhidko, mwenye umri wa miaka 39, alimpigia simu mke wake Olha jioni ile- Machi 3 – na akanong’oneza kwamba hakuweza kuongea kwasababu anaweza kusikika. Kulikuwa kimya sana. Alisema walikuwa wamejificha." 

Asubuhi iliyofuata, Yulia, mke wa Andriy Dvornikov, dereva wa kusambaza bidhaa, alipokea ujumbe uliosema: "Tumezingirwa, tumekaa hapa, lakini nitaondoka hapa karibuni kwani kuna fursa ya kufanya hivyo." Alimwambia mke wake afute jumbe zote na picha kwenye simu yake. Na akamwambia anampenda. 

Chanzo cha picha, OLHA AND ANATOLIY PRYKHIDKO

Maelezo ya picha,

"Saa 10 asubuhi, [Anatoliy] alinitumia ujumbe akisema 'bado tumekaa vizuri.' Huo ulikuwa ujumbe wake wa mwisho," anasema Olha Prykhidko

Huku machozi yakimtiririka usoni, Olha Prykhidko,ananiambia  kuhusu mawasiliano yake ya mwisho kutoka kwa Anatoliy katika asubuhi ile ya tarehe 4 Machi  : "Saa nne asubuhi, alituma ujumbe akisema 'bado tumekaa hapa tumejificha .' Huo ndio ulikuwa ujumbe wake wa mwisho." 

Chini ya saa moja Warusi walikuwa wamevunja mlango na kuingia ndani. 

Ivan Skyba anakumbuka vipigo na maswali yaliyokuwa yanaulizwa kwa sauti ya  kali. Simu za mkononi na viatu vilichuliwa . Kufikia saa tano asubuhi picha za CCTV zilizonasa tukio zinaonesha wanaume waliokamatwa wakiongozwa na baadaye kupelekwa  katika mtaa wa Yablunska Street  kuelekea numba 144. Kila mmoja wao alikuwa ameweka mkono kweney mkanda wa mwanaume mwingine mbele yake  na mwingine kweney kichwa chake. Walikuwa wamejipanga wakitazama mbele ya ukuta uliokuwa karibu na ngome na kupigishwa magoti.  

Warusi walifunga mashati na masweta yao ili wasiweze kuangalia. Walipigwa na vishikio vya bunduki na kutukanwa.  Kulingana na Ivan walipaza sauti : "Ninyi ni wapiganaji wa Bandera (kikundi kilichopinga  Usovieti katika Vita kuu ya pili ya dunia). Ulitaka kutuchoma na mchanganyiko wa Molotov! Tutawachoma mkiwa hai sasa!" 

Ivan anasema Warusi waliamua kuwatisha wengine  kwa kumpiga risasi Vitaliy Karpenko ambaye alikuwa na umri wa miaka 28, mfanyakazi wa duka la ushirika. Baada ya hili, kijana mdogo zaidi katika kikundi alichanganyikiwa na kuwaambia Warusi kwamba wote ni wajumbe wa kikosi cha ulinzi wa eneo. Vipigo vikaongeza.   

Ivan Skyba na mwanaume mwingine, Andriy Verbovyi, baba wa mmoja wao na ambaye pia ni  mrandaji waliletwa ndani ya jengo. Katika uchunguzi hilo lilifuatia , Ivan  alikwa nan doo iliyowekwa kichwnai kwake na alilazimishwa kuinama na kuegamia ukuta. 

Matofali yalilundikwa mgongoni mwake, hadi alipoanguka. Alipigwa tena na matofari yaliendelewa kupasuliwa juu ya mgongo wake.  

Wakati mmoja alisikia polisi wakimwambia  Andriy Verbovyi  kwamba watampiga risasi mguuni. Kulisikika risasi. Baada ya hilo hakumsikia Andriy tena. 

Halafu Ivan aliondolewa katika jengo kujiunga na wanaume wengine. Baadhi ya kile kilichofanyika kilishuhudiwa na wakazi wa eneo hilo ambao waliamrishwa na Warusi  kukusanyika mbele ya mtaa namba 144, lakini waendelee kutengana na wanaume wengine.

Lucy Moskalenko anakumbuka afisa wa Urusi akimwambia afunike macho ya binti yake kwasababu wataona vitu ambavyo hawatavisahau . Alituambia " Msiwaangalie  msiangalie watu waliolala chini. Sio binadamu.  

Niwachafu kabisa. Wachafu. Sio binadamu. Ni wanyama.'" Dada yake, Irina Volynets, alikuwa ameambatana naLucy. Wote wanakumbuka kelele za magari ya makombora ya vita ya Warusi, na jinsi mbwa walivyokuwa eneo hilo walivyokuwa wakipigana, ni kama kichaa kilikuwa kimeingia katika eneo. 

Kisha Irina alipigwa na mshtuko.Aliona kwamba mwanafunzi mwenzake wa zamani, Andriy Verbovyi, mvulana ambaye alikuwa ameketi kando yake kutoka shule ya chekechea, na njia yote ya shule, alikuwa amelala chini akivuja damu. Wiki chache tu kabla, walikuwa wametembea nyumbani kutoka kituo cha ununuzi pamoja.

Kulikuwa na karatasi iliyotupwa chini karibu naye. "Alikuwa amelala pale, akiwa amejipinda kutokana na baridi. Alikuwa akinitazama moja kwa moja. Tuliangaliana machoni," anasema. Irina alitaka kwenda kumfunika rafiki yake wa zamani na karatasi, chochote ambacho kingeweza kumfanya apate joto. Lakini hakufanya hivyo. "Je, aliogopa sana?" Nauliza.

"Haikuwa hofu kubwa kama kukata tamaa," anajibu, "na nilikuwa nimechanganyikiwa sana wakati huo, na sikuweza kuelewa jinsi ilivyokuwa, na kwa nini mwanafunzi mwenzangu alikuwa amelala chini." Kila kitu kilikuwa kikifanyika kwa haraka sana. Mbali na hilo, alikuwa ameona tu kwamba mtoto wake Slavyk alikuwa katika foleni ya wanaume. Alikuwa ametekwa kando na kupigwa, kabla ya kuletwa kuungana na wengine.

Alipokuwa akisubiri kwenye foleni Slavyk aliona damu kwenye sakafu karibu naye, na kusikia Warusi wakizungumza kuhusu mtu aliyejeruhiwa. Hakika huyu alikuwa Andriy Verbovyi. "Niliwasikia wakizungumza wao kwa wao ili kummaliza kwa sababu hangefanikiwa," anakumbuka Slavyk. alianza kuhofia maisha yake mwenyewe.

Irina alipata afisa na kumwelezea kuhusu hali ya Slavyk. Askari huyo alisikiliza. Kisha akamwita mtoaji habari wa Kiukreni - labda mtu aliyekamatwa ambaye alikuwa amepasuka baada ya kupigwa risasi Vitaliy Karpenko - na kumuuliza: "Je, yeye ni mmoja wao?"

"La," jibu lilikuja. Slavyk aliachiliwa na kuwasilishwa kwa mama yake. Wakazi waliambiwa waende nyumbani, lakini Irina anakumbuka hisia za kutisha alizopata slipokuwa akiondoka. "Nilikuwa na hofu jambo la kutisha lingetokea." 

Siku iliyofuata, Machi 5, mke wa Andriy Verbovyi, Natalya, alimtumia ujumbe. 

"Uko wapi? Niko na mkufu wako [wa bahati], tna kidani chake pia. Nakulinda dhidi ya vitu vyote vibaya. Tunakuombea. Tunasubiri simu yako. Tuandikie japo ujumbe wa maneno mawiliWrite us at least ." 

Wakti huo, Andriy alikuwa amefariki. 

Ivan Skyba alihisi muda unayoyoma. Kufikia baadaye mchana wa wa Machi 4, wawili kati ya wanaume wanane waliotekwa pamoja naye walikuwa wameuawa kwa kupigwa risasi. "Warusi walikuwa wakisemezana kuhusiu kile watakachotufanyia. Mazungumzo yalienda hivi: 'Tufanye nini nao?' Mtu wa pili anasema, 'Wamalize, lakini watoe nje ili miili yao isilale hapa.'" 

Wanaume waliobaki waliopelekwa nyuma y aua mdogo. Kutoka chini ya ukingo wa nguo zake Ivan aliona mwili wa mtu ukiwa kwenye jukwa dogo la saruji. Alikuwa amepigwa risasi awali. Warusi walianza kuwathihaki waathiriwa wao. "Walikuwa wakifurahia kuwaua wakitumia maneno ya matusi, wakisema, "kapooey (kifo) ndio mwisho wako!" Ivan anakumbuka kurushiana maneno ya mwisho na wenzake. "Tuliagana. Ilikuw ahivyo That was it." Miongoni mwa aliowaaga ni Svyatoslav Turovsky, baba wa kiroho wa binti yake. 

Kulingana na Ivan, Anatoliy Prykhidko ghafla aliamua kutoroka. TLakini Warusi waliwamiminia risasi wengine. "Nilihisi risasi ikipitia ubavyuni mwangu," Ivan anakumbuk. "Itlinijeruhi nikaanguka chini." 

Chanzo cha picha, IVAN SKYBA

Ivan hawezi kukumbuka Warusi walichukua muda gani haswa, lakini ilikuwa madakika zaidi ya masaa. Alipobaini wameondoka alijaribu kuangalia chini kupitia koti lake.

Ua lilikuwa kimya bila mtu yeyote. Sasa ndio nafasi yake. Alinyoosha mkono kuchukua viatu kutoka kwa miguu karibu naye – ya mtu aliyeuawa alipowaona wameingia uani mara ya kwanza.

Alimvua mwanamume huyo viatu na kuvivalia miguuni. Kisha akatambaa kuelekea nje ya ua na kwenda kwenye bustani lililokuwa karibu. Kulikuwa na ua lingine la kuvuka kabla ya  kuingia kwenye nyumba iliyoachwa nawenyewe wakati wa mashambulio ya makombora.

Kilichofuata ni kisa kingine cha kusikitisha. INdani ya nyumba hiyo Ivan alitibu jaraha lake kwa kutumia maji ya dawa aliyopata kwenye bafu na kubadilisha nguo zake na kuvalia zile zilizoachwa nyuma na mwenye nyumba hiyo. Alijifunika blanketi na kujaribu kulala. Lakini alisikia sauti. Sauti za Warusi. Alibaini baadaye kwamba maaskari wa Urusi pia walikuwa wakipumzoka katika nyumba hiyo. 

"Waliniona na kuanza kuniuliza mimini nani na nilikua nafanya nini huko." Aliwashawishi kuwa ni mmiliki wa nyumba na kwamba familia yake ileondolewa. Kuhusu majeraha yake , alielezea kuwa yalitokana na milipuko ya mabomu. Maaskari waliamini alichosema lakini wakamwambia kwamba hawezi kukaa mahali alipokuwa. Badala yake, walisema watampeleka katika kambi yao kupata huduma ya matibabu. Katika barabara ya 144 Yablunska. "Nilikuwa na uwoga nini kitakachotokea baadaye – kutoka kwa utumwa mmoja hadi mwingine."

Lakini bahati ya Ivan ilisimama. Katika kambi, madaktari wa kijeshi walitibu majeraha yake. Ikiwa wanajeshi waliompiga risasi bado wangalipo,huenda hawakumuona akirudi, au kumtambua. Aliunanishwa na raia waliokuwa wamepewa makazi katikajengo moja. Baada ya siku kadhaa, waliruhusiwa kuondoka. 

Miili ya wanume waliouwa wakilinda Bucha Pamoja na Ivan iliachwa ikiwa imetapakaa uani, ambako Warususi walikuwa wakitupa taka, kwa miezi kadhaa tangu uvamizi wao. Ivan alipata familia yake ikiwa bado inajificha vita nyumbani. Waliweza kutoroka Bucha, na hatumaye kuondoka Ukraine hadi Poland, na licha ya saa kadhaa za mapigano makali katik aeneo la 144 Yablunska.