Urusi na Ukraine: Ni kweli 'Ubabe' wa Putin ulisababisha vita ?

Putin

Chanzo cha picha, AFP

Kauli ya Waziri mkuu wa Uingereza  Boris Johnson,  ambaye alisema kuwa Vladimir Putin angekuwa mwanamke asingeanzisha vita, iliibua mjadala. Nchini Urusi. Mjadala huo haukuwa wa kushangaza,  kutokana jinsi  rais huyo wa Urusi alivyodumu mamlakani kwa muda mrefu na jinsi alivyotengeneza picha ya "unaume halisi", ambayo sio tu imekuwa jambo la kejeli katika vyombo vya habari vya Magharibi , lakini pia kitu cha utafiti wa kisayansi . "mfumo dume sumu" wa sumu na tabia ya mfumo dume ambayo ni maarufu  katika jamii ya Urusi  huenda ilichochea  kuibuka kwa vita na Ukraine na uungaji mkono wa uvamizi, wanasaikolojia na wanasosholojia waliohojiwa na BBC wanaamini.   

Kwa kipindi cha miezi minne iliyopita, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amewaita mabalozi mara tatu kuhusiana na taarifa za wanasiasa kigeni. Mara mbili mwezi Machi. Wanadiplomasia wa Urusi walitoa  "pingamizi kali"  kwa balozi wa Marekani George Sullivan -baada ya Seneta Lindsey Graham kumtakia Vladimir Putin kifo, na rais wa marekani Joe Biden alimuita Putin mhalifu wa kivita, jangili na dikteta kwa siku kadhaa - muuaji. 

Kwa mara ya tatu, mwezi Juni, balozi wa Uingereza aliitwa na  Wizara ya mambo ya nje baada ya Boris Johnson kusema kuwa Putin alikuwa mfano wa  " mfumo dume sumu."

"Kama Putin angekuwa mwanamke- jambo ambalo silo- lakini kama angelikuwa , sidhani kama angeanza vita vyake vya ubabe- uvamizi na ghasia jinsi  alivyofanya. "Kama unataka mfano halisi wa uanaume sumu, hicho ndicho anachokifanya nchini Ukraine," Johnson alisema. 

Baadaye aliungwa mkono na Waziri wa ulinzi wa Uingereza  Ben Wallace, ambaye alisema Putin ''anajiona hatoshi" na  mtizamo wa "ubabe" wa dunia ulisababisha vita.

 Kujibu hayo, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alilalamika kuwa Johnson anaweza kupelekwa kumuona daktari wa akili  Freud, halafu Putin mwenyewe alitoa somo kuhusu ukali wa  Margaret Thatcher. Na siku chache baadaye, Balozi wa Uingereza   Deborah Bronnert aliitwa na Wizara ya mambo ya Urusi na kuelezea "kupinga vikali  kauli  za dharau kwa uongozi wa Uingereza kwa Urusi, kiongozi wake na maafisa wawakilishi wa mamlaka, pamoja na watu wa Urusi."

"Uanaume halisi"  

Jibu la Maafisa wa Urusi halionekani kutokuwa na uwiano sana, kama utakumbuka jinsi Rais Putin alivyojenga haiba na sura yake kwa muda mrefu "mwanaume halisi", wataalamu wanasema.

Katika kipindi chake chote cha utawala, Putin aliikumbusha dunia nguvu zake na na uthabiti alonao kimwili kutokana na mazoezi ya mwili anayoyafanya, alipokuwa akishuka chini ya Ziwa Baikal, akipaa na Korongo wa Siberia, akipiga mbizi chini ya bahari Taman Bay, akitembelea chui wa Amur na bila shaka alionekana akiwa amepanda juu ya farasi akiwa kifua wazi.

 Matukio hayo yaliyonyeshwa kwa umakini na Putin yanafanana kusema kweli na yale ya "uanaume wa sumu" na  "uchawi." Mtendo haya yanaonyesha wazo la mwanaume ambaye anatabia za uchokozi, hamu ya mamlaka, asiye kuwa na hisia ,mwenye chuki ya jinsia fulani au anayewadharau wanawake ,”anasema mwanasaikolojia wa familia Marina Travkova.

Sura ya mbabe Putin, ambaye binafsi anajionesha kama ‘’kiongozi mara’’ mwenye maadili ya "kitamaduni", ikilinganishwa na ile ya viongozi wa nchi za Magharibi, ilikuwa ni mzaha kwa muda mrefu.

Hata katika mkutano uliopita, viongozi wa nchi zenye utajiri mkubwa zaidi wa viwanda G7 hawakuwahi kupinga kulizungumzia,sawa na kauli za Johnson, walijadili kwa mzaha na kuonesha kwamba ni wenye nguvu zaidi kuliko Putin.  

Rais wa Urusi , kwa upande wake huwafanya maadui zake kama wajinsi ya kike anasema mwanahistoria wa masuala ya jinsia katika  taasisi ya MIT, Elizabeth Wood.

Haishangazi, alipojibu kuhusu mzaha uliofanywa na washiriki  wa  kikao cha G7, Putin alisema kama viongozi wa Magharibi wangevua nguo zao "wangechukiza " na akawashauri wafanye mazoezi ya viungo. 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ligi ya Mpira wa magongo wa Usiku,  ambayo Putin hucheza na maafisa na wanariadha wa kulipwa, ni mfano wa shirika lla wanaume lenye ushawishi  

Si Putin pekee anayejijengea picha ya uanaume pekee, bali ukweli ni kwamba amejenga mawazo hayo kote nchini Urusi, baadhi ya wataalamu wanasema.  

Huku Putin akianza kubadilika kuwa "aina mpya uanaume wa Mrusi," uwakilishi wa Urusi pa umebadilika, anasema  Elena Gapova profesa wa masuala ya kijamii katika Chuo kikuu cha Western Michigan.   

 Kulingana na  Gapova, iwapo mwanzoni kwa karne ya 20 mwanafalsafa Vladimir Rozanov aliielezea Urusi kama mwanamke a,mbaye daima anamtafuta bwana harusi ,mume, kwahiyo ili kuelewa kile kinachoendelea nchini Urusi katika miaka ya 2000,ni vyema kukumbuka wimbo "Such as Putin."

Katika mfumo huu, kila kitu huamliwa na wanaume, siasa ni chafu, wanawake hawatakiwi kuingilia. “Kitu kama hicho kinafanyika katika mashirika mbali mbali ya serikali  ambapo utapata wakijiita : “wanaume wapambanaji”, “Mbwa mwitu wa Usiku, “Wagnerites” – majina yote haya yamejengwa kwa kuwatenga wanawake.

Tazama vile wanawake walivyowekwa katika vyeo  vya jeshi la ulinzi - National Guard wanakuwa maarufu kwa vigezo gani  - wanashiriki katika mashindano ya urembo , "- anacheka Wood.

Uanaume kama ishara ya mamlaka 

Hata katika "klabu hii ya wanaume" Putin lazima kila mara aendelee kuwa  "mwanaume wa kwanza". Ilikuwa ni muonekano wake wa kiume ambao umekuwa njia ya Putin ya kuonyesha nguvu za mamlaka, anasema Elizabeth Wood.

Je vita vya Ukraine ni ubabe?

Maelezo ya video,

Vita vya Ukraine: CCTV ikionyesha raia wakitoroka makombora ya Urusi katika Kremenchuk

Picha ya Putin na mfumo dume wake, inaonekana, na inaweza kuwa na athari za moja kwa moja ya vita na Ukraine  Ukraine.

Vita vilivyoanzishwa na Putin vinaweza kuitwa kweli  "vita vya ubabe" kwa maana kwamba- pamoja na baadashi ya malengo ya kisiasa – ni wazi kwamba lengo la kifikra: ni kujionyesha, kuthibitisha umuhimu wake kwa nchi nyingine.

Unaweza pia kusoma

'Mateka wa sura'

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini , iwapo Putin  angekuwa mwanamke ingekuwaje?  

Wataalamu wote waliohojiwa na BBC walikubaliana na jambo moja: Maneno aliyoyasema Bw Johnson kwamba Putin angekuwa mwanamke asingeanzisha vita yanaonekana kutokuwa na uhusiano wowote na hali halisi.

“Maneno ya Johnson yanafa kuchukuliwa zaidi kama kielelezo,” anasema Elena Gapova, “Kuna mambo ambayo kwa  kawaida ambayo wanawake  huwa hawahusiki nayo, kwamba wanawake sio wachokozi, na wana huruma zaidi. Lakini hii ni kutokana na ukweli kwamba wana uwezekano mdogo zaidi wa kujipata katika nafasi hizo kijamii ambapo unaweza kuanzisha vita au kuchukua maamuzi hayo makubwa  ."

 Kulingana na Elena Gapova , madai yake kwamba historia ya vita vya dunia na mageuzi vilitokea kwasababu ya mfumo dume, na kama kungekuwa na wanawake wengi mamlakani, historia  ingekuwa tofauti. 

 Johnson kusema kweli alielezea mawazo ya ubaguzi kuwahusu wanawake, ambapo ni rahisi kwa wanawake kuzungumza na kufikia maafikiano, kuonyesha mapungufu, kuonyesha hisia. Lakini akayatumia kukabiliana na mfume dume wa Putin, anasema mwanasaikolojia Marina Travkova.