Wafahamu nyota wanawake wa Kombe la Euro 2022

e

Chanzo cha picha, Getty Images

 Michuano ya Kombe la Ulaya la wanawake itafanyika England kuanzia tarehe 6 hadi 31, Julai mwaka huu na timu bora za katika bara hilo zitakabiliana. 

Lakini je ni wachezaji gani maarufu  katika kombe hili?. BBC inawaangazia wachezaji  nyota zaidi 10 ambao watashiriki katika Euro 2022.   

Alexia Potias ( Uhispania)

Chanzo cha picha, QUALITY SPORTS IMAGES

Akiwa na umri wa miaka 28 kiungo huyu wa kati wa tumu ya taifa ya Uhispania alishinda tuzo ya Ballon d'Or  mwezi Novemba na alikuwa nafasi muhimu katika ushindi wa kwanza wa timu yake  Barcelona, katika  Kombe la washindi la Ulaya  la mwaka (2021). 

Pamoja na wachezaji wenzake katika timu hiyo, alifika fainali za shindano la hilo mwaka 2022. Oktoba, Potias aliweza kushinda rekodi ya michezo  mingi katika timu ya taifa lakeakiwa amecheza mechi 90 .   

Lena Oberdorf (Ujerumani)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka, kiungo huyu wa kati wa klabu ya  Dusseldorf. 

katika Kombe la Dunia la mwaka 2019, wakati alipokuwa na umri wa miaka 17 pekee, aliweza kutaribishwa katika timu ya taifa ya soka ya Ujerumani kwa mara ya kwanza.

Katika mwaka2017, wakati timu ya taifa ya Ujerumani iliposhinda kombe la washindi la vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 . " Tunaweza kusema kuwa ni kiungo wa kati mwenye uwezo zaidi hadi leo .  "Ni mchezaji anayeumudu  mpira vyema."

"Ni mchezaji anayeweza kuigeuza Ujerumani kuwa mojawapo ya iwashindani wakali kwa ajili ya championi, kwasbabu anaweza kuwasilisha mawazo ya ushindi miongoni  wachezaji wenzake  katika timu."

Ada Hegerberg (Norway)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka 26 mshambuliaji Hegerberg, tayari ameshinda  tuzo ya Ballon d'Or  mwkaa 2018 baada ya kuondoka katika timu ya taifa  kupinga kile alichokiona kama ukosefu wa heshima kwa wachezaji wa kike katika Norway.

Ni moja wa wachezaji maarufu sana wa soka duniani: alishinda michuono ya Kombe la washindi la Ulaya mara sita, Ligi ya soka ya Ufaransa mara saba, Kombe la FA mara tano na Kombe la FA la Norway mara moja.   "Ada anaonekana kuwa alizaliwa kuwa mshindi! 

Unaweza pia kusoma:

Vivian Miedma (Uholanzi)

Chanzo cha picha, Getty Images

 Vivian mwenye umri wa miaka 25 ni mshambuliaji wa Arsenal  ambaye ni mfungaji bora zaidi katika historia ya timu ya taifa ya wanawake ya Uholanzi. Pamoja na timu yake alishinda Euro 2017 na kufikia fainali ya  Kombe la Dunia la mwaka 2019.

Alishinda ligi mara tatu : mara moja akiwa katika Arsenal - England na mara mbili akiwa katika klabu ya Bayern Munich nchini Ujerumani. Pia anashikilia rekodi ya mfungaji bora ya  Super League ya wanawake  na mchezaji mwenye umri mdogo zaidi  (miaka 15)  aliyewahi kucheza  katika Ligi ya Uholanzi .

"Kiwango chake cha akili cha mchezo ni cha hali ya juu  na cha ajabu sana. Ni mchezaji wa hadhi ya kimataifa , na kitu ambacho watu wengi hawajui uwezo wake wa kimwili  . "Vivian ni mchezaji mwenye nguvu sana, anayeweza kukimbia kwa haraka . Uwezo wake huu umewafanya wapinzani wake kupata ugumu sana wa kumkabili .

Lauren Hamp (England)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka 21-  ni mchezaji wa Klabu ya  Manchester City. Msimu huu, alishinda tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kw amra yan ne na kuvunja rekodi . 

Mwaka huu alishinda Kombe la FA .  Pia ana historia ya kushinda katika Kombe la soka la England (2020)  na amecheza mechi mara 21 kwa ajili ya timu ya taifa ya England.

Kutokana na kasi yake, mlinzi yeyote atakuwa na wakati mgumu wa kumzuia katika kabiliano ya moja mmoja.  

Wendy Renard (Ufaransa)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka 31- mlinzi wa klabu ya  Lyon  katika mashindao ya washindi 14 . 

Anashikilia rekodi ya ligi ya soka ya Ufaransa. Ameshinda tayari vikomve vya Ulaya mara nane  n ani nahodha wa klabu na timu taifa  lake.

Mwezi Mei alikuwa mchezaji wa kwanza kufikia rekodi ya mechi 100 katika Champiopni Ligi. 

Jina lake limejumuishwa katika kikosi kilichochaguliwa cha wanawake wanaocheza soka wa muongo uliopita, na pia amekwisha chaguliwa katika timu ya FIFA yam waka mara sita. 

Nahodha Fridolina Rolfo (Sweden)

Chanzo cha picha, Getty Images

Fridolina Rolfo  ambaye ana umri wa miaka 28- ni mshambuliaji wa    Barcelona  ambaye ameshinda ligi katika timu tatu tofauti. Katika mwaka 2021, alikuwa mchezaji wa mwaka wa soka wa Sweden.

Pamoja na timu ya taifa ya Sweden, alishinda  taji la shaba la fedha la  Olympiki mara mbili na taji la shaba la Dunia mara moja  "Ni mchezaji thabiti  mwenye mikwaju mirefu na anapochomoka sio rahisi kumsimamisha."

  Rachel Furness (Ireland ya Kaskazini)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo huyu wa kati wa Liverpool  ana umri wa miaka 34. Ni mfungaji bora zaidi  katika historia ya timu ya taifa ya Ireland Kaskazini.

Katika mwaka 2021, baada ya kucheza nafasi muhimu katika timu yan chi yake na kuiwezesha kufikaa katika mashindano muhimu zaidi la kimataifa   (Kombe la Dunia na Euro),  alipokea Tuzo la mchezaji bora zaidi wa mwaka kutoka  BBC.

Pernille Harder (Denmark)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka 29, mshambuliaji huyu kutoka klabu ya Chelsea ndiye mchezaji  wa kike wa soka mwenye thamani ya juu zaidi katika historia ya soka kwa   kuhama kutoka Wolfsburg kuja  London katika mwaka 2020. Ni mchezaji bora mara mbili wa UEFA na ameshinda kombe la Chambpioni Ligi mara sita.

"Parlin kila mara huwa katika mahali panapofaa katika wakati unaofaa kwasababu anauelewa vyama mchezo''.

Caroline Graham Hansen (Norway)

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka  27-kiungo wa kati wa  Barcelona ana mchango muhimu katika timu ya taifa ya Norway ambapo alifikia fainali za Euro mwaka 2013 akiwa  kijana mdogo. Alishinda Ligi mara sita na Kombe la mapigwa wa Ulaya mara moja