Vitisho vya kutisha vya Putin kwa Sweden, Finland na NATO

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameishutumu NATO kwa kuwa na  "tamaa za kifalme", huku washirika wa Magharibi wakiahidi kuongeza usaidizi wao kwa Ukraine. 

Akizungumza katika Turkmenistan, Bw Putin aliwamnia waandishi wa habari kwamba wajumbe wa Muungano wa NATO hawana nia katika kuboresha maisha ya watu wa Ukraine. Alisema Urusi itajibu hatua yoyote ya kuongeza vikosi vya ziada katika Sweden na Finland, nchi ambazo ziko katika mchakato wa kujiunga na NATO.   

Inafahamika kwamba hii ni ziara ya kwanza ya Bw Putin nje ya Urusi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine. Katika kikao cha Madrid,  Katibu Mkuu wa Muungano wa NATO Jens Stoltenberg aliahidi usaidizi kwa Ukraine kwa muda wote wa vita hata vichukue muda gani.

NATO imezikaribisha rasmi Sweden na  Finland  kujiunga na muungano- na hivyo kumaliza sera yake ya kutofungamana na upande wowote. Uturuki imepinga uamuazi huo, ikizishutumu nchi hizo mbili kwa kuwapokea  wanaharakati wa Kikurdi kutoka Uturuki wanaochukuliwa kama magaidi.

Lakini raisi wa uturuki  Recep Tayyip Erdogan baadaye alikubali ombi lao, na badala na akahakikishiwa usalama.   

Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images

Uamuzi huu unafuatia mkutano baina ya Bw Erdogan, Katibu mkuu wa NATO na viongozi wa Finland na Sweden.

 Ofisi ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema imepata kile ilichokitaka kutoka kwa Sweden na Finland. 

Nchi hizo za Scandinavia zilitangaza nia yao ya kujiunga na Nato mwezi Mei, katika kujibu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. 

Katibu Mkuu wa Muungano wa Nato  Stoltenberg alisema kuwa kwamba mchakato utaharakishwa, akitangaza ushirika wao  kwa NATO. 

Joe Biden pia alizungumza kwa njia ya simu na Bw Erdogan  Jumanne. Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani Celeste Wallander alisema kuwa rais huyo alifikia makubaliano na Uturuki, lakini aliongeza kuwa Marekani iliunga mkono usasa wa ndege za kijeshi za Uturuki na ataendelea na mazungumzo kuhusu ombi la Ankara F-16.

Moscow ilisema kuwa upanuzi wa muungano wa NATO utakuwa na madhara ambayo hayakulengwa na kusababisha  ‘'ukosefu wa usalama wa muda mrefu’’.

NATO ina nguvu kiasi gani?

Chanzo cha picha, Getty Images

Kanuni ya msingi ya muungano huo w akijeshi wa kimataifa (NATO) ni mfumo wa pamoja wa ulinzi, ambao unamaanisha kwamba kama mmoja wa wajumbe anaposhambuliwa nan chi nyingine, basi kila nchi mwanachama lazima aingie vitani kuilinda nchi iliyoshambuliwa.   Kwa maana kwamba wajumbe wote wa NATO wataishambulia nchi iliyoshambulia mmoja wa wanachama wake.

Bahati mbaya, maslahi ya NATO yanajumisha nchi kama vile Montenegro,  ambayo hutumia kiasi cha pauni milioni 67 pekee kwa mwaka katika ulinzi, wakati baadhi yanchi nyingine zenye nguvu zaidi zinatumia pesa zaidi katika muungano huo. 

Marekani hutumia zaidi ya maradufu ya pes azote za ulinzi zinatotolewa na NATO kwa ujuml, huku takriban dola 705 (£ 516bn) zilikadiriwa kutumiwa katika mwaka   2021, kulingana na Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo .

Zaidi ya hayo  mwekezaji mkubwa zaidi katika ulinzi, Marekani pia ina hifadhi kubwa ya silaha na idadi kubwa ya wanajeshi waliopewa mafunzo- milioni 1.3 waliosajiriwa na wanaoshiriki katika mapigano, ikiwa na wanajeshi wengine 865,000 wa ziada, kulingana na  New York Times  mwaka 2017.

Uingereza ni nchi ya pili kwa kuwa na matumizi makubwa katika muungano wa NATO, ikiwekeza karibu pauni bilioni 50 kila mwaka ikilinganishwa na Ujerumani ambayo inawekeza pauni bilioni 45, Ufaransa bilioni 42 na Italia bilioni 20.

Ingawa hakuna kikosi cha NATO cha kudumu, Muungano unanufaika na kushirikishana uwezo wa kijeshi na uzoefu wa kila nchi mwanachama. Kila nchi ina kitu fulani cha  kuongezea, vikosi, vifaru vya kijeshi, manuari za kivita n ahata ndege za kisasa za vita. 

Hadi le oleo wanahesabu  karibu watu milioni 3.5, wote wafanyakazi, wanajeshi na raia katika nchi wanachama wa Muungano huo. Kila nchi mwanachama inakubali kuchangia kulingana na viwango vya mikakati mbali mbali  nUchaguzi wa urais Uganda: Ni rasmi Kizza Besigye hatagombea urais nchini humo matokeo mbali mbali.

Kwa ujumla mataifa wajumbe wa NATO ni 30.