Jinsi ya kuishi miaka100 - Wataalamu waelezea siri

Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, Kiko Tanaka, alifari akiwa na na umri wa miaka

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

 Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, Kiko Tanaka, alifari akiwa na na umri wa miaka  

 Hapo zamani, maisha marefu yalionekana ni kitu kisichowezekana. Lakini sasa mambo yamebadilika. Je uzee  kucheleweshwa au hata kuzuiwa? Je wale wenye umri wa zaidi ya miaka 100 wanasiri ambayo inaweza kumsaidia kula mtu kuishi miaka mingi?

 Ijumaa,Januari 2, 1903, mtoto mchanga wa kike anayeitwa Kiko Tanaka  alizaliwa katika kijiji kidogo kilichopo katika kisiwa cha kusini mwa Japan. Katika mwaka huo huo, mashindano yam bio za baiskeli ya Tour de France yalianzishwa Paris  na kampuni ya magari ya Ford iliuza gari lake la kwanza. Kiko Tanaka alifariki dunia Aprili akiwa na umri wa  miaka 119, na alitambuliwa rasmi kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani. 

Aliishi miaka yake ya mwisho ya maisha yake katika nyumba ya wazee, akiamka saa kumi na mbili asubuhi kila siku kufanya hesabu, kucheza michezo ya ndani ya nyumba, kula chokoleti na kunywa kahawa na soda. 

 Kuwapata watu  wanaoishi miaka zaidi ya mia moja kama Koshi Tanaka sasa sio jambo lisilo la kawaida.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wazee wengi Japan  huanza ''ajira ya pili ''baada ya kustaafu

Ajira ya pili

Dr. Hiroko Akiyama  ni mtaalamu aliyebobea katika sayansi ya uzee (gerontology). Ni makamu mwenyekiti wa zamani wa Baraza la kisayansi la Japan na profesa katia Chuo Kikuu cha Tokyo.

 Hiroko Akiyama alisema kuwa Japan ni mojawapo ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na jamii inayozeeka. Wastani wa muda wa kuishi  wa Wajapan  kwa sasa ni mkubwa wa hadi miaka 88, na zaidi ya robo ya idadi ya watu kwa sasa wana umri wa zaidi ya miaka 65.

Wengine wenye matarajio sawa na hayo ya muda mrefu wa kuishi ni pamoja na  Hong Kong, Singapore, Switzerland, Ital ana Uhispania.

 Data kutoka kwa Wizra ya Afya ya Japan, Wafanyakani na Ustawi wa jamii zinaonyesha kwamba idadi kubwa ya watu wana umri wa miaka 100 nchini Japan na walifikia rekodi ya  watu  86,510 mwaka jana, ongezeko la zaidi ya watu 6,000 ikilinganishwa na kipindi saw ana hicho katika mwaka uliopita.

 Akiyama alisema kwamba kuishi mwa miaka mingi ni matokeo ya mambo mbali mbali, mojawapo ikiwa ni pamoja na mfumo wa bima ya afya kwa wote. Japan ina mfumo raihisi wa upatikanaji wa huduma za afya tangu miaka ya 1960, pili, watu wa Japan ni wtu wanaokuwa makini sana na afya zao, na wanaishi mtindo wa maisha unaozingatia afya, watu wengi huenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa matibabu mara kwa mara , Watu wa Japan pia hucheza michezo zaidi katika shughuli zao za kila siku.

 Zaidi ya hayo, Japan ni nchi yenye watu wenye viwango vya chini zaidi vya unene wa katika nchi zinazoendelea .Ulaji wa vyakula vyenye viwango vya chini vya Mafuta na ulaji wa samaki zaidi, mboga, mizizi ya majini na chai ya kijani kibichi, Wajapan wengi wanaamini kwa chakula cha kawaida ni kizuri kwa nyanja zote za maisha.

 Lakini huku watu wanaishi umri mrefu, idadi ya watu  wa Japan kwa ujumla inapungua. Hiyo ni kwasababu viwango vya uzazu vimeshuka kwa muda, na kufikia kiwango cha chini kuwahi kushuhudiwa nchini humo mwaka jana. 

 Akiyana alisema kuwa umri wa watu wanaofanya kazi umeongezeka, huku idadi ya wale wenye umri wa miaka 65 na zaidi, hususan wenye umei wa miaka 75 na zaidi ikiongezeka.

 Huku idadi ya wazee ikiongezeka, watu pia walibaini kuwa wazee pia wana mahitaji tofauti. 

 Serikali zinazokabidhiniana madaraka nchini Japan zimetambua hili, lakini juhudi zilionderkana kuendelea kuboressha sera zilizoanzishwa ili kuweza kuwasaidia wazee. 

 Hiroko Akiyama, 78, ameanza ajira yake ya pili."Nilikuwa profesa wa chuo kwa muda mrefu,"alisema. "Nilipokuwa na umri wa miaka 70, nilianza ukulima. Kuna watu wanee, nikiwemo mimi, wenye ujuzi tofauti, kwahiyo tulianza kampuni ambayo ilikupesha pesa nyingi. Ardhi ya kilimo na tukaanza ukulima mdogo. Nilipokuwa mdogo, nilitaka kuwa mkulima. Kwahiyo illikuwa ni ndoto yangu ya kwa miaka mingi .”

Alipoulizwa iwapo anataka kuishi miaka 100, alisema, sina uhakika. Mama yangu alifariki miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 98. Alikuwa na maisha mazuri. Sina uhakika kama ninataka kuishi miaka mingi zaidi yake…Sina utashi sana wa kuishi miaka zaidi ya 100."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Muda wa kuishi wa watu wa Japan umeongezeka, lakini tatizo la uzee pia linaonekana   

Kuzeeka ni nini?

Cathy Slack,  mhadthiri wa ngazi ya juu  katika kituo cha Afya ya wazee cha Aston kilichoko Birmingham, nchini Uingereza, anachunguza kuhusu jinsi watu wanavyozeeka, na iwapo mchakato wa kibaiolojia wa uzee unaweza kucheleweshwa.

 Dalili za nje za kuzeeka zinafahamika, kama vile kusinyaa kwa mwili na mvi, lakini kuna mambo mengine chini ya ngozi yanayoleta utofauti

Uzee ni mchakato wa kibinafsi sana,  anasema Slack said, na hakuna watu wwaili wanaozeeka sawa. 

 Kuzeeka kusema kweli kunaathiri  nyama katika mwili, anasema. Watu wengi hupata uzoezu wa kile knachoitwa kupungua kwa uwezo wa mwili  kunakotokana na uzee katika maeneo mengi ya mwili wao,  kuanzia ubongo hadi katika mfumo wa uzazi, kadri wanavyozeeka. "   

  Kwahiyo ni vipi tunaweza kuboresha uwezekano wa kuishi miaka 100?

 Iwapo mapacha wanaofanana watawekwa kwenye mazingira tofauti, watazeeka tofauti, anasema  mtafiti, Slacck. Watu sasa wanaishi miaka mingi kuliko  awali, lakini mitindo ya maisha sio ya afya kuliko zamani, "hili ni tatizo tunalohitaji kulitatua".

 Alisema, "Ni jambo linalochosha na lililopitwa na wakati kujaribu  kuendelez akuishi maisha ya afya, kujaribu shughuli za afya kadri unavyoendelea kuzeeka,  kula vye. Usizidishe viwango vya haya yote. Sio kufanya kidogo au sana. Dhibiti kiasi cha pombe unayokunywa, usivute sigara, huo ndio udshauri unaochosha ambao maafisa wa umma wamekuwa wakijaribu kutupatia kwa muda mrefu.”

  La muhimu kwa yote hay ani kuzisaidia seli kujikarabati na kuwa mpya, na pia kupata usingizi wa kutosha. Wanasayansi pia wanajifunza faida za vidhibiti vya uzee vya kufunga kula chakula mara kwa mara.

Ninaweza kuchelewesha uzee?

Ni vigumu kujua ni watu wangapi duniani wanaishi umri wa miaka 100 au zaid. Kitengo cha idadi ya watu cha Umoja wa Mataifa kinakadiria kuwa kutakuwa na watu 573,000 katika mwaka 2021. Shirika hilo linabashiri kuwa idadi hiyo itaongezeka. 

 Dkt  Nir Barzilai ni mkurugenzi wa taasisi ya Uzeekatika Chuo cha tiba cha  Albert Einstein College  cha  New York City na ni mkurugenzi wa Chama cha watafiri wa umri nchini Marekani. 

 Anasema: "Katika maabara yangu, tunashuhudia kila siku mchakato wa kuzeeka ambao unaweza kucheleweshwa na mara nyingine unaweza kusitishwa. Yote haya yanawezekana ," alisema.

 Uwezo wa kwanza wa kuzuwia mchakato wa kuzeeka. Unaitwa  Dorian Gray, mhusika wa kubuni ambaye binafsi hazeeki, lakini anaonyesha kuwa anazeeka. Wapili anaitwa  Wolverine au  Fountain of Youth, ambayo huwafanya watu warudishe nyuma umri na kuwa vijana.  Ni vifumu sana, ni vigumu sana , "ni kitu ambacho kitakuwa kigumu sana tutakachoweza kukifanya ."

 Baadhi ya dawa zinazotia matumaini zinazolenga uzee zimeidhinishwa na mamlaka za viwango na zipo kwa kiasi kikubwa, lakini matibabu mengine, kama vile dawa za kuzuia uzee baada ya kupandikiziwa viungo hazijapatikana. 

 Kuhusu iwapo atashuhudia mafanikio makubwa katika kipindi cha maisha yake katika njanja hii  Dkt  Barzilai  anasema jibu ni ndio inawezekana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wajapan wengi wanazingatia sana ulaji wa vyakula vyenye afya

"Tunza mwili wako "

Robert Waldinger  ni profesa wa afya ya akili katia Chuo kikuu cha   tiba cha Harvard  na mkurugenzi wa Utafiti endelevu katika Harvard katika maendeleo ya makuzi ya watu wazima.

 Utafiti  ulianza 1938, akiwafuatilia wanafunzi wa Harvard . Mwkaa mmoja baadaye, watu wengine masikini 456 waliokulia maeneo ya Boston waliongezwa kwenye utafiti huo.

 Aligundua kuwa watu wenye watu wa kuongea nao na mahusiano bora huishi mika mingi na maisha ya afya zaidi kuliko wale wenye uhusiano na watu wachache 

 

 Alisema mwanzoni watu 724 walishiriki katika utafiti wake, lakini karibu wote walifariki, lakini pua kulikuwa na wachache chini ya 50, walioishi katika wakiwa na miaka 90 na ushee, baadhi yao hata waliishi zaidi ya miaka 100. 

 

Je ni vipi upweke unaathiri  maisha marefu?

 Kuna tafiti nyingi katika eneo hili kwa sasa, anasema Waldinger. Maelezo bora ni kwamba hii inahusiana na msongo wa mawazona udhibiti wa msongo huu. Fikiria kuhusu hilo, iwapo una hasira au mazungumzo magumu mchana, unaweza kuhisi umechoka kimwili. Lakini unapokuja nyumbani na kuongea na mtu  fulani, ambaye yuko tayari kukusikiliza, unaweza kuhisi mwili wako umetulia. "Tunaamni kwamba wale ambao ni wapweke zaidi huwa hawatulii. Miili yao kila wakati huwa inakabiliwa na  mchoko unaotokana na msongo wa mawazo.  Hiyo inaansha kuwa viwango vya juu vya homoni za msongo huzunguka, na kusababisha maumivu ya kudumu na hatimaye kuharibu mifumo ya miili yao. Kwahiyo, baadhi ya tafiti, zinaonyesha kuwa kuwa na mahusiano mazuri husaidia kudhibiti msongo wa mawazo."

 Lakini mahusiano kweli ni muhimu katika kumsaidia mtu kuishi miaka mingi? Tunafahamu kuwa kuna watu ambao huwa wanapenda tu kuwa peke yao na wako tu sawa.

 Kwa hili, jibu la Waldinger ni kwamba kuna watu wa aina hiyo . "Baadhi ya watu ni wakimya asilia—hilo sio tatizo, baadhi ya watu hupenda kuzungumza. Kuna watu wengi wanaowazingira, kuna shinikizo kwa wakimya, na labda wanahitaji mtu mmoja au wawili tu wa kuongea nao walio karibu yao . Hicho ndicho wnachokihitaji, ndicho wachokitaka Ndio, ni vyema kwao. Hakuna njia moja tu ya kuishi maisha ya afya.

 

 Ushauri wa Profesa Robert Waldinger ni : "Utunze mwili wakona kila mara kumbuka kwamba unaweza kuhitaji kuishi miaka 100."