Ni njia zipi hatari zaidi za wahamiaji duniani?

wahamiaji

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa, linakadiria kuwa tangu 2014 takriban wahamiaji 50,000 wamefariki au kutoweka walipokuwa wakijaribu kufika marekani au katika Muungano wa Ulaya

Maafa mawili mabaya ambayo yameathiri watu wanaojaribu kuvuka mipaka ya kimataifa katika muda wa siku chache.

Siku ya Ijumaa, takriban watu 23 walikufa wakati umati mkubwa ulipojaribu kuvuka uzio wa mpaka kutoka Morocco na kuingia katika eneo la Melilla Afrika Kaskazini nchini Uhispania.

Waligundua miili ya watu wasiopungua 46 ndani ya lori lililotelekezwa.

Hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo, wataalam wanaonya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), linakadiria kuwa tangu mwaka 2014 karibu wahamiaji 50,000 wamekufa au kutoweka wakijaribu kufika nchi kama Marekani au Umoja wa Ulaya.

Shirika hilo linaamini kwamba idadi halisi yawatu wanaokufa au kutoweka huenda ikawa juu zaidi. 

 Lakini ni njia zipi hatari zaidi duniani kwa wahamiaji? Na kwa nini?

Mediteranea ya kati

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

njia ya Katikati mwa Bahari ya Mediterraneaninafahamika kama njia hatari zaidi duniani

Kulingana na IOM, hii ni njia hatari zaidi duniani kwa wahamiaji. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 19,500 wamekufa wakijaribu kuvuka bahari ya  Mediterranea kutoka Afrika Kaskazini kwenda Ulaya tangu mwaka 2014.

Jaribio la kuvuka mara nyingi hufanywa kwa kutumia maboti ya kujitengenezea katika mazingira msongamano mkubwa watu.

Boti hizo mara nyingi huendeshwa na makundi ya kihalifu na walanguzi wa watu. 

Tunisia, ambayo kando na Libya ni kitovu kikuu cha wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya kupitia njia ya kati ya Mediterania, kuna hata makaburi yaliyohifadhiwa wale wanaozama baharini.

"Kuona makaburi haya hapa kunanifanya nijisikie huzuni sana," Vicky, mhamiaji wa Nigeria anayetarajia kufunga safari kutoka Tunisia, aliliambia shirika la habari la AFP alipokuwa akizuru makaburi hayo.

"Ninapoona hivi ],Sina hakika tena kama nataka kuvuka bahari," aliongeza.

Mashirika kama IOM yanahofia kwamba wahamiaji wengine hawatakatishwa tamaa. "Kuondoka kwa wahamiaji kwenye Mediterania ya kati kunaendelea. Jambo la kutia wasi wasi zaidi ni idadi kubwa ya vifo vinavyoendelea kwenye kivuko hiki hatari zaidi duniani.

Inaendelea kupoteza maisha kwa kukosekana hatua madhubuti za mataifa," anasema Safa Msehli, msemaji wa IOM.

Njia za ndani za Kiafrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kivuko cha Sahara ni hatari kuu kwa wahamiaji wanaojaribu kufika Afrika magharibi

Kwa wahamiaji wengi wa Kiafrika, ndoto ya kufika Ulaya huanza na safari kupitia bara lao ambayo mara nyingi inahusisha kuvuka kwa muda mrefu kwenye Jangwa la Sahara kuelekea nchi za Afrika Kaskazini.

Hali mbaya ya mazingira ni tishio kubwa: IOM inakadiria kuwa kivuko cha Sahara kilisababisha vifo vya karibu watu 5,400 kati ya mwaka 2014 na 2022.

"Jangwani unaona watu wakifa. Baadhi yao kwa ajili ya kwa kukosa nguvu, walifia huko. Wengine, kwa ajili kuishiwa na maji ya kunywa," mhamiaji Abdullah Ibrahim, aliliambia shirika la habari la AFP kuhusu uzoefu wake wa kuvuka.

Tishio jingine kubwa kwa wahamiaji ni watu wengi wanaosafirisha magenge yanayofanya kazi katika eneo hilo.  

"Ghasia mikononi mwa wasafirishaji, wasafirishaji na maafisa wa mpaka katika eneo hilo pia huchangia sehemu kubwa ya vifo vilivyorekodiwa kwenye njia za wahamiaji katika Jangwa la Sahara," IOM ilisema katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu suala hilo.

Kivuko cha mpaka wa Marekani -Mexico

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wahamiaji wakijaribu kuvuka kwenye mpaka wa Marekani na Mexico Mwakitumia njia nyingi, lakini baadhi hujaribu kufanya safari hiyo kwa miguu

Ijapokuwa nija zote za uhamiaji  katika eneo la Amerika hazifiki Marekani, ni lengo kuu wa wengi wa watu wanaopania kutafuta makazi mapya katika eneo hilo.

Mpaka kati ya Marekani na Mexico una changamoto zake: eneo hilo ni maarufu kwa jiografia yake isiyo nzuri, ikijumuisha maeneo ya jangwa, na wahamiaji mara nyingi hujaribu kuvuka hadi Marekani kupitia mto hatari wa Rio Grande unaopita kwenye sehemu ya mpaka.

Kufa maji ni moja ya sababu kuu ya vifo katika njia hii ambayo, IOM inakadiria imeangamiza zaidi ya watu 3,000 tangu mwaka 2014.

Wale wanaojaribu kuepuka hatari za asili, kwa kujificha kwenye magari, wanakabiliwa na hatari tofauti kama zile zilizosababisha vifo huko San Antonio.

"Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengine ya kupoteza maisha katika njia za wahamiaji kuelekea Marekani," anasema Safa Msehli, msemaji wa IOM.

Mnamo Desemba 2021, wahamiaji 56 walikufa huko Chiapas, Mexico baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali.

Njia za Asia

Chanzo cha picha, Getty Images

IOM inasema kuwa zaidi ya wahamiaji 4 kati ya 10 kote duniani mwaka 2020 walizaliwa barani Asia, na bara hilo lina njia kadhaa kuu za wahamiaji.

Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa, karibu watu 5,000 wamefariki au kupotea barani Asia katika kipindi cha miaka minane iliyopita.

Baadhi ya vifo hivyo vinahusisha wahamiaji wa Rohingya na Bangladesh wanaotumia njia za baharini zinazovuka Ghuba ya Bengal na Bahari ya Andaman hadi katika nchi jirani, au hata hatimaye kufika Ulaya.Hali ngumu wanayokumbana nayo wakati wa kuvuka inakuwa mbaya zaidi.

''Tuna njaa,Sikuweza kunywa, hakukuwa na maji ya kunywa. Hakukuwa na chakula, hakuna wali, hatukuweza kula. Ilikuwa hivyo baharini kwa muda wa mwezi mmoja," Muhammad Ilyas, mkimbizi wa Rohingya mwenye umri wa miaka 37, aliambia shirika la habari la AFP baada ya kuokolewa na jeshi la wanamaji la India kufuatia kuharibika kwa boti aliyokuwa akisafiria.

Kama ilivyo kwa njia zingine, wahamiaji hawa pia mara nyingi huwa waathiriwa wa dhulma za magenge ya wasafirishaji wa watu.