Afya: Jizoeze kuangalia haja kubwa yako, unaweza kuokoa maisha yako

Stool

Chanzo cha picha, Getty Images

"Angalia haja kubwa yako."

Huo ndio ujumbe mzito uliotolewa katika kampeni yake ya uhamasishaji kuhusu saratani ya utumbo mpana na mtangazaji wa BBC Deborah James, ambaye aliugua na kufariki wiki jana.

Deborah James, mtangazaji wa BBC ambaye alifanya vita yake dhidi ya saratani kuonekana, afariki akiwa na umri wa miaka 40. Lakini saratani hii, pia inaitwa saratani ya matumbo au koloni ni nini, na jinsi ya kuigundua mapema? Hapa tunakupa mwongozo wa vitendo. Unawezaje kugundua saratani ya koloni?

Kuna ishara kuu tatu za kuzingatia:

 • Kinyesi kuwa na damu bila sababu dhahiri. Inaweza kuwa nyekundu au damu ya mzee.
 • Mabadiliko katika njia ya kinyesi, kama vile kwenda kujisaidia mara nyingi zaidi au kinyesi kuwa chepesi au kigumu zaidi.
 • Kuhisi maumivu au uvimbe kwenye tumbo la chini.

Kunaweza pia kuwa na dalili nyingine kama vile:

 • Kupungua uzito.
 • Unahisi kuwa haujamaliza vizuri kujisaidia hata baada ya kutoka kujisaidia.
 • Unahisi uchovu au kizunguzungu kuliko kawaida.

Kuwa na dalili hizi haimaanishi kuwa ni saratani ya matumbo, lakini ushauri ni kumuona daktari ikiwa utazigundua kwa wiki tatu au zaidi na ikiwa haujisikii vizuri.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa sababu saratani inapogunduliwa mapema, ni rahisi zaidi kutibu. Wakati mwingine saratani ya utumbo mpana inaweza kuzuia uchafu kupita kwenye utumbo na hii inaweza kusababisha kuziba, na kusababisha maumivu makali ya tumbo, kuvimbiwa na magonjwa.

Utahitaji kumuona daktari wako au kwenda kwa ER mara moja katika hali hizi.

Angalia vizuri kile kinachotoka unapoenda chooni kujisaidia na usione aibu kusema. Unapaswa kuangalia damu kwenye kinyesi na vile vile kutokwa na damu kutoka kwa fandasi.

Damu nyekundu inaweza kutokea kutokana na mishipa ya damu iliyovimba (hemorrhoids) kwenye njia ya haja kubwa, lakini inaweza pia kusababishwa na saratani ya utumbo mpana.

Unaweza pia kugundua mabadiliko katika tabia ya matumbo, kama vile kinyesi laini au kujisaidia mara nyingi zaidi kuliko kawaida.

Nawezaje kuangalia kinyesi changu?

Angalia vizuri kile kinachotoka unapoenda chooni kujisaidia na usione aibu kusema. Unapaswa kuangalia damu kwenye kinyesi na vile vile kutokwa na damu.

Damu nyekundu inaweza kutokea kutokana na mishipa ya damu iliyovimba (hemorrhoids) kwenye njia ya haja kubwa, lakini inaweza pia kusababishwa na saratani ya utumbo mpana.

Unaweza pia kugundua mabadiliko katika tabia ya matumbo, kama vile kinyesi laini au kujisaidia mara nyingi zaidi kuliko kawaida.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni nini husababisha saratani ya utumbo mpana?

Hakuna mtu aliye na uhakika ni nini hasa husababisha, lakini kuna mambo machache ambayo yanaweza kuwa sababu:

Unapokuwa mkubwa, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba saratani itaonekana na katika utumbo sio tofauti: kesi nyingi ni kwa watu wazima zaidi ya umri wa miaka 50.

 • Kula chakula chenye nyama nyekundu na nyama iliyochakatwa.
 • Kuvuta sigara kunaweza kuongeza hatari ya aina nyingi za saratani.
 • Kunywa pombe kupita kiasi.
 • Kuwa na uzito mkubwa au unene.
 • Kuwa na historia ya 'polyps' kwenye utumbo ambayo inaweza kuendeleza kuwa uvimbe.

Je, inarithiwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto?

Katika hali nyingi, saratani ya utumbo mpana sio ya kurithi, lakini unapaswa kumwambia daktari wako ikiwa una jamaa wa karibu waliogunduliwa kuwa nayo kabla ya umri wa miaka 50.

Baadhi ya hali kama kuwa na ugonjwa wa 'Lynch', hukuweka katika hatari kubwa zaidi ya kupata saratani hii, lakini pia zinaweza kuzuiwa ikiwa madaktari wanajua kuhusu hali hiyo.

Jinsi ya kupunguza hatari?

Zaidi ya nusu ya saratani ya matumbo inaweza kuzuiwa ikiwa watu walifuata mtindo bora wa maisha, wanasayansi wanasema.

Hiyo inamaanisha kufanya mazoezi zaidi, kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi na mafuta kidogo, na kunywa glasi sita hadi nane za maji kwa siku.

Lakini pia inamaanisha kwamba umuone daktari kama una dalili zozote za kutisha na kupata vipimo vya uchunguzi wa saratani mara tu zinapotolewa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, saratani ya utumbo mpana hutambuliwaje?

Inaweza kuwa kwa njia ya colonoscopy, utaratibu kuwekwa kamera ndani ya mirija mirefu kuangalia ndani ya utumbo mzima, au sigmoidoscopy flexible, ambayo inaonekana katika sehemu ya utumbo.

Zaidi ya 90% ya watu waliogunduliwa na saratani ya utumbo mpana katika hatua ya awali wataishi kwa miaka mitano au zaidi, ikilinganishwa na 44% ya wale waliogunduliwa katika hatua za mwisho mwisho.

Nafasi za kuishi zimeongezeka zaidi ya mara mbili katika miaka 40 iliyopita: zaidi ya nusu ya wagonjwa sasa wanaishi miaka 10 au zaidi, ikilinganishwa na mmoja kati ya watano katika miaka ya 1970, kulingana na takwimu za Uingereza.

Ni matibabu gani yanapatikana?

Saratani ya utumbo mpana inatibika hasa ikigundulika mapema. Matibabu yanakuwa ya kibinafsi zaidi, na maendeleo katika upimaji wa 'kijeni' yanamaanisha kuwa utunzaji unaweza kumuhusu tu mmoja mmoja.

Njia hii bado inahitaji urekebishaji mzuri, lakini intoa miaka ya ziada ya maisha kwa watu walio na saratani.