Mikakati mitatu ya NATO kukabiliana na Urusi na China

Joe Biden

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano na waandishi wa habari siku ya mwisho ya Mkutano wa NATO mjini Madrid, Uhispania.

NATO imetangaza mpango wake mpya katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ndani ya mfumo wa mkutano wa kilele uliofanyika Juni 29 na 30 huko Madrid, Uhispania.

Mradi huo unajumuisha uwepo mkubwa zaidi wa wanajeshi wa Marekani barani Ulaya, hasa mashariki mwa bara hilo, pamoja na kifurushi cha usaidizi cha kina kwa Ukraine, ambacho kinajumuisha mafuta, vifaa vya matibabu, fulana zisizo na risasi na mifumo ya kuzuia ndege zisizo na rubani.

Shirika hilo la kijeshi pia lilitoa taarifa juu ya ‘’mkakati wake,’’ nyaraka ambayo inaweka mkakati wake wa kijeshi na usalama kwa miaka 10 ijayo, ikielezea kwa undani vitisho vinavyokabili demokrasia ya Magharibi na kuelezea jinsi nchi za Magharibi zinakusudia kukabiliana navyo.

Ni maandishi ambayo yanabadilisha kwa haraka maono kuhusu uhusiano wake na China na Urusi.

Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) ni muungano wa kijeshi wa kujihami ulioanzishwa mwaka 1949 na nchi 12, zikiwemo Marekani, Canada, Ufaransa na Uingereza.

Wanachama wake walikubali kuja kusaidiana katika tukio la shambulio la silaha dhidi ya nchi yoyote mwanachama.

Ni miaka michache tu iliyopita ilishutumiwa kwa kutekeleza unyama wa mateso katika ‘’ubongo hadi mtu anafariki’’, lakini imeibuka tena, ikionyesha umoja na mshikamano mkubwa, baada ya uvamizi wa Ukraine ulioamriwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Moscow pia inaiona NATO kama tishio na iliishutumu Jumatano kwa kuwa na ‘’matamanio ya kifalme’’ na kujaribu kusisitiza ‘’ukuu’’ wake kupitia mzozo wa Urusi-Ukraine.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani Joe Biden alisisitiza kwamba NATO ‘’inahitajika zaidi sasa kuliko hapo awali’’.

Pia unaweza kusoma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan awali alikuwa akipinga Finland na Sweden kujiunga na NATO, lakini msimamo wake umebadilika katika siku za hivi karibuni.

Muungano huo umepitia mapitio yake makubwa zaidi tangu Vita Baridi huko Madrid katika siku za hivi karibuni, kulingana na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.

Katika makala haya tunaangazia ambo matatu kueleza mkakati mpya wa muungano mkubwa zaidi wa kijeshi ulimwenguni unajumuisha nini.

1. Ongezeko la matumizi ya fedha na kijeshi

Kulingana na mwandishi wa BBC wa masuala ya ulinzi Frank Gardner, uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeipa NATO ‘’mshtuko wa volti 50,000.

Moja ya matokeo ya moja kwa moja ya ‘’tishio’’ la Urusi ni kwamba baadhi ya nchi katika muungano zimekubali kutumia pesa nyingi katika ulinzi.

 Uingereza imeahidi kuongeza matumizi hadi sawa na 2.5% ya Pato la Taifa ifikapo 2030 na imeonyesha kuwa itawashinikiza washirika wengine wa Magharibi pia kuongeza bajeti yao, Waziri Mkuu Boris Johnson alisema.

Kwa upande wake, Marekani ilitangaza kwamba itaongeza uwepo wake wa kijeshi kote Ulaya katika kukabiliana na uvamizi huo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

NATO itaongeza bajeti na idadi ya wanajeshi barani Ulaya.

Wakati wa mkutano huo katika mji mkuu wa Uhispania, Biden alitangaza kwamba umoja huo ‘’utaimarishwa katika pande zote, katika nyanja zote: ardhi, anga na bahari’’.

Mpango huo mpya unatoa wito kwa zaidi ya wanajeshi 300,000 kuwa tayari sana mwaka ujao, zaidi ya 40,000 waliopo hivi sasa.

Makao makuu ya kijeshi ya kudumu pia yataundwa nchini Poland, huku Marekani ikituma meli mpya za kivita nchini Uhispania, ndege za kivita nchini Uingereza na wanajeshi wa ardhini nchini Romania.

Biden alisisitiza ahadi ya muungano huo ‘’kutetea kila inchi’’ ya eneo lake.

‘’Tunamaanisha tunaposema kuwa shambulio dhidi ya mtu mmoja ni shambulio dhidi ya wote,’’ alisema.

2. Urusi: kutoka kwa mshirika hadi tishio

Kwa mujibu wa dhana mpya ya kimkakati ya NATO, Shirikisho la Urusi ni ‘’tishio kubwa zaidi na la moja kwa moja kwa usalama wa washirika na kwa amani na utulivu wa Magharibi.’’

Nyaraka hiyo inaonyesha kuwa muungano wa kijeshi hauwezi tena kuichukulia Urusi kama mshirika, lakini utaendelea kuwa ‘’tayari kuweka njia za mawasiliano na Moscow’’ ili kuepusha kuongezeka kwa mzozo.

NATO imesema haiwezi kuondoa uwezekano wa shambulio dhidi ya mamlaka na ukamilifu wa eneo la washirika wowote.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Katika mkutano wa Madrid, viongozi wake walikubali maombi ya uanachama yaliyowasilishwa hivi karibuni na Finland na Sweden, majimbo mawili ya Nordic ambayo hayakuegemea upande wowote

Uanachama wake lazima uidhinishwe na serikali za wanachama 30 wa shirika.

Putin alionya Jumatano kwamba ikiwa Funland na Uswidi zitakubali wanajeshi wa NATO na miundombinu ya kijeshi kwenye eneo lao, Moscow itajibu ‘’kwa ulinganifu.’’

Alitarajia kwamba nchi yake ingelazimika ‘’kuwa na vitisho vivyo hivyo katika eneo ambalo vitisho dhidi yetu vimewekwa.

Kujiunga kwa Helsinki na Stockholm kwa NATO kungeashiria moja ya mabadiliko makubwa katika usalama wa Ulaya katika miongo kadhaa.

3. China ni ‘’changamoto’’

Mkakati wa shirika hilo pia umebainisha China kwa mara ya kwanza kama ‘’changamoto ya kimfumo kwa usalama wa Euro-Atlantic.’’

Stoltenberg alisema Jumatano kwamba muungano huo sasa unakabiliwa na ‘’zama za ushindani wa kimkakati.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi

‘’China inaongeza kwa kiasi kikubwa nguvu zake, ikiwa ni pamoja na silaha za nyuklia, na kuwatisha majirani zake, ikiwa ni pamoja na Taiwan,’’ aliongeza.

‘’China sio adui wetu, lakini ni lazima tuwe macho kuhusu changamoto kubwa inazoleta.’’

Katika mkakati wa NATO ambao ulikubaliwa mwaka 2010 China haikutajwa.

Lakini maandishi mapya yanabainisha kuwa sera za Beijing zinapinga maslahi, usalama na maadili ya shirika.

‘’Operesheni mbaya za PRC na kimtandao na matamshi yake ya makabiliano na habari potovu yanalenga washirika na kudhuru usalama wa muungano,’’ waraka ulisema.

NATO inaonya zaidi kwamba serikali ya China ‘’inapanua kwa haraka’’ uwezo wake wa nyuklia bila kuongeza uwazi au kujihusisha na udhibiti wa silaha kwa nia njema.

Hii sio tu wasiwasi kwa wanachama wa NATO, lakini pia nchi jirani za Asia na Oceania.