Kutekwa nyara kwa ndege kulivyosababisha kuuawa kwa kaka wa Waziri Mkuu wa Israel

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo Juni 27, 1974, ndege ya abiria kutoka mji mkuu wa Israeli Tel Aviv hadi Paris ilitekwa nyara na wanaume wanne na kuwapeleka Uganda.

Kulikuwa na watu 250 kwenye ndege hiyo, iliyomilikiwa na Air France, yenye nambari ya 139.

Abiria 100 hivi walikuwa Wayahudi, na ndege hiyo ilikuwa ikielekea Athens, Ugiriki.

Ilipotua Athens, abiria zaidi  waliingia ndani ya ndege , na kuwafikia watu 58 wakiwemo watekaji nyara wanne.

Muda mfupi baada ya kupaa, watekaji nyara hao walielekeza ndege hiyo hadi Benghazi, Libya, baada ya kujaza mafuta kwa saa kadhaa kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Ndege hiyo ilitua Uganda Juni 28, chini ya  utawala wa Idi Amin.

Utekaji nyara huo uliamriwa na Wadi Haddad, mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PFLP-EO).

Operesheni hiyo ya utekaji nyara pia ilihusisha wanachama wawili wa kundi la waasi wa mrengo wa kushoto wa Ujerumani.

Watekaji nyara hao walitaka kuachiliwa kwa wanamgambo 40 wanaoshikiliwa na Israel na wengine 13 wanaozuiliwa katika nchi nyingine nne.

Wanachama 53 waliotakiwa kuachiliwa walikuwa kutoka Israel, Ufaransa, Ujerumani, Uswizi na Kenya.

Rais wa Uganda Idi Amin pia alijiunga na kundi hilo, akiwasaidia silaha na wanajeshi.

Unaweza pia kusoma

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya abiria wote waliotekwa nyara kuhamishiwa katika uwanja wa zamani wa a Ndege wa Entebbe, watekaji nyara waliwatenganisha abiria -Waisraeli na Wayahudi kutoka nchi nyingine.

Mara tu serikali ya Israel iliposikia utekaji nyara huo, mipango ya kijeshi ilizinduliwa kukabiliana nao watekaji nyara hao .

Watekaji nyara hao walisema iwapo watu wao hawataachiliwa wangewaua abiria wote kufikia Julai 1, mwendo wa saa mbili usiku.

Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barak alikuwa kamanda mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Idara yake iliagizwa kuandaa mpango wa uokoaji.

Aliambia BBC kuwa tayari kulikuwa na  mvutano katika uongozi wa kisiasa wa Israel, ambao walikuwa wakifikiria maamuzi yanayoweza kutokea.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo Juni 30, matumaini yalififia baada ya kundi hilo kuwaachilia watu 47 wasio Waisraeli ambao walipelekwa Paris.

Mara moja wanachama wa timu ya kijasusi ya Israel ya Mossad walitumwa mjini Paris kukusanya taarifa kuhusu walioachiliwa.

Waziri Mkuu Barak alisema mambo mawili muhimu yalisaidia kupanga shughuli ya uokoaji.

"Moja ni kwamba tuligundua kuwa jeshi la Uganda lilikuwa sawa kabisa na watekaji nyara, na lingine ni kwamba tulikuwa na habari nyingi juu ya jengo la zamani la uwanja, ili tuchukue hatua," alisema.

Jinsi ndege ilivyotekwa nyara

 

Huku kukiwa hakuna uamuzi wa mwisho juu ya operesheni ya uokoaji kufanywa, wakati muda wa kuwakamata watekaji nyara mnamo Julai 1 ukikaribia, maafisa wa Israeli walitangaza kuwa wako tayari kufanya mazungumzo.

Kwa sababu hiyo, watekaji nyara waliongeza muda wa mwisho, ambao waliweka tarehe 4 Julai. Pia waliachilia  watu wengine 101.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mnamo Julai 3, Baraza la Mawaziri la Israeli liliidhinisha operesheni. Saa chache baadaye kikosi kazi kiliondoka.

Hakuna aliyejua kwamba makomando 200 walikuwa wamesafiri kwa ndege nne kutoka Israel, wakisafiri maili 2,500, hadi walipofika uwanja wa ndege wa Entebbe.

Ndege hizo ziliruka pande mbalimbali, bila shaka, na kuruka kwa urefu wa chini hadi futi 100 juu ya Bahari Nyekundu, ili kutoroka rada kutoka Misri na Saudi Arabia.

Mpango ulikuwa kwa timu ya waokoaji ya Israeli kusafiri hadi eneo la ujenzi kwa lori.

Awali makomando wa Israel walipigana na wanajeshi wawili wa Uganda, ambao waliwaua walipokuwa wakijaribu kukabiliana na jeshi la Israel.

Waliingia ghafla kwenye jengo walilokuwa watekaji nyara.

Kuuawa kwa kaka wa Benjamin Netanyahu

Israel inasema vikosi vyake viliwaua watekaji nyara saba na wanajeshi 20 wa Uganda ndani ya dakika chache, na kuwaokoa watu wao.

Kwa upande wa Israel, ni Kanali Jonathan Netanyahu tu, kamanda wa kikosi cha uokoaji na mtu aliyepanga operesheni hiyo, ndiye aliyeuawa.

Jonathan alikuwa kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli.

Kwa heshima ya kazi iliyofanywa na kakake Benjamin Netanyahu, Operesheni hiyo  iliitwa "Operesheni Jonathan".

Maafisa wa Israel wanasema waliokoa zaidi ya watu 100 bila masharti kutoka  kwa watekaji nyara.

Miaka 40 baadaye, mnamo 2016, Waziri Mkuu wa wakati huo wa Israeli Benjamin Netanyahu alitembelea eneo la operesheni ambayo kaka yake aliuawa.