Je kuna unyanyasaji wa kingono katika shirika la Umoja wa Mataifa?

Martina

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Martina Bostrom, mshauri wa zamani wa UNAIDS aliiambia BBC kuwa alinyanyaswa kingono kazini

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa amesema  ripoti za unyanyasaji wa kingono na ufisadi katika Umoja wa Mataifa zinapaswa kuchunguzwa na jopo la wataalamu bila kuchelewa.

Kauli za Purna Sen zinakuja baada ya uchunguzi wab BBC kuhusu unyanyasaji wa kingono katika Umoja wa Mataifa ambao ulifichua kuwa wafanyakazi kadhaa wa umoja huo wamefukuzwa kazi kwa kujaribu kuripoti unyanyasaji huo. 

Kulingana na Purna Sen, Umoja wa Mataifa unapaswa’’kuchukua hatua’’ na kukubali mapendekezo yote yaliyotolewa na jopo. 

Msemaji wa Umoja wa Mataifa aliiambia BBC kwamba shirika hilo linashugulikia usalama wa wale walioripoti unyanyasaji.

Uchunguzi huo wa BBC unaitwa "Ufichuzi :Mtazamo ndani ya Umoja wa Mataifa  ." unadai kuwepo kwa ufisadi,utovu wa nidhamu na unyanyasaji wa kingono ndani ya Umoja wa mataifa.

Maafisa waliojaribu kutoa madai hayo waliiambia BBC kwamba wameadhibiwa na kufutwa kazi kwasababu walizungumza wazi. 

Maelezo ya picha,

Purna Sen: "ni kwanini Katibu mkuu 'anatia chumvi, nini tunachojua? Nini ukweli

Kulingana na na maelezo ya  Purna Sen aliyoyatoa katika makala ya BBC,wanawake wanaofanya kazi katika Umoja wa Mataifa  "walifuatwa, walibakwa na kubakwa tena."Uliteuliwa mwaka 2018 kama Waziri wa nchi wa masuala ya demokrasia , unyanyasaji na ubaguzi. "Kadiri wanaume wanavyokufa kwa ajili ya kile wanachokifanya, wanakifanya zaidi," anasema.

Aliongeza kuwa hatashangazwa na kwamba ripoti ya BBC  " ni ya kusikitisha sana" aliiambia BBC Newsnight.

"Inaonyesha kwamba kulikuwa na hofundani ya Umoja wa Mataifa," alisema

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Madai ya dhidi ya  Dr. Luresh yalichunguzwa, lakini shirika la Umoja wa Mataifa halijaweza kuzungumzia kuhusu madai hayo ," Umoja wa Mataifa.  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres alitaka kuweka tume inayojumuisha wataalamu mbali mbali kutathmini matukio  ya wafanyakazi na kupendekeza hatua zinazoweza kuchukuliwa. 

Utawala wa Guterres  ulisema katika taarifa kwamba uko wazi kwa jaribio lolote la kuundwa kwa kamati ya nje "kushugulikia ukiukaji wowote ."

Msemaji wa Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa  Ban Ki-moon, Stephane Dujarric, alikiambia kipindi cha BBC cha  Newshour kwamba Katibu Mkuu alikuwa " amelichukulia hili kwa umakini sana tangu alipochukua mamlaka ".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

BBC imepokea sauti za siri zilizorekodiwa. Kielelezp

kinga ya kidiplomasia

Hadhi ya kisheria ya Umoja wa Mataifa imelindwa. Maafisa wa ngazi ya juu wana kinga. Umoja wa Mataifa unalindwa dhidi ya sheria za taifa lolote.

Hakikisho hilo linatolewa kwa umoja huo ili kuulinda dhidi ya uingiliwaji wa shughuli zake. Hatahivyo, kulingana na Umoja wa Mataifa, hakikisho hili halisaidii maslahi ya wafanyakazi wake. Kwahiyo, hauwalindi wale waliotekeleza uhalifu kama vile wa unyanyasaji wa kingono. 

BBC imepokea sauti za siri zilizorekodiwa. Inaonyesha kuwa maafisa ICC wakati wote hawafanyi kazi yao ipasavyo. Mkurugenzi wa upelelezi anasikika akiongea katika mkutano wa wafanyakazi. Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa alisema hakuweza kujizuia kutoa machozi  na kuelezea jinsi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyoweka mkono katika nguo yake ya ndani. 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

jengo la Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa ina wasaidizi kadhaa wa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

 Katika sauti iliyorekodiwa, Svenson alisema alikuwa ameripoti madai ya unyanyasaji wa kingono kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na maafisa wengine wa ngazi ya juu, lakini mdomo wake ulifungwa haraka.   

 "Ninadhani shirika limezama katika ufisadi," alisema Peter Gallo’’

Peter Gallo ni mwanaume ambaye alishirikisha BBC sauti iliyorekodiwa. "Nilifanya kazi kama mchunguzi katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini  New York. Kutokana na uzoefu wangu, ninaamini kwamba shirika hili limezama katika ufisadi, ”alisema katika makala ya BBC.

Ofisi ya  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ilisema kuwa shirika hilo liko tayari''kumuadhibu mgfanyakazi, awe mwenye umri mdogo au umri mkubwa, aliyehusika na unyanyasaji wa kingono ."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Antonio Guterres

Martina Bostrom, mshauri wa zamani wa UNAIDS, pia aliimbia BBC kwamba alinyanyaswa kingono kazini.

"Unyanyasaji wa kingono, unyonyaji na unyanyasaji wa kingono vinafanyika katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Inatokea wakati wa saa za kawaida za kazi, kila mahali, ”alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Martina Bostrom: "Nilimuamba akome na kuniacha niende"

Alisema alilengwa na Luis Luresh. Luresh alikuwa Naibu Mkurugenzi  Mtendaji na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  wa  UNAIDS. Martina alimuita  Luresh " ‘sura mweusi" na akasema kuwa alifahamika kwa tabia yake mbaya.

Alisema baada ya tukio la kazi mjini Bangkok katika mwaka 2015, Luresh falimbusu kwa nguvu katika rift . Halafu alijaribu kumvuta kumpeleka ndani ya chumba chake.  

 "Nilimuomba aache kufanya hivyo na aniache niondoke," alisema. Ilibidi nifunge mlango ili niendelee kubakia ndani ya rift. 

Katika mwaka 2018, Luis Luresh aliondoka katika Umoja wa Mataifa. Alipongezwa kwa ‘’kazi nzuri aliyoifanyia Umoja wa Mataifa kwa miaka 22’’ "Sijawahi kamwe kumpiga au kumnyanyasa yeyote," alisema. Madai hayana msingi, ”aliiambia BBC.

Agosti, 2021, Martina alipokea barua kutoka Umoja wa Mataifa. Katika barua hiyo, Umoja wa Mataifa ulikiri kuwa martina, amekuwa  "akinyanyaswa kingono kwa muda mrefu." Hatahivyo, katika mwaka 2015, kuhusiana na ripoti ya unyanyasaji wa kingono, shirika hilo lilisema kuwa  "kitu fulani cha kusikitisha kilitokea kwako, ambacho umekielezea mara kwa mara katika maelezo ya hali yako," lakini matokeo  "hayakidhi viwango vya ushahidi." 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kulingana na Purna Sen, kisa cha Martina ni dalili ya tatizo kubwa katika Umoja wa Mataifa 

Kulingana na  Purna Sen, kisa cha Martina ni dalili ya tatizo kubwa katika Umoja wa Mataifa  symptom.

Kulingana na makala ya BBC, mtu mmoja kati ya watatu ’’la kushangaza’’ Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walisema wamekuwa wakinyanyaswa kingono kazini. Hatahivyo visa vingi hafikufichuliwa.

Taarifa kutoka katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ilisema: "Kumekuwa na mafanikio makubwa katika kupambana na unyanyasaji wa kingono…Hakuna shirika ambalo linaweza kuepuka hilo. ”

Taarifa hiyo ilisema kuwa hatua kama vile kuwaajiri wapelelezi wa kike, kuwasiliana na wafanyakazi ili waripoti unyanyasaji, na mafuzo bora ya utawala vimejumuishwa. 

Lakini katika mahojiano na BBC Newsnight, Purna Sen alisema makala ilishindwa kuonyesha iwapo kuna  ahadi ya kutovumilika kwa vitendo hivyo na kwamba "bado kuna kazi zaidi siku zijazo."

"Umoja wa Mataifa umeweza kutatua matatizo yake makubwa siku za nyuma," alisema. Lakini haukufanya vya kutosha. Niliona vitu vya kutisha.Wanaweza na wanapaswa kutatua masuala haya haraka. Sio tu kwa maneno. ” Alisema

Unaweza pia kusoma: